Virusi vya corona: Walioambukizwa Tanzania wafikia 254

Watanzania wanahimizwa kunawa mikono kudhibiti maambukizi ya coronavirus
Maelezo ya picha, Watanzania wanahimizwa kunawa mikono kudhibiti maambukizi ya coronavirus
Iliyochapishwa

Wizara ya afya nchini Tanzania imethibitisha kuwa watu 84 wapya wameambukizwa virusi vya corona na kufikisha idadi ya wagonjwa wa Covid-19 kufikia 254.

Wagonjwa hao wanatoka katika pande zote mbili za Tanzania, Zanzibar.

Kwa upande wa Bara maambukizi ya virusi hivyo sasa yameripotiwa katika mikoa 17, na wagonjwa wapya waliotangazwa Jumanne na Waziri Ummy mwalimu wanatoka mikoa ya Dar es Salaam(33), Arusha (4),Mbeya(3), Dodoma (3), Kilimanjaro(3), Pwani,(3) Tanga(3), Manyara(2), Tabora(1), Ruvuma(2), Morogoro(2) Rukwa(2), Kagera(1), Mara(1) na Lindi (1).

Habari zaidi zilizotolewa Jumatatu jioni na wizara hiyo zinaarifu kuwa watu watatu wapya wamefariki kutokana na sababu zinazohusiana na maradhi ya Covid-19.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo wagonjwa wote walioripotiwa Tanzania bara wanaendelea kupata nafuu isipokuwa wanne ambao wanahitaji uangalizi maalum.

Kufikia sasa katika eneo la Tanzania bara wagonjwa wameambukizwa kama ifuatavyo kwenye mabano

Wagonjwa 23 kati hao 84 waliothibitishwa ni wale waliotolwa na Wizara ya Afya ya Zanzibar Jumatatu.

Hatuazilizochukuliwa kudhibiti maambukizi ni zipi?

  • Shule zote na vyuo vya elimu vimefungwa mpaka itakapotangazwa ili kuzuia kuenea kwa maambukizi ya corona nchini humo.
  • Pamoja na kuzuia mikusanyiko yote ya watu wengi yakiwemo matamasha ya muziki, mikutano ya hadhara mbalimbali ikiwemo ya kisiasa.
  • Magari ya usafiri wa umma hatayakiwi kujaza abiria, na wote lazima wawe wameketi vitini.
  • Ndege za abiria zimezuiwa kutua nchini humo.
  • Kuanzia Jumatatu ya Aprili 20 ni lazima kwa wakaazi wote wa Dar es Salaam kuvaa barakoa wanapokuwa maeneo ya umma.
  • Biashara zote za chakula jijini Dar es Salaam zinatakiwa kufunga bidhaa zao na kutoruhusu watu kula kwenye migahawa.
Coronavirus
Banner

Awali Bunge la Tanzania lilithibitisha kwamba mmoja wa wabunge wake ameambukizwa virusi vya corona.

Taarifa hiyo imetolewa na naibu spika wa bunge Tulia Ackson japo hakutaja jina la mbunge huyo.

Aliongeza kuwa mbunge huyo anaendelea vizuri na kuongeza kuwa serikali inamuangalia na kumpatia matibabu stahiki.

Kulingana na maelezo ya mbunge huyo alisafiri na kwenda mjini Dar es Salaam hivi karibuni.

Kwa sasa vikao vya bunge hilo vimeahirishwa ili linyunyuziwe dawa ya kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya corona.

Tanzania imekuwa ikikosolewa kwa kutochukua hatua kali ikiwemo kuendelea kuruhusu maeneo ya ibada kuwa wazi.

Baadhi ya wanaharakati pamoja na viongozi wa upinzanii pia wanaitaka serikali kuweka marufuku ya watu kutoka na kuingia jijini Dar es Salaam ambayo inaonekana kuwa kitovu cha maambukizi ya virusi hivyo nchini humo.