Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kuapishwa kwa Joe Biden: Ni masuala gani Biden atakayapa kipaumbele?
Joe Biden amekua katika siasa kwa kipindi cha miaka 50, lakini hakutegemea kukabiliana na changamoto kubwa katika siku yake ya kwanza ya utawala.
Vipaumbele vyake ni vipi?
Suala la kwanza ambalo ataanza nalo kwa kipindi cha kwa siku 10, ni kufanyia marekebisho amri za mtangulizi wake na nyingine kuidhinisha kwa kuwa zilikuwa nyingi.
Kipaumbele cha kwanza katika orodha ni kufuta marufuku tata za kusafiri, zilizowekwa na mtangulizi wake Donald Trump dhidi ya nchi alizoziangalia kama tisho la usalama, na kujiunga tena na mkataba wa mazingira wa Paris.
Yafuatayo ni mambo tunayofahamu ambayo rais atahitaji kuyashughulikia mara tu anapoingia madarakani.
Kukabiliana na janga la virusi vya corona
Wamarekani kuvaa barakoa
Virusi vya corona vimewauwa watu zaidi ya 400,000 nchini Marekani-na janga hilo na athari zake nyingi itakuwa ni kipaumbele cha kwanza cha utawala mpya.
Bw Biden amesema "moja ya mapambano muhimu zaidi ambayo utawala wetu utakabiliana nayo" Joe Biden amehaidi kutekeleza mkakati wake wa kukabiliana na Covid mara moja atakapoingia madarakani.
Unaweza pia kusoma:
Moja ya amri zake itakuwa ni kuwataka watu kote nchini Marekani kuvaa barakoa katika sehemu za umma na wakati wa kusafiri baina ya majimbo.
Bado, hakuna hakikisho kuwa magavana ambao hadi sasa wamekataa uvaaji wa barakoa kama jambo la lazima watabadili msimamo wao ghafla -inaonekana hakuna sheria inayompatia rais mamlaka ya kufanya uvaaji wa barakoa kuwa sheria kote nchini.
Bw Biden anaonekana kukubaliana na hilo, na akasema kuwa binafsi atajaribu kuwashawishi magavana kukubaliana na hilo.
Endapo hawatakubali, amehaidi kutoa miito kwa mameya na maafisa wakuu kuwashawishi kutekeleza hilo. Pia hakuna maelezo bado kuhusu jinsi hilo litakavyotekelezwa.
Dozi milioni 100 za chanjo katika siku 100
Bw Biden anataka kuharakisha utoaji wa chanjo kwenda kwa kasi akiwa na lengo la watu milioni 100 kupata chanjo ya kwanza dhidi ya Covid ndani ya siku zake 100 madarakani.
Moja ya mpango wa haraka ni kutoa dozi zote za chanjo zilizo badala ya kuzishikilia katika hifadhi za chanjo.
Pia anatarajiwa kuchukua hatua kwa kuzingatia mamlaka ya rais katika juhudi za kutengeneza matumizi ya kipimo cha haraka na kuweka mfumo wa kitaifa wa kusambaza vifaa , madawa na vifaa vya kujkinga na maambukizi , au PPE.
Kujiunga tena na WHO
katika ajenda zake ni ahadi ya kufuta uamuzi wa kuiondoa Marekani katika Shirika la Afya duniani (WHO).
Bw Trump alitangaza mipango ya kuondokana na uanachama wa WHO, akiishutumu kwa kutoshughulikia vyema Covid baada ya virusi kujitokeza nchini China na kusema kuwa ilishindwa kufanya "mageuzi yaliyohitajika sana ".
Amri za rais - Mipango ya Bw Biden katika wiki mbili baada ya kuchukua madaraka. Haya ndio mambo machache yanayotarajiwa:
- Marekani kurejea katika makubaliano ya Paris ya mazingira - mkataba wa dunia juu ya kupunguzwa kwa hewa chafu
- Kubadilisha marufuku tata ya usafiri kuhusu mataifa ya kiislamu
- Uvaaji wa barakoa kuwa wa lazima katika maeno ya umma na wakati wa kusafiri baina ya majimbo
- Kuendelea kusitisha malipo ya mikopo ya wanafunzi wakati wa janga la corona
Mageuzi katika ubaguzi wa rangi na Haki katika uhalifu
Kukabiliana ubaguzi wa rangi ni mzozo wa nne -sambamba na Covid, uchumi na hali ya hewa - Bw biden anasema lazima lishugulikiwe haraka.
Baadhi ya sera hizo -kama kutatua tofauti za kijamii katika makazi na huduma za afya - ni mambo yanayoingiliana na mipango mingine.
Ameahidi kuunda bodi ya usimamizi ya kusaidia katika mageuzi ya idara za polisi katika kipindi cha siku zake za kwanza 100 za utawala wake, ingawa maelezo ya mpango huo yaliyopo ni machache.
Kuwalinda wapenzi wa jinsia moja na waliobadili -LGBT
Pia ametoa ahadi kwa watu wa LGBT , kama vile kuelekeza raslimali katia kusaidia kuzuia ghasia dhidi ya watu wenye jinsia na waliobadili jinsia , na kukomesha marufuku ya kuwazuia kuhudumu katika jeshi , na kurejesha muongozo kwa ajili ya wanafunzi waliobadili jinsia/ wenye jinsia mbili katika shule.
Kutoa hakikishi kwa washirika wa Marekani
Rais ajaye wa marekani anasema kuwa anapanga kuwafikia haraka washirika wa Marekani ili kutatua mizozo na kuwaahidi kwamba " Marekani iko nyuma yenu ", akisema kuwa Marekani lazima "ithibitishie ulimwengu kuwa imejiandaa kuongoza tena- sio kwa mfano tu wa nguvu bali kwa nguvu za mfano wetu ".
Amesema akiwa katika ofisi ya rais al maarufu kama Oval Office- atazungumza na washirika wa Nato kwa ujumbe "tumerejea na unaweza kututegemea tena ".
Ingawa Bw Trump hakuwa rais wa kwanza kuwekea shinikizo mikataba mingine na wajumbe wa Muungano wa mkataba wa Nato kwa kuwataka wajumbe kutumia fedha zaidi za za ulinzi, alitishia wakati mwingine kujiondoa katika muungano huo ambao Bw Biden ameuita "mkataba wa ukuta wa demokrasia huru ".
Hatua za uchumi
Msaada kwa wapangaji na wamiliki wa nyumba
Timu ya Bw Biden imesema mipango ya kuongeza muda wa kuwafukuza na kuwafungia nyumba watu kutokana na mikopo - ambayo ilisitishwa mapema katika mwanzoni mwa janga-pamoja na kusimamishwa kwa malipo ya mikopo ya wanafunzi na riba.
Maafisa wa mpito wa Bw Biden alisema anapanga kuagiza mashirika ya serikali wiki hii " kuchukua hatua ya mara moja ya kutoa msaada wa kiuchumi kwa familia za wafanyakazi ", ingawa hawakutoa taarifa zaidi.
Dola trilioni 1.9 kwa ajili ya uchumi wa virusi vya corona
Wiki iliyopita, Bw Biden alitangaza dola trilioni 1.9 (£1.4tn) za mpango wa kuchochea uchumi kutokana na athari za Corona , akisema kuwa "mzozo mkubwa uliosabisha maumivu kwa binadamu na hakuna muda wa kupoteza ".
Iwapo itapitishwa na Congress, utahusisha malipo ya moja kwa mija ya dola 1,400 kwa Wamarekani wote.
Pia amejumuisha fedha za kusaidia usalama wa kufungula tena shule, ambazo anataka , jambo analotaka lifanyike katika kipindi cha siku 100.