Coronavirus: Shirika la Afya la Duniani latoa angalizo dhidi ya kasi ya maambukizi

Chanzo cha picha, Getty Images
Shirika la afya duniania (WHO) limetoa angalizo kuhusu ongezeko la kasi la maambukizi ya virusi vya corona , ikiwa zaidi ya wagonjwa wapya 300,000 wakiwa wamethibitishwa kuwa na virusi hivyo.
Ni siku 67 sasa tangu ilipotiwa kwa mara ya kwanza kuwa wagonjwa wa Covid-19 walifikia 100,000 , baada ya siku 11 waliripotiwa wengine 100,000, na baada ya siku nne tu, kwa mara ya tatu wagonjwa wengine 100,000 waliripotiwa.
Hata hivyo Mkurugenzi WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amsema kuwa bado kuna namna ya kukabiliana na janga hili.
Ametaka mataifa kuzingatia vipimo na kufuatilia wale ambao walikuwa wamehusiana na waliokuwa na maambukizi.
"Kile ambacho kinazingatiwa zaidi ni nini tunafanya. Huwezi kushinda mechi ya mpira wa miguu kwa kulinda goli tu , unapaswa kushambulia pia , rais wa shirikisho la soka dniani-Fifa Gianni Infantino alizungumza hayo wakati akianzisha kampeni ya wachezaji mpira ya kutokomeza virusi vya corona.

Dkt. Tedros alisema kuwa kuwataka watu kubaki nyumbani na kuchuukua hatua ya kujitenga na wengine ni hatua muhimu ambazo zinaweza kusaidia kukabiliana na maambukizi haya taratibu lakini akatafsiri jitihada hizi kuwa ni njia za kujilinda na hazitasaidia kupata ushindi.
"Ushindi , unahitaji virusi hivi vishambuliwe kwa nguvu zote na mbinu zenye kudhamiria ushindi - kupima kila mtu, kuwatenganisha na kuwaangalia kwa karibu wale waliobanika kuwa na maambukizi, kuwafuatilia wale waliohusiana na yule aliyethibitishwa kuwa na maambukiz na kuwaweka karantini."



Chanzo cha picha, AFP
Dkt.Tedros ameeleza kuwa kengele ya kutuamsha imepiga kupitia ripoti ambazo zimeripotiwa ulimwenguni kote kuwa na idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya corona na kati ya walioambukizwa, wahudumu wa afya wamo pia wakionekana kukosa vifaa vya kujikinga wakati wa kutoa huduma.
"Wahudumu wa afya wanaweza kufanya kazi yao vizuri endapo kuna usalama katika kazi wanayoifanya," alionya. "Hata kama tutafanya kila kitu kwa uhakika, kama hatutaweka kipaumbele cha kuwalinda wahudumu wa afya basi watu wengi wataufa kwa sababu wahudumu wa afya ambao wangetulinda na afya zetu nao wanaumwa."
Alisema kuwa WHO limekuwa likifanya kazi na washirika wengine na kusisitiza kutoa kipaumbele cha matumizi ya kutumia vifaa vya kujilinda na kutangaza kuwa kuna uhaba wa vifaa kwa dunia nzima kwa jumla.
Lakini alisisitiza kuwa:"Hatua hizo zinafanya zoezi la kukabiliana na virusi vya corona kwenda taratibu na virusi kusambaa zaidi na hata kusababisha matokeo ambayo hatukua tumeyatarajia na hii ni kwa sababu ya uhaba wa vitendea kazi na vifaa vya kujikingia na kwafanya wahudunu wa afya kufanya kazi kwa ufanisi bila kuzurika."
Mkuu huyo wa shirika la afya duniani-WHO ametaka mataifa washirikiane na kuahidi kutekeleza suala hili kidunia na kusema kuwataka mataifa makubwa duniani ya kundi la G20 group kufanyia kazi suala hilo wiki hii ili kuhakikisha vifaa vinatengenezwa na kusambazwa, kuzuia usafiriishaji wa kutoka sehemu moja mpaka nyingine kunafanya mahitaji muhimu yakosekane.













