Joselyne Umutoniwase: Mnyarwanda aliyefanikiwa kibiashara baada ya kuuza masanduku mawili ya nguo

Iliyochapishwa

Katika mfululizo wa taarifa kuwahusu viongozi, tunawaangazia viongozi wa biashara kutoka maeneo tofauti ya dunia. Wiki hii tunazungumza na mbunifu wa mitindo Mnyarwanda Joselyne Umutoniwase.

Mnamo mwaka 2010, Joselyne Umutoniwase alichukua uamuzi mgumu. Alikua akifanya kazi kama mhariri wa filamu kwa miaka mitano lakini aliamua kufuata ndoto yake ya kuwa mbunifu wa mitindo ya mavazi.

Alitengeneza nguo za mitindo yake kwa mara ya kwanza wakati aliposafiri kwenda Ujerumani kwa mafunzo ya filamu, ambapo alichukua mabegi mawili yaliyokua yamejaa nguo blauzi , sketi na magauni.

"Wajerumani vijana walifurahishwa sana na mtindo na rangi nzuri za kuvutia za vitenge vilivyochorwa michoro ya kiafrika vya wax ," anasema.

Aliuza nguo zote alizopeleka katika kipindi cha miezi mitatu.

"Sikujua kwamba ningeweza kupata pesa nzuri kwa kuuza nguo nilizobuni mwenyewe ,"anasema kutoka katika eneo la biashara yake mjini Kigali.

Uzoefu wa Ujerumani ulimpa moyo wa kujiamini wa kutosha na usaidizi kidogo wa kubadili kazi yake.

Aliacha kufanya kazi kama mhariri wa filamu, akanunua mashine tatu za kushona nguo, akawakodisha mafundi cherehani na kuanzisha nembo yake binafsi ya mitindo Rwanda Clothing.

Sasa, miaka minane baadae, anaendesha kituo cha ushonaji kikiwa na mafundi wa nguo 37 walioajiriwa, akiuza nguo kuanzia dola 50 hadi dola 120 (£40-£95).

Joselyen alivutiwa na nguo, kwani alikulia katika familia ya kipato cha kati katika mji mkuu Kigali.

Alinunua nguo za bei rahisi za mitumba ambazo hakuna mtu aliyezitaka, anasem. ''Nilitenganisha sehemu zote kuangalia ni vipi nguo hizi zilitengenezwa.''

Lakini kutokana na kwamba nguo nyingi zinakuja Rwanda kutoka China na India, sikuona kama ni kitu kinachoweza kunipatia ajira, na badala yake nikasomea filamu, kuwafurahisha wazazi , Teknolojia ya mawasiliano(IT)

Baba yake na wajomba zake wanamiliki biashara kadhaa. Hii ilimhamasisha kuanza saluni ndogo ya kusuka nywele wakati alipokua akisoma sekondari.

Lakini uzoefu wao pia ulimuonyesha ni jinsi gani pia mambo yanavyoweza kwenda kombo. ''Nilisikitika sana nilipokua mtoto, wakati baba yaangu alipolazimika kufunga biashara yake ya kichinjio (bucha) kwasababu mshirika wake katika biashara hiyo alitoroka na pesa zote."

Kupata pesa pia ilikua ni changamoto , kwani benki hazikutaka kuipatia mkopo kwa kampuni yake ya Nguo za Rwanda Rwanda Clothing.

"Fasheni ilikua ni sekta mbayo hakuna mtu yeyote aliyeichukulia kama kitu cha maana wakati huo," anasema, na kwa maoni ya benki , "mimi kama mwanamke mwenye umri wa miaka 24 kuwa muanzilishi wa kampuni halikua ni suala ambalo walilipa uzito."

Hatahivyo, alikutana na wakili na muwekezaji Roman Schulz wakati alipokwenda nchini Ujerumani mwaka 2010. Alifurahia sana kazi yake ya ubunifu na kipaji cha asili kama mbunifu wa mavazi, akamuamini na baadae akawa mshirika wake wa kibiashara na mume wake.

Waliweka pamoja pesa zao kiasi cha dola $10,000 walizokua wamejiwekea na kuwaajiri wafanyakazi wake.

Anakiri kwamba alifanya makosa machache. Kwa mfano katika maonesho yake mawili za kwanza za fasheni.

" na kuwaalika watu muhimu-VIP. lilikua ni jambo zuri lakini sikuhitaji wanamitindo 25, kutoa vinywaji vya bure. Ningefanya onyesho hili kwa ujanja na kwa garama cha chini zaidi ," anasema.

"Joselyne kila mara huwa na ari ya ujasiliamali na malengo ya juu nay a zaidi ya kile alichofikia ," anasema Alice Nkulikiyinka, Mkurugenzi wa mtandao wa wafanyabiashara wenye taaluma nchini Rwanda.

"Kampuni yake imekua mfulurizo, ikitoa ajira kwa watu zaidi ya 40 . Joselyne alianzisha nembo inayotambuliwa kimataifa ."

Mwaka 2018, moya ya njozi kubwa za Joselyne ilitimia wakati alipoalikwa katika maonyesho ya wiki ya Milan -Milan Fashion Week.

"Ilikua ni ushindi kuwepo pale," anasema. "Nilihisi vizuri sana kutambuliwa kwa kiasi kile kwa kazi yangu kuwasilisha mitindo yangu ya mavazi yangu katika maonesho."

Anasema angependa kuanza kuuza kimataifa kupitia duka la mtandao, lakini uwezo bado ni changamoto,

"Sitaweza kuhimili kushuhudia wateja wakinirudishia nguo ," anasema, jambo ambalo ni gumu kuliepuka katika fasheni.

Sasa anapanga kuanza duka la mtandaoni Ulaya la vitu vya ndani na mapambo kama vile skafu, mito na mikoba. Lakini yuko makini kutowasahau wateja wake wa mwanzoni.

"Unapakua haraka sana na kuwakatisha tama wateja ulionao, unaweza kuharibu biashara yako."

Lakini mipango yake imeahirishwa kutokana na mozo wa virusi vya corona.

"Tulilazimika kufunga biashra wakati wa sheria ya kukaa nyumbani ya siku 45. Na ingawa serikali imelegeza masharti ya kukaa nyumbani hivi karibuni, wateja bado wanaogopa kuja ."

Mafundi wake wanafanya kazi kwa zamu ili kuheshimu maagizo ya kutokaribiana, anasema.

"Nchini Rwanda, tumezoea changamoto. Zimetulazimisha kuwa wabunifu zaidi, kujifunza kupata suluhu na kupata na mawazo mapya."

Joselyne na familia yake walilazimika kukimbilia nchi jirani wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 na akawapoteza bibi zake (nyanya zake) na wajomba kadhaa, mashangazi na mabinamu.

"Nina kumbukumbu za mbali sana kwani nilikua na umri wa miaka sita tu na huenda tukio la mauaji ya kimbari lilichangia kusahau baadhi ya mambo kwani lilikua ni la kutia kiwewe ," anasema.

" Katika miaka iliyofuatia, nakumbuka nilivyokua ninafikiria muda mwingi juu ya tukio la mauaji ya kimbari, nikijiuliza'ni kwanini jambo kama hili lilitokea kwa nchi yangu ?"

Awali alitaka kuondoka Rwanda kabisa.

"Ilikua inaumiza sana kujua kwamba kitu kama hicho kilitokea kwa nchi yangu. Na nilikua naogopa kinaweza kutokea tena. Unahisi

Kutokuwa salama muda fulani na haumuamini mtu yeyote.

''Lakini wakati unafika, unaamua kuwa na amani. Kwa vyovyote vile , huwezi kusema ukweli kubadilisha hali hii.''

"Pia niliona barabara mpya zikijengwa, nyumba mpya zikajengwa. Nikaona nchi inakarabatiwa. Na mambo chanya, baada ya maafa yale, watu kusema kweli wanataka kuishi ."