Virusi vya corona: Wakenya walaani ubaguzi wa rangi wanaodaiwa kufanyiwa wenzao Uchina

    • Author, Dinah Gahamanyi
    • Nafasi, BBC News Swahili
  • Iliyochapishwa
  • Muda wa kusoma: Dakika 3

Baada ya Waafrika wanaoishi nchini Uchina kulalamika kuwa wanabaguliwa na kufurushwa kwenye nyumba na hoteli, serikali ya Uchina imesema kuwa inawachukulia wageni wote kwa usawa.

Kauli ya msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Uchina Zhao Lijian inakuja wakati video na picha zilizotumwa kwenye mitandao ya kijamii za watu wanaodaiwa kuwa ni Waafrika waliokwama kwenye mitaa ya Uchina baada kufurushwa kwenye nyumba na hoteli na kubaki bila makazi.

Amesema Nchini Uchina kazi yetu ya dhahurura ni kuchukua hatua za kudhibiti mlipuko, amesema Lijian.

Tunafuatilia kwa hali ya juu matukio na kutolelewa kuliko jitokeza katka mchakato huu. Tunaomba mamlaka husika kuboresha kazi zake, tunatumai wote Wachina na Wageni nchini Uchina wanazingatia sheria za kukabiliana na janga, shirikiana na tuunge mkono katika mapambano dhidi ya virusi imesema taarifa ya ya twitter kupitia Ubalozi wa China nchini Kenya

Baadhi ya Wakenya walioko nchini Uchina kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari nchini Kenya wamekua wakizungumzia masaibu wanayoyapitia baada ya kufurushwa na kubaguliwa huku wakinyimwa huduma kwa kile wanachodai wanaangaliwa kama wageni wanaosambaza virusi vya corona.

Wamekua wakiiomba serikali yao kurudi nyumbani kutokana na ubaguzi wa rangi dhidi ya Waafrika wanaoishi Uchina baada ya janga la virusi vya corona.

Taarifa za mateso wanayodaiwa kupitia Wakenya nchini Uchina zimeibua hisia kali hususan katika mitandao ya kijamii ambapo baadhi ya Wakenya wameomba uhusiano baina ya mataifa hayo mawili uchunguzwe upya.

Kupitia kampeni #ChinaMustExplain au #ChinaLazimaEeleze kwenye mitandao ya kijamii Wakenya wamekua wakielezea hisia zao kuhusu hali ya wenzao nchini Uchina, huku wengi wakiitaka serikali ya Kenya kuchukua hatua kunusuru raia hao.

Mbunge wa zamani wa Kiambuu William Kabogo kwenye ukurasa wake wa Twitter amemsihi rais Kenyatta Kutuma ndege kuwachukua Wakenya wanaoishi Uchina:

@SokoAnalyst amesema wanamsubiri rais ajibu kuhusu ubaguzi wa rangi dhidi ya Wakenya nchini Uchina na hawatakubali watu wanyanyaswe wakiwa kimya na watu wao wakiishi maisha ya raha nchini Kenya:

Gazeti la The Daily Nation nchini Kenya limeripoti kuwa Wakenya wengi wanaoishi nchini Uchina kwa sasa wanaishi kwenye mitaani wakitegemea chakula kutoka kwa wasamalia wema na mahitaji mengine ya kimsingi.

Polisi wa Uchina wanadaiwa kufurusha kwenye nyumba Wakenya na Waafrika wengine na kuwanyang'anya nyaraka zao za kisheria.

Wakenya, hususan wale wanaoishi maeneo ya Guangdong, wanadaiwa kuathiriwa na wimbi hili na wanaripotiwa kuishi kwa hofu kutokana na ukatili wanaokabiliana nao huku hawajafanya uhalifu wowote.

Katika taarifa yake ya hivi punde ,wizara ya mambo ya nje nchini Kenya imethithitisha kutambua kuhusu visa vya kutowatendea haki raia wa Kigeni, na imesema kuwa kupitia ubalozi wake nchini Uchina imepokea hakikisho kuwa serikali ya Uchina inalichukulia suala hilo kwa umakini na maafisa wa Guangzou wamepewa jukumu la kuchukua hatua za mara moja kulinda haki za Waafrika.

Taarifa zaidi kuhusu virusi vya corona:

Unaweza pia kutazama: