Waziri Mkuu wa Lebanon ashindwa kuunda serikali mpya baada ya mlipuko

Iliyochapishwa

Waziri Mkuu ambaye ameteuliwa Lebanon Mustapha Adib ameachana na juhudi za kuunda serikali mpya kutokana matakwa ya mabadiliko kutoka kwa walio wengi.

Bwana Amid hakutoa maelezo kuhusu uamuzi wake.

Hata hivyo, ripoti mbalimbali zinasema ni kutokana na ugumu wa upande wa Shia unaohitaji kushikilia wizara ya fedha na wizara ya juu ndani ya baraza la mawaziri.

Lebanon iko katika hali ngumu ya kiuchumi. Hali hii ni kutokana na mlipuko mkubwa uliotokea Agosti 04, jijini Beirut ambapo watu 190 waliuawa na 6000 kujeruhiwa.

Serikali ya Lebanoni iliyopita ilijiuzuru kutokana na shinikizo la machafuko baada ya mlipuko, ulioathiri sehemu kubwa ya mji mkuu.

Sababu ya mkasa ilikuwa ni upangwaji wa tani 2750 za kemkali ya Ammonium Nitratez iliyokuwa imehifadhiwa bila kujali usalama ndani ya ghala kwa miaka sita katika bandari ya jijini Beirut .

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, mlipuko huo unakadiriwa kusababisha hasara ya dola bilioni 4.6 (sawa na Pauni bilioni 3.4) kutokana na uharibifu wa majengo na miundombinu uliotokea.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amevitaka Vikundi vya Kisiasa vya Lebanon kuunda serikali mpya haraka.

Bwana Macron mejitolea kusaidia kuandaa mkutano katikati ya mwezi Oktoba.

Kwa nini Adib ameacha mpango wa kuunda serikali?

Mustapha Adib, ambaye ni balozi wa zamani wa Lebanon nchini Ujerumani, aliteuliwa kushika nafasi hiyo Agosti 31.

Alisikika akisema anataka kuanza mabadiliko haraka na kulitaka Shirika la Fedha Duniani kusaidia hilo.

Lakini wanasiasa wa kiislamu wa sunni wanaonekana kupata kikwazo bungeni kutoka kwa upande wa waislamu wa shia.

Hezbollah and Amal walitaka kuendelea kushikilia wizara ya Fedha.

Kwa kuongezea, Bwana Adib ameripotiwa akisisitiza kuhusu kuunda baraza la watumishi wa umma, wakati vikundi vya kisiasa vikihitaji uteuzi sahihi wa mawaziri.

Baada ya kukutana na Rais Michael Aoun Jumamosi, Bwana Adib alisema "alikuwa akijitetea mwenyewe kwa kutokuunda serikali".

Aliwaomba radhi Walebanon kwa "kushindwa kuelewa matakwa ya wanamabadiliko" kuitumikia nchi, lakini aliongeza kusema hakuhitaji kuongoza baraza la mawaziri "alifungua na kushindwa"

Vipi hali ya Lebanon?

Waandamanaji wanaopinga Serikali wamefanya jukwaa la mikutano ya hadhara takriban mwaka mmoja, wakihitaji kung'olewa kwa mfumo mzima wa siasa.

Nguvu hii imejikita zaidi kwenye matakwa ya kimadhehebu ndani ya nchi, serikali iliyoshika hatamu inalaumiwa kwa kutokuwa nnnnnnnnnna ufanisi na uongozi wa kisomi.

Uteuzi wa kisiasa na nafasi nying hutokana na kuwemo kati ya madhehebu ya kidini ya jamii za taifa hilo, hali iliyosababisha kuwepo kwa ukabila na rushwa iliyokithiri.

Hata kabla ya mlipuko, nchi ilikuwa kwenye matatizo makubwa ya kifedha na kuporomoka kwa sarafu, ukosefu wa ajira na kuongezeka kwa umasikini.