Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mahakama ya Canada yaamua Marekani 'sio salama' kwa wahamiaji
Mahakama nchini Canada imeamua kwamba mkataba wa kuwapa hifadhi wakimbizi iliyofikiwa kati ya nchi hiyo na Marekani umekikwa kutokana na jinsi Marekani inavyowashughulika wakimbizi.
Makubaliano ya nchi ya tatu salama, iliyofikiwa tangu mwaka 2004, inawataka wakimbizi kuomba hifadhi salama katika nchi ya kwanza wanayofika.
Lakini siku ya Jumatano, jaji mmoja amesema kuwa mkataba huo unakiuka katiba kwa kuhofia Marekani huenda ikawafunga wahamiaji.
Uamuzi huo unashiria ushindi mkubwa kwa wanaharakati wa masuala ya uhamiaji nchini Canada.
Mawakili wa wakimbizi wiliokuwa wamefukuzwa katika mpaka Canada walikuwa waliwasilisha kesi mahakamani kupinga makubaliano hayo ,wakihoji ''usalama'' wa Marekani kwa watu wanaomba hifadhi .
Wahamiaji kuzuiliwa kuingia Marekani kutokana na corona
Nedira Jemal Mustefa, mmoja wa wakimbizi waliolazimishwa kusalia nchini Marekani, aliifahamisha mahakama jinsi alivyopitia kipindi kigumu alipokua amefungiwa Marekani "niliingiwa na uoga baada ya kutengwa,"kwa mujibu wa uamuzi wa mahakama.
"Sote tunajua jinsi Marekani inavyowanyanyasa watu wnaotafuta hifadhi nchinoi humo," Maureen Silcoff, rais wa chama cha mawakili wa wakimbizi nchi Canada, aliiambia shirika la habari la Reuters.
Mpaka wa umbali wa kilomita (8,891) kati ya Marekani na Canada ndio mrefu zaidi kati ya nchi mbili duniani.
Je, Mkataba wa Nchi Salama ya Tatu ni Nini?
Makubaliano ya nchi salama ya tatu ni sera iliyofikiwa kuwashughulikia masuala ya wahamiaji ili kuzuia mvutano wa kidipolomasia kati ya nchi zinazowapokea wakimbizi.
Sera hiyo pia inawashawishi wahamijaji kuvuka kiharamu na kuingi nchini Canada ili kuepuka kurudishwa katika vituo vya mpakani.
Tangu mwaka 2017, wakati Rais Donald Trump alipoingia madarakani kwa ahadi ya kushughulikia suala la uhamiaji haramu, karibu watu some 58,000 wamevuka mpaka na kurejea Canada kwa kuhofia kukamatwa.
Canada imekua ikiwapokea wahamiaji hao hadi pale janga la corona lilipozuka, wakati serikali ya Canada ilipotangaza kwamba watarejeshwa walikotoka.
Kumekua na wito wa kuitaka Canada kufutilia mbali sera ya uhamiaji na Marekani.