Jacob Blake aliyepooza afunguliwa pingu alizokuwa amefungwa hospitalini

Chanzo cha picha, Getty Images
Jacob Blake, mwanaume mweusi aliyepigwa risasi kwa nyumba na polisi nchini Marekani huko Wisconsin, inasemekana kwamba amefunguliwa pingu alizokuwa amefungwa akiwa hospitali.
Polisi huko Kenosha ilisema kuwa Bwana Blake alikuwa kizuizini kutokana na vibali vya kukamatwa kwake vya awali na kufungwa pingu ilikuwa ni sera ambayo imekuwepo.
Mwendesha mashtaka ameambia vyombo vya habari vya Marekani kwamba vibali vya kukamatwa kwake vilikuwa vimefutwa na kwamba maafisa waliokuwa wanamlinda Bwana Blake walikuwa wameondoka.
Bwana Blake alipooza baada ya kupigwa risasi mara saba na afisa wa polisi na bado haijafahamika ikiwa atatembea temba kwa miguu yake.
Wakati huohuo, kusikilizwa kwa kesi ya kijana mmoja aliyeshitakiwa kwa mauaji ya watu wawili wakati wa maandamano ya kupinga tukio la kupigwa risasi kwa Bwana Blake kumeahirishwa kwa mwezi mmoja.
Kyle Rittenhouse, 17, alitakiwa kufika mbele ya mahakama huko kaunti ya Lake, Illinois, kusikiliza ombi la kuwasilishwa kwake Wisconsin.
Lakini hakimu aliahirisha kesi ya kusikiliza ombi hilo hadi Septemba 25.
Bwana Rittenhouse hakuwa mahakamani wakati wa kesi hiyo iliyofanyika Ijumaa kupitia njia ya mtandao.
Anakabiliwa na mashitaka sita ikiwemo mauaji ya kukusudia daraja la kwanza na umiliki wa silaha hatari chini ya umri wa miaka 18.
Rittenhouse anatetewa na kampuni moja maafuru ya sheria ambayo wateja wake ni pamoja na mwanasheria wa kibinafsi wa Rais Donald Trump, Rudolph Giuliani na aliyekuwa mshauri wa Trump Carter Page.
Familia imesema nini?
Baba yake Blake ambaye pia anajulikana kama Jacob Blake, alizungumza na wanahabari baada ya kumtembelea kijana wake hospitali.
"Nilichukia kumuona akiwa kitandani na amefungwa pingu," alisema, akinukuliwa na gazeti la Chicago Sun-Times. "Hawezi kwenda popote. Kwanini munamfunga pingu akiwa kitandani?"
Polisi na serikali wamesema nini?
Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Gavana Evers amesema ''ombi la kupata maafisa wa ulinzi ilikua ni kusaidia kusimamia sheria ''kulinda miundombinu'' na kuhakikisha kuwa watu wanaandamana kwa usalama.
Alisema kuwa anasambaza maafisa karibu 125 wa kulinda usalama Jumatatu usiku.
Mapema asubuhi baaadhi ya waandamanaji walijaribu kuingia kwenye jengo la usalama la mji wa Kenosha, wakitaka maafisa waliohusika katika tukio la kufyatua risasi wakamatwe.
Mlango ulivunjwa kabla ya maafisa kutumia dawa ya kupuliza yenye pilipili kusambaratisha kundi la watu.
Mamia ya watu pia waliandamana mpaka makao makuu ya polisi usiku wa Jumapili wakikemea tukio hilo.
Gavana Evers amekemea tukio hilo, akisema kuwa Bwana Blake hakuwa ''mtu wa kwanza kufyatuliwa risasi au kujeruhiwa au kuuawa mikononi mwa polisi.''
Lakini gavana wa Democratic amekosolewa kwa jibu lake.
Lakini gavana huyo amekosolewa kutokana na kauli yake, mkuu wa polisi mjini Kenosha Pete Deates, amesema kuwa kauli ya Evers ''haikuwa ya kuwajibika'' na kusema kuwa watu wanapaswa kusubiri mpaka pale ukweli utakapojulikana.

Chanzo cha picha, EPA
Bwana Evers pia amesema kuwa kutakuwa na kipindi maalumu kwa wabunge ifikapo tarehe 31 Agosti kujadili sheria zilizotangazwa mwanzoni mwa mwaka huu kuhusu uwazi na uwajibikaji wa watu baada ya kuuawa kwa George Floyd.
Tunachokifahamu kuhusu shambulio hilo?
Idara ya polisi imesema kuwa afisa wa polisi ''aliyehusika kwenye tukio la kufaytua risasi'' lililotokea siku ya Jumapili.
Na kuongeza kuwa maafisa ''walitoa msaada wa haraka'' kwa bwana Blake, ambaye alifikishwa hospitali mjini Milwaukee akiwa katika hali mbaya.
Katika picha ya video, maafisa watatu walionekana wakimuonesha silaha mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina Blake wakati akielekea kwenye gari aina ya SUV iliyokuwa imeegeshwa.
Alipofungua mlango na kutaka kuingia ndani, alioneka ofisa mmoja akimkamata shati na kumfyatulia risasi. Milio saba ya risasi ilisikika kwenye video hiyo huku mashuhuda wakipiga kelele.
Polisi wamesema maafisa hawajaeleza kilichosababisha hata wakafyatua risasi. Haijulikani ni nani aliwaita polisi na kilichotokea kabla ya video kuanza kurekodiwa.
Pia unaweza kutazama:













