Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mahakama ya juu zaidi China yamuajiri jaji mkuu mstaafu wa Uganda
Mahakama ya Juu zaidi nchini China imemteua mwanasheria mkuu wa zamani wa Uganda, Bart Katureebe, kama mwanachama wa jopokazi la wataalamu wa kuamua mzizo ya biashara ya kimataifa.
Jaji Katureebe atahudumu katika kamati hiyo kwa kipindi cha miaka mine ijayo.
Alistaafu kutoka mahakama ya juu zaidi ya Uganda mwezi Juni baada ya kutimiza miaka 70 kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo.
"Nimefurahia sana uteuzi hu, kwasababu ni kamati ya ngazi ya juu ambayo itaimarisha taaluma yangu," alinukuliwa na akisema katika taarifa iliyowekwa katika mtandao wa twitter wa idara ya mahakama ya Uganda.
Chama cha mawakili nchini Uganda pia kimempongeza Jaji Katureebe.
Kamati hiyo ya wataalamu, ilibuniwa mwezi Agost mwaka 2018, ni sehemu ya mahakama ya kimataifa ya biashara ya China (CICC) ambayo ni kitengo cha mahakama ya juu zaidi ya China.
Kamati hiyo inajumuisha viongozi 31 wa mashirika ya kimataifa, wataalamu wa sheria, wanazuoni, majaji na mawakili walioteuliwa kutoka nchi tofauti, taarifa kutoka idara ya mahakama ya Uganda iliongeza.
Inatatua mizozo ya kimataifa ya bishara inayopewa, kutoa maoni ya kisheria kuhusu sheia ya kimatafa wakati inapoumbwa kufanya hivyo na kutoa ushauri kuhusu hatma ya baadaye ya CICC.
Ubalozi wa China nchini Uganda umempongeza Jaji Katureebe kufuatia uteuzi wake.