Virusi vya corona: Vatican inasema chanjo za corona 'zinakubalika kimaadili'

Iliyochapishwa

Utumizi wa chanjo zilizotengenezwa kutokana na seli za mimba zilizotolewa "unakubalika kimaadili", Kanisa Katoliki imetangaza Jumatatu.

Kusipokuwa na njia nyingine mbadala, chanjo kama hizo "zinaweza kutumiwa kwa dhamira njema",Vatican imesema.

Iliongezea kuwa hatua hiyo haimaanishi "inaaunga mkono rasmi" utoaji mimba uliofanyika.

Chanjo kadhaa zimetengezwa kwa kutumia vijusi vya mimba iliyotolewa miongo kadhaa iliyopita.

Hata hivyo hakuna hata chanjo moja zilizotengezwa zina na seli za vijusi.

"Chanjo zote zimeidhinishwa kuwa salama na zinaweza kutumiwa kwa nia njema na ufahamike kwamba matumizi ya chanjo kama hizi sio ushirikiano rasmi na utoaji mimba ambao seli zinazotumiwa katika utengenezaji wa chanjo zinatokana," Usharika wa Vatican wa Mafundisho ya Imani ulitangaza katika taarifa Jumatatu.

Taarifa hiyo iliyoidhinishwa na Papa Francis, pia ilisema "sharti la kimaadili" ni kuhakikisha nchi masikini zinapata chanjo inayofanya kazi vyema.

Suala la kukubali au kupinga chanjo ya corona limewagawanya viongozi wa kidini, wakati kangamano la Marekani la Makasisi wa Katoliki wiki iliyopita likionekana kuliunga mkono.

"Kutokana na dharura ya janga hili, ukosefu wa chanjo mbadala na ukweli kwamba inahusiswa na na utoaji mimba uliofanyika miongo kadhaa iliyopita bila shaka kupata chanjo iliyotengezwa wakati huu inaweza kukubalika kimaadili," taarifa iliyochapishwa na wanachama wa makundi hayo mawili walisema.

Ilisema chanjo za kampuni ya Pfizer/BioNTech na Moderna, ambazo zilitengezwa kutokana na mimba iliyotolewa kufanyia majaribio chanjo zilifanya vyema kuliko chanjo za Oxford/AstraZeneca, ambazo zilitumia seli kama hizo kutengeza, kuboresha katika awamu ya kufanyia majaribio.

Mahali ambapo hakuna njia nyingine, hata hivyo, "chanjo ya AstraZeneca itakubaliwa kutumika", taarika hiyo ilisema.

Nchi nyingi zilizo na idada ya juu ya watu walioambukizwa virusi vya corona ilna idadi kubwa ya Wakatoliki, ikiwa ni pamoja na Brazil, Mexico, Italia na Uhispania.

Taarifa ya uamuzi wa Vatican kuhusu suala hilo imekuja wakati ambapo shirika la habari la AFP limeripoti kuwa makadinali wawili wa karibu na Papa Francis wamepatikana na virusi vya corona.