Uchaguzi wa Marekani 2020: Seneta wa Republican kupinga kuidhinishwa kwa kwa Joe Biden

Mwanachama wa Republican anasema kwamba atakuwa seneta wa kwanza kupinga wakati bunge la Congress litakapomuidhinisha rais mteule Joe Biden wiki ijayo.
Seneta wa Missouri Josh Hawley alisema kwamba alikuwa na wasiwasi wa maadili licha ya kutokuwa na ushahidi wa kuwepo kwa udanganyifu katika uchaguzi uliopita.
Kundi moja la wanachama wa Republican katika bunge wawakiishi pia linapanga kupinga matokeo ya uchaguzi.
Lakini pingamizi hizo hazitarajiwa kubadilisha matokeo.
Baraza la wajumbe linaloidhinisha matokeo ya uchaguzi kwa kutoa pointi kwa kila jimbo lililoshindwa na wapinzani hao wawili mapema liliidhinisha ushindi wa rais mteule Joe Biden dhidi ya Trump kwa 306-232. Kura hiyo ni lazima zihakikiwe na bunge la Congress ifikiapo Januari 6 .
Siku ya kuapishwa kwa rais mteule na makamu wake itakuwa tarehe 20 Januari.
Tangu aliposhindwa katika uchaguzi, bwana Trump mara kadhaa amedai kwamba kulikuwa na udanganyifu wakati wa shughuli hiyo bila ya kutoa ushahidi.
Hatua za kisheria za rais huyo wa chama cha Republican kubadilisha matokeo zimekataliwa na mahakama.
Je Hawley alisema nini?
Bwana Hawley alisema hangeweza kupiga kura ili kuidhinisha matokeo hayo bila kusema wazi kwamba baadhi ya majimbo hususan Pennsylvania, lilishindwa kuheshimu sheria zake za uchaguzi.
Alisema kwamba bunge la Congress linapaswa kuchunguza madai ya udanganyifu wa kura na kuchukua hatua zitakazolinda maadili ya uchaguzi .
Lakini Bunge la Congress limeshindwa kuchukua hatua kufikia sasa.
Bwana Hawley ambaye ni seneta kwa mara ya kwanza anyeidaiwa kuwa na hamu ya kuwania urais hakutoa ushahidi wowote ambao huenda ungebadilisha matokeo rasmi.
Je ni nini kitakachofanyika wakati bunge la Congress litakapokutana?

Chanzo cha picha, Getty Images
Pingamizi ya hesabu ya kura zinazoungwa mkono na wanachama wa bunge hilo na mwanachama wa bunge la seneti ni sharti liangaziwe na wawakilishi katika mjadala wa saa mbili.
Lakini kwa kura ya jimbo moja kukataliwa , wabunge walio wengi ni sharti waunge mkono pingamizi hiyo kutoka kila bunge.
Hali hiyo kufikia sasa huenda isitokee kwa kuwa chama cha Democrats kina wabunge wengi katika bunge la uwakilishi na lile la seneti na kwamba tayari wabunge hao wamesema kwamba hawatapinga matokeo hayo.
Lakini seneta wa Congress Mo Brooks , mwananchama wa Republican kutoka jimbo la Alabama , ameahidi kupinga mpango huo ikimaanisha kwamba mjadala na kupigwa kwa kura tarehe 6 Januari ni hatua itakayofanyika.












