Virusi vya corona: Mbunge wa Tanzania aambukizwa

Naibu spika wa bunge la Tanzania

Chanzo cha picha, Tanzania Parliament

Iliyochapishwa

Bunge la Tanzania limethibitisha kwamba mmoja wa wabunge wake ameambukizwa virusi vya corona.

Taarifa hiyo imetolewa na naibu spika wa bunge Ackson Tulia japo hakutaja jina la mbunge huyo.

''Tumepata taarifa kwamba mmoja wetu amepata maambukizi'' alisema.

Aliongeza kuwa mbunge huyo anaendelea vizuri na kuongeza kuwa serikali inamuangalia na kumpatia matibabu stahiki.

Kulingana na maelezo ya mbunge huyo alisafiri na kwenda mjini Dar es Salaam hivi karibuni.

Kwa sasa vikao vya bunge hilo vimeahirishwa ili linyunyuziwe dawa ya kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya corona.

''Wabunge wote mtatakiwa kuondoka kabisa maeneo ya bunge ilikutoa nafasi kwa ofisi na wataalamu wa afya kuendelea na zoezi la kunyunyiza dawa ili kutakasa eneo la bunge'' aliendelea kusema Dkt Tulia.

Mudada mfupi uliopita Wizara ya afya nchini Tanzania imethibitisha kuwa watu 84 wapya wameambukizwa virusi vya corona na kufikisha idadi ya wagonjwa wa Covid-19 kufikia 254.

Wagonjwa 23 kati hao 84 waliothibitishwa ni wale waliotolwa na Wizara ya Afya ya Zanzibar Jumatatu.

Coronavirus
Banner

Huku hayo yakijiri mchungaji mashuhuri wa kike na mbunge wa viti maalum Gertrude Rwakatale amefariki dunia mapema Jumatatu akiwa na umri wa miaka 69.

Mwanawe wa kiume ameambia vyombo vya habari kuwa Bi Rwakatare alifariki kutokana na tatizo la shinikizo la damu alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali moja jijini Dar es Salaam.