Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kuapishwa kwa Joe Biden: Donald Trump asema imekuwa heshima kwake kuhudumia taifa la Marekani
Rais Donald Trump amelihutubia taifa la Marekani kabla hajaondoka madarakani na kusema: "Tumefanya kile ambacho tulikuja kukifanya na tumefanya mambo mengine mengi."
Katika video aliyoiweka kwenye mtandao wa YouTube, alisema "mapambano yalikuwa makali, vita ilikuwa ngumu... kwasababu hicho ndicho mlinichagua kukifanya".
Bwana Trump anaondoka madarakani akiwa bado hakubaliani na matokeo ya uchaguzi wa Novemba, ambao ulimuibua Joe Biden kuwa rais.
Bwana Biden ataapishwa leo Jumatano.
Wiki mbili za mwisho za utawala wa bwana Trump',umekumbwa na ghasia baada ya wafuasi wake kuvamia jengo la bunge la Capitol Hill, wakipinga matokeo ya uchaguzi.
"Ghasia za kisiasa ni shambulio la kila kitu tunachothamini kama Wamarekani. Kamwe hatuwezi kuvumilia," Bwana Trump alisema katika video yake, ambapo bado hakutambua ushindi wa mrithi wake.
Trump alisema nini zaidi?
Bwana Trump mwenyewe ameshtakiwa kwa uchochezi juu ya shambulio la uvamizi wa bunge na atakabilina na kesi hiyo baada ya kuondoka madarakani. Ikiwa atakutwa na hatia, anaweza kuzuiwa kufanya shughuli zozote za umma.
Trump ni rais wa kwanza kushtakiwa mara mbili. Kesi yake ya kwanza ilimuhusisha na kutumia wadhifa wake vibaya nchini Ukraine lakini alifanikiwa kushinda kesi hiyo baada ya kupata kura nyingi kutoka kwa chama chake cha Republican.
Ghasia hizo za kisiasa zimefunika changamoto inayoikabili Marekani ya ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona ambapo zaidi ya Wamarekani 400,000 walikufa kutokana na Covid 19 na watu milioni 24 wameathirika na janga hilo.
Katika ujumbe wake, bwana Trump alisema utawala wake umeweza kujenga uchumi wa Marekani kwa kiwango cha juu zaidi katika historia ya dunia.
Soko la hisa la Marekani limeongezeka, ingawa uchumi bado uko katika wakati mgumu kutokana na janga la corona.
Waajiri wengi walisitisha ajira za watu mwezi Desemba, Mauzo ya rejareja yalishuka katika miezi ya hivi karibuni huku madai ya wasiokuwa na ajira yakiwa yameongezeka.
Donald Trump, katika hotuba yake ya dakika 20, alisema utawala wake umefanya kile ambacho walikuja kukifanya na wamefanya zaidi.
Mtu anaweza kujadili mafanikio yake kama amepiga hatua kwa maili 400 (640km) kwa kujenga ukuta mpakani, kupunguza kodi, kurejesha sheria, kuwaapisha majaji, vita ya kibiashara na makubaliano ya kidiplomasia na mataifa ya mashariki ya kati ni kkiwango kikubwa cha mafanikio.
Lakini kwa namna moja au nyingine kujisifu kwake kuna ukweli.
Trump alipoingia madarakani mwaka 2016 aliweza kuweka mazingira mazuri ya kisiasa. Alifanya kampeni kama mtu wa nje na kupaza sauti kwa wale ambao walihisi mfumo hauwajali wao.
"Vita ilikuwa kubwa , mapambano yalikuwa makali , ni maamuzi magumu kwasababu hiyo ndio sababu iliyowafanya mnichague," alisema.
Ghasia na chuki aliyoipandikiza Trump wakati wa kuondoka kwake madarakani uimesababishwa na uvamizi wa jengo la bunge la Capitol wiki mbili zilizopita, imeharibu sifa zake na itamchukua muda mrefu kubadili mtazamo wa watu juu ya hilo.
Baada ya miaka minne za mila na desturi zilizozoeleka, watu wanamtathmini kuwa , Trump anaondoka madarakani akiwa ameiacha Marekani ikiwa imebadilika - kiuhalisia na kimtazamo na hata taifa hilo limebadilika moja kwa moja.
Kuwa aliweka ahadi na ameitunza.
Biden anajitayarisha vipi kuingia madarakani?
Bwana Biden na mke wake wanaondoka nyumbani kwao Delaware kwenda kuishi Ikulu Washington, ambapo rais huyu mteule alihudumu kwa miaka 36 kama seneta kabla hajawa makamu wa rais wa Barack Obama kuanzia mwaka 2008 mpaka 2016.
"Nikifa, Delaware itaandikwa katika moyo wangu," alisema kwa hisia wakati akihutubia kuwaaga,
Jumatano, ataenda Ikulu na katika jengo la bunge Capitol kwa ajili ya kuapishwa majira ya saa sita mchana.
Uapisho huu hautafanana na uapisho mwingine wowote: Washington ina ulinzi mkali tangu jengo la Capitol kuvamiwa ,maelfu ya askari wanafanya doria nje ya ukuta wa White House.
Idadi ndogo tu ya watu itaruhusiwa kuhudhuria kushuhudia shughuli hilo ya uapisho,tofauti na miaka ya nyuma ambapo mamia ya maelfu ya watu walikuwa wanahudhuria tukio hilo.
Miongoni mwa watu ambao hawatahudhuria shughuli hizo rais Trump atakuwa miongoni mwao. Ataondoka Florida Jumatano asubuhi - rais wa kwanza kutohudhuria shughuli hizo za uapisho wa mrithi wake alikuwa Andrew Johnson mwaka 1869.