Coronavirus: Virusi ni nini na kwanini vinahatarisha maisha ya wahudumu wa afya?

Health care professionals take a break awaiting patients as they test for COVID-19 at the ProHEALTH testing site in Jericho, New York, March 24, 2020.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Healthcare workers are disproportionately at risk of Covid-19 infection
Iliyochapishwa

Katika makabiliano dhidi ya Covid-19, wahudumu wa afya kote duniani ndio wanaotaabika zaidi.

Maelfu yao wameambukizwa virusi vya corona huku idadi ya wanaokufa ikiendelea kuongezeka.

Licha ya vifaa vya kujilinda kama vile sare maalum na barakoa, madaktari, wauguzi na wahudumu wengine wa afya inaonekana ndio walioko katika hatari zaidi ya kuambukizwa virusi hivi na pengine pia wako katika hatari ya kuwa wagonjwa zaidi.

Lakini kwanini wanaugua?

Virusi

Watalaamau wanasema virusi ambavyo wanakabiliana navyo wakati wa kutibu wagonjwa ni sehemu kubwa inayochangia vifo vyao.

Baada ya kirusi kuingia mwilini, kinavamia seli na kuanza kujizalisha. Virusi hivi vinaanza kujijenga siku zinazofuata na hivyo basi mgonjwa huyo atakuwa na kiwango kikubwa cha virusi.

Kiwango kikubwa cha virusi kuna maanisha kwamba utaumwa sana na pia mgonjwa anakuwa katika hatari ya kupata maambukizi.

Medical workers perform the Cesarean section operation on a suspected COVID-19 patient in Wuhan Union Hospital in Wuhan in central China's Hubei province Saturday, March 07, 2020.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wahudumu wa afya wao ndio wanaoshuhulikia wagonjwa na hivyo kuwa katika hatari zaidi ya kupata maambukizi

“Virusi vikiwa vingi ndani yangu kuna uwezekano mkubwa kwamba virusi hivi nitavirithisha kwako,”Professor Wendy Barclay, kutoka idara ya Magonjwa ya kuambukiza katika Imperial College London, amezungmza na kipindi cha BBC cha Newsnight.

Madaktari na wauguzi mara nyingi huwa karibu sana na watu walioambukizwa na kusababisha hao wenyewe kupata virusi vingi zaidi mwilini, kumaanisha kwamba wako katika hatari ya kuambukizwa virusi vingi zaidi.

Monjwa mmoja aliefanyiwa upasuaji katika hospitali ya Wuhan china, aliambukiza wahudumu 14 wa afya hata kabla ya homa yake kupungua, kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Prof Barclay amesema: “Mfumo wako wa kinga, hata kama wewe ni mtu mwenye afya nzuri una wakati mgumu wa kukabiliana na virusi vyote mwilini.

“Kiwango cha virusi utakachoambukizwa kitakuwa ndio chenye kuweka wazi nguvu ya mwili wako ya kupigana na virusi hivyo, vita ambavyo ni kati ya virusi na mfumo wako wa kinga ya mwili.

“Ikiwa utaambukiza wanyama, kwa mfano, kwa viwango tofauti vya virusi, wale ambao wataambukizwa kiwango kikubwa cha virusi ndio watakao kuwa wagonjwa.”

line

Covid-19 inaingia vipi kwenye mwili wako?

A body with animations of coronavirus

Chanzo cha picha, Getty Images

Ikiwa mtu ameambukizwa virusi vya Covid-19 ambavyo pia vinafahamika kama Sars-CoV-2, huenda vikajikita upande wa juu wa wa njia ya kupumua vikiwa tayari kusambaa kupitia pumzi au kukohoa.

“Kila wakati tunapozungumza au kupumua, tunatoa matone ambayo yanatoka kwenye pua na koo na huruka nje hadi hewani,” Profesa Barclay amesema hivyo katika kipindi cha Newsnight.

Baadhi ya matone haya pia huruka na kutua kwenye maeneo mbalimbali. Hii ndio sababu mara nyingi huwa tunaarifiwa ni muhimu kutokaribiana na pia unatakiwa kuosha mikono kila mara.

Bado haijafahamika ni chemchembe ngapi mtu atakuwa nazo mwilini ndio aanze kuugua.

“Kwa homa ya mafua, kwa kirusi kinachofahamika, mtu anaweza kuwa mgonjwa akipata chembechembe tatu pekee nambazo huanza maambukizi. Kwa Corona bado haijafahamika ni chembechembe ngapi zinazosababisha maambukizi lakini kuna uwezekano ni kidogo mno,” Profesa Barclay amesema.

line

Waliokatika mstari wa mbele kuambukizwa

Haijulikani ni mara ngapi mhudumu wa afya akimuhudumia mgonjwa anaweza kuambukizwa.

Lakini dada kutokana na mlipuko wa SARS mwaka 2002-2003 unapendekeza kwamba asilimia 21ya visa vya corona vilikuwa vimesababishwa na wahudumu wa afya, kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Hilo limejitokeza tena kwa wale wanaosimamia wagonjwa wa Covid-19.

Nchini Italia, zaidi ya watu 6,200 ambao walithibitishwa kwamba wameambukizwa virusi vya Corona walikuwa ni wahudumu wa afya.

Nchini Spaini, inakadiriwa kwamba visa 6,500 au asilimia 12% ya walioambukizwa ni wahudumu wa afya.

A Spanish healthcare worker wears a mask

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nchini Spain, wahudumu wa afya walioambukizwa ni asilimia 12

Na mwanzoni mwa Machi, China ilikadiria kwamba wahudumu wa afya 3,300 walikuwa wameambukizwa.

Hii inamaanisha kwamba kati ya asilimia 4-12 ya visa vilivyothibitishwa ni vya wahudumu wa afya.

Afisa mmoja mwandamizi wa wahudumu wa afya Uingereza ameiambia BBC kwamba hadi asilimia 50 ya wafanyakazi wa hospitali hanaumwa.

Na wakati watu wakidhani kwamba hospitali ni sehemu ya kudhibiti maambukizi hayo, huenda ikawa chanzo kikuu cha virusi vya corona.

Kupitia BBC, madaktari wamesema kwamba walijitahidi kuwaruhusu wagonjwa ambao hawakuwa wanaugua corona kurejea nyumbani hata kabla hawajapona, kujaribu kuwalinda wasiambukizwe.

Maelezo zaidi
Banner

Kinga dhaifu

Health workers in Zimbabwe have gone on strike as the country enters a 3-week lockdown

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wahudumu wa afya Zimbabwe wamegoma wakati ambapo amri ya kutotoka nje imetangazwa kwa wiki ya tatu.

Hatari ya maambukizi ndio sababu ambayo imefanya wahudumu wa afya katika nchi nyingi duniani wamekasirishwa na ukosefu wa vifaa vya kutosha vya kujikinga.

Ufaransa, madaktari wamechukua hatua ya kisheria dhidi ya serikali kwa kile ambacho wanasema ni kushindwa kuzalisha barakoa kwa wingi ambako wanasema kunawaweka katika hatari ya kupata maambukizi.

Madaktari na wauguzi nchini Zimbabwe wamegoma wakilalamikia ukosefu wa vifaa vya kujikinga huku nchi hiyo ikiwa imeanza amri ya kutotoka nje kwa wiki tatu kama njia moja ya kujaribu kudhibiti usambaaji wa virusi vya coona.

Nchini Uingereza UK, Neil Dickson, mkuu wa chama cha wahudumu wa afya Uingereza, amesema kwamba ukosefu wa vifaa vya kutosha vya kujikinga kumetoa imani ya madaktari na wauguzi.

Ingawa serikali ya Uingereza imenza kutumia jeshi kusambaza mamilioni ya barakoa kwa wahudumu wa afya, "Itachukua muda kurejesha uaminifu uliokuwepo", Dickson anaamini hivyo.

"Tatizo jingine ni kwamba uzalishaji wa barakoa kwa ujumla unafanyika Asia. Na China, imekuwa na changamoto kuhakikisha kwamba uzalishajishaji huo unaendelea kuwepo."