Kuapishwa kwa Joe Biden: Hotuba yake yasisisitiza bila umoja -haitakuwa rahisi

Iliyochapishwa

Saa sita na dakika moja, katikati ya hotuba ya kuapishwa kwake Joe Biden kuwa rasmi rais wa 46 wa Marekani.

Alikuwa tayari ameelezea kazi ngumu iliyo mbele yake yeye na taifa kwa ujumla - katika kile alichokiita "majira ya baridi ya hatari"

Marekani inakabiliwa na janga baya la Covid -19 ambalo limesababisha vifo vya watu wengi na kufungwa kwa biashara, mazingira ya kutisha, vilio vya dharura vya haki za kijamii na kuongezeka kwa uhasama katika "itikadi kali za kisiasa, ukuu wa wazungu na ugaidi wa ndani ya nchi ".

Hotuba yake haikuwa ya mapendekezo wala suluhu.

Hayo yaliwekwa kando kwa ajili ya nyaraka zilizotolewa mapema leo asubuhi zikiainisha sheria au amri zake 17 za kwanza kama rais- kuhusu uhamiaji, mabadiliko ya hali ya hewa, haki za wapenzi wa jinsia moja na waliobadili jinsia (LGBT) na afya ya umma miongoni mwa nyingine.

Badala yake, Biden alitumia hotuba yake kutoa matumaini - na kutoa wito, wakati mwingine kwa msisitizo, kwamba nchi lazima iungane katika kukabiliana na changamoto zilizopo, kwamba lazima iache kipindi cha sasa "vita visivyo vya kiraia ".

"Bila umoja, hakuna amani, ni chuki na hasira ," alisema. "Hakuna mafanikio, ni uchovu wa hasira. Hakuna taifa , ni hali ya machafuko tu."

"Hiki ni kipindi chetu cha kihistoria na cha changamoto ,"aliendelea . "Na umoja ndio njia tunayopaswa kuifuata kuelekea mbele ".

Wakati fulani, hotuba ya Biden ilionekana kumkosoa mtangulizi wake , ingawa hakumtaja kwa jina la Donald Trump.

Wakati Trump mara nyingi amekuwa akizungumzia kuhusu ukuu wa marekani na kutukuza waasisi wake, Bw Biden alisema kuwa historia ya taifa imekuwa katika "mapambano wakati wote" baina ya ubora wake na wakati mwingine hali mbaya halisi.

Wakati ambapo mshauri wa Trump Kellyanne Conway alizungumzia "ukweli mbadala " takriban miaka minne iliyopita, Biden alisema : "Kuna ukweli na kuna uongo-uongo ulielezwa kwa ajili ya mamlaka na kwa ajili ya faida ."

Biden alikamilisha hotuba yake kwa kutahadharisha kwamba Marekani haipaswi "kugeka juu ndani" - wote kama watu binafsi kurudi nyuma kama "vikundi vinavyoshindana "na kama taifa ambalo lililoko katika jukwaa la dunia.

"Tutakarabati miungano yetu na kujihusisha na dunia kwa mara nyingine tena ," alisema.

Kwa maneno, Biden aligeuza ukurasa kutoka kwa ule wa siku za Trump wa "Marekani kwanza ".

Siku 100 za kwanza za utawala wowote ule ni muhimu kwa rais mpya . Ni vipi vipaumbele vyake? atakavyovitimiza katika uongozi wake?

Hotuba ya Biden ilionesha taswira halisi kwamba Biden anaingia mamlakani huku vipaumbele vyake vikiwa tayari vipo.

Serikali yake itahusika na usambazaji wa chanjo za virusi vya corona kwa njia ya haraka na ya usawa . Baada ya hilo , atatakiwa kushughulikia masuala ya kijamii na kiuchumi yaliyovurugwa na janga la corona.

Virusi vimeongeza ukosefu wa usawa katika mapato na kuzisukuma familia nyingi kukaribia kufilisika kiuchumi.

Viliathiri sekta za usafiri na utalii na kuyaumiza kifedha majimbo na serikali kuu.

Mafanikio yake yatapimwa mapema , huku akisukuma bunge la congress lililogawanyika kuidhinisha msaada mwingine mkubwa kifedha wa kukabiliana na athari za janga .

Kama anataka kuuidhinisha haraka , atahitaji uungwaji mkono wa seneti, na tayari kuna ishara kuwa baadhi huenda wanajianda kupinga matumizi zaidi ya fedha.

Vilevile kuna kesi ya mashitaka ya Seneti dhidi ya Trump, ambayo bado italeta changamoto nyingine kwa umoja wa taifa.

Jina la Trump litakuwa katika habari kwa wiki kadhaa, huku watetezi wake wakimuunga mkono na wapinzani wake wakitoa wito awajibishwe kwa mateso.

Baada ya hilo, huenda njia ya siasa ya Biden ikageuka. Amesema anataka kuboresha huduma za afya nchini marekani, kutatua tatizo la madeni yanayoongezeka ya vyuo vikuu , kufanya uwekezaji mpya katika miundo mbinu na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Unaweza pia kusoma:

Ameahidi kusukuma mabadiliko ya sheria za uhamiaji ambazo zinajumuisha kutoa uraia wa wahamiaji wasio na vibali.

Yale anayoyapatia kipaumbele, na ni vipi juhudi zake zitazaa mafanikio, huenda yakawa mafanikio ya jumla ya utawala wake.

Sherehe za kuapishwa kwake zimeisha. Lakini , kama Biden alivyoeleza katika hotuba yake, wamarekani wanakabiliana na moja ya changamoto kubwa zaidi katika historia ya taifa lao.

"Tutahukumiwa kwa jinsi tunavyotatua mizozo hii ya enzi yetu ," alisema.

Biden alikampeni dhidi ya Trump kwa ajili ya fursa ya kukabiliana na mizozo hiyo, Sasa ni fursa yake.