Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tuzo za MTV za muziki wa Afrika 2020: Orodha kamili yawaliochaguliwa
Orodha ya wanamuziki wenye vipaji waliochaguliwa kwa ajili ya kupata tuzo za muziki wa Afrika la MTV Africa Music Awards (MAMAs), imetangazwa huku majina maarufu na mapya yakijitokeza tena kwenye orodha hiyo.
Tukio la kutoa tuzo hizo za mwaka 2021 litafanyika mjini Kampala Uganda tarehe 21 Februari 2020 kwa njia ya mtandao kutokana na janga la virusi vya corona.
Wanamuziki wa Afrika wenye vipaji waliochaguliwa ni pamoja na Burna Boy, Busiswa, Davido, Diamond Platnumz, Innoss'B, Kabza De Small, John Blaq, Master KG, Suspect 95, Sheebah, Soraia Ramos, Tiwa Savage, Yemi Alade and WizKid - ambao kila mmoja amechaguliwa kwa tuzo mbili.
Ni nani walioongoza?
Kikundi cha muziki cha São Tomé and Príncipe -Calema waliongoza kwa kuteuliwa tuzo tatu za Msanii wa mwaka, Kikundi bora zaidi cha mwaka , na Kikundi bora kilichoigiza mtindo wa muziki wa Kireno wa Lusophone.
Wasanii waliochaguliwa kwa tuzo za MAMA 52 kutoka nchi 15 walitangazwa katika kipindi cha muziki cha MTV Base Jumatano jioni katika kipindi maalum cha dakika 45 ambacho kilitangazwa katika MTV Base.
Ifuatayo ni orodha kamili ya wanamuziki walioteliwa kwa ajili ya Tuzo za MAMA 2021 Awards na makundi yao walivyoshinda:
Mwanamuziki bora wa kike:
Simi (Nigeria)
Sheebah (Uganda)
Sho Madjozi (South Africa)
Busiswa (South Africa)
Yemi Alade (Nigeria)
Soraia Ramos (Cape Verde)
Tiwa Savage (Nigeria)
Mwanamuziki bora wa kiume:
Burna Boy (Nigeria)
Innoss'B (Democratic Republic of Congo)
Kabza De Small (South Africa)
Harmonize (Tanzania)
Fireboy DML (Nigeria)
Master KG (South Africa)
Rema (Nigeria)
Kikundi bora cha muziki
Blaq Diamond (South Africa)
Sauti Sol (Kenya)
Kabza De Small / DJ Maphorisa (South Africa)
Calema (São Tomé and Príncipe)
Ethic (Kenya)
Rostam (Tanzania)
Msanii wa mwaka:
Burna Boy (Nigeria)
Calema (São Tomé and Príncipe)
Diamond Platnumz (Tanzania)
Master KG (South Africa)
Davido (Nigeria)
Tiwa Savage (Nigeria)
Wizkid (Nigeria)
Msanii aliyepata mafanikio :
Elaine (South Africa)
Tems (Nigeria)
Omah Lay (Nigeria)
Zuchu (Tanzania)
John Blaq (Uganda)
Sha Sha (Zimbabwe)
Focalistic (South Africa)
Mwanamuziki bora wa Hip Hop
Nasty C (South Africa)
Suspect 95 (Cote d'Ivoire)
Khaligraph Jones (Kenya)
Kwesi Arthur (Ghana)
NGA (Angola)
OMG (Senegal)
Wasanii bora wa muziki wa Uganda
Sheebah
Bebe Cool
John Blaq
Vinka
Daddy Andre
Spice Diana
Wasanii bora wa muziki wa Lusophone
Calema (São Tomé and Príncipe)
Preto Show (Angola)
Anna Joyce (Angola)
Mr Bow (Mozambique)
Nelson Freitas (Cape Verde)
Soraia Ramos (Cape Verde)
Wasanii bora wa muziki wa kifaransa
Innoss'B (Democratic Republic of Congo)
Suspect 95 (Cote d'Ivoire)
Dip Doundou Guiss (Senegal)
Stanley Enow (Cameroon)
Fally Ipupa (Democratic Republic of Congo)
Gaz Mawete (Democratic Republic of Congo)
Wasanii bora wa muziki wakati wa Lockdown
Diamond Platnumz (Tanzania) - Africa Day Benefit Concert
Black Motion (South Africa) - Red Bull Rendezvous
Niniola ft Busiswa (Nigeria / SA) - Africa Day Benefit Concert
Singuila (Congo) - DCDR Series
AKA (South Africa) - AKA TV
Yemi Alade (Nigeria) - Poverty (live session)
Unaweza pia kutazama: