Je ni kwa nini mama huyu alimuoa binti mwenye umri wa mwanawe?

Phyllis Irwin kulia na Lillian Faderman, waliamua kuoana

Chanzo cha picha, Lillian Faderman

Maelezo ya picha, Phyllis Irwin kulia na Lillian Faderman, waliamua kuoana
Iliyochapishwa

Mwaka 1971 kufuatiwa kuzinduliwa kwa vuguvu la wanawake la women liberation movement , Profesa wa Chuo kikuu cha jimbo la California Lillian faderman aliwasiliana na mkurugenzi mmoja wa kituo hicho Phyllis Irwin kufungua programu ya utafiti wa wanawake.

Ilikuwa mwanzo wa mapenzi yaliodumu nusu karne , lakini yakakumbwa na changmoto nyingi si haba. Wakati walipokutana kwa mara ya kwanza mapenzi ya jinsia moja yalikuwa haramu.

'Tulionekana kuwa wahalifu karibia katika kila jimbo', wanasema wanandoa hao. ''Wapenzi wengi wa jinsia moja , walikuwa wakijificha'', wanasema.

Lakini hilo halikuwazuia kuanzisha familia moja na kufanya sheria kutambua kundi la familia yao.

Katika mahojiano na kipindi kimoja cha redio cha idhaa ya BBC, wanawake hao walisema jinsi walivyopata mbinu ya kutumia sheria ili familia yao iweze kutambuliwa, swala ambalo hawakufaidika nalo wakati jamii ilipokuwa ikilipinga.

Wakati walipoanza kuchumbiana, hawakujionyesha moja kwa moja kuwa wapenzi wa jinsia moja. Wakati huo tulikuwa tukifunga midomo yetu na kuendelea na mashai yetu, alisema Phyllis, ambaye ana umri wa miaka 91 leo.

Miaka ya 1970 mapenzi ya jinsia moja yalikua na adhabu kali nchini Marekani

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Miaka ya 1970 mapenzi ya jinsia moja yalikua na adhabu kali nchini Marekani

''Lakini wengine walidhania kwamba walijua uhusiano wetu katika chuo kikuu. Walituita Phyllis na Lills kwa sababu tulikuwa pamoja mara kwa mara'', alicheka lilian.

''Nadhania wenzetu walituelewa , na nilipoanza kuchapisha vitabu kuhusu historia ya wapenzi wa jinsia moja , niliona kana kwamba kila mmoja wetu alielewa kwamba tulikuwa wanandoa''.

Miaka mitatu baada ya kuendelea na uhusiano wao, waliamua kupata mtoto. Lilian ambaye ni mdogo kwa miaka 11 alienda kumuona mtaalamu wa maswala ua ujauzito.

Kupewa ujauzito kwa njia ya kisayansi halikjuwa jambo la kawaida. Na Hususan kama wewe huna uhusiano wowote wa kimapenzi na mwanamume.

Lakini Lillian alifanikiwa kumshawishi daktari kumsaidia, bila kusema sababu za kumfanya yeye kutaka kuwa na mtoto bila kuwa na uhusiano na mwanamume.

''Daktari aliniuliza kwa nini sijaolewa iwapo nataka kuwa na mtoto'', anakumbuka.

''Nilijibu: Nina umri wa miaka 34, nina shahada ya udaktari na wadhfa wa naibu wa rais wa maswala ya elimu katika chuo na nadhani inagharimu kupata wanaume''.

Daktari alijibu kwa urahisi: Naelewa unachosema na alinipachika mimba hiyo kupitia mbinu hiyo ya kisayansi ambayo ilifanikiwa.

Lilian alimshawishi daktari kwamba kutokana na umri wake mkubwa na cheo chake ingekuwa gharama kwake kutafuta mume wakati ambapo alitaka kuwa mama

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Lilian alimshawishi daktari kwamba kutokana na umri wake mkubwa na cheo chake ingekuwa gharama kwake kutafuta mume wakati ambapo alitaka kuwa mama

''Sheria hiyo inasema kwamba wanawake wawili hawakuweza kuoana - tungefurahia kuoana - sheria inasema kwamba haiwezekani mtoto kuwa na wazazi wa jinsia moja , na tulijua kwamba ilikuwa muhimu kuwa na mshikamano wa kisheria kwa sababu ya Avrom''

''Hivyobasi tulifanya hivyo. Hatukuhisi vibaya hata kidogo'', alisema.

Wanawake hao waliamua kuitumia hadithi hii sio tu kwasababu za kisheria.

Faida ya kuchukua mtoto na kuishi naye ni kwamba Avrom , ambaye alizaliwa wakati ambapo hakukuwepo watoto wengi wa wazazi wa jinsia moja , wakati alipokuwa mdogo angeweza kumtambulisha Phyllis kwa rafiki zake kuwa bibi yake.

''Nadhani hii ilikuwa rahisi kwake, ijapokuwa alijua kwamba Phyllis alikua mamake mwengine. Ana umri wa miaka 45 leo na bado anamuita mama Phyllis'', kulingana na Lillian.

Kwa upande wake, Phyllis anasema hakuwa na tatizo kuitwa bibi.

''Nilifurahi kwamba alikuwa anahisi vyema kunitambulisha mimi kama mtu muhimu katika maisha yake ,hivyobasi jina hilo halikunikera''.

Familia ya watu watatu

Mwaka 1975 , Lilian alijifungua mtoto kwa jina Avrom, mtoto wa pekee wa wanandoa hao. Phyllis alimpeleka hospitalini , lakini kutoka kwa ombi la Lilian aliyetaka kujifungua, ambaye alikuwa na hofu.

Kila kitu kilifanyika ilivyopangwa na mwanamke huyo akarudi nyumbani na mara familia ikawa na watu watatu.

Hatahivyo walianza kugundua vikwazo vya familia yao kisheria.

''Tulikuwa na wasiwasi mkubwa kwamba hakukuwa na sheria ya kutambua uhusiano wetu kisheria''.

''Kile kilichotutia wasiwasi zaidi ni kwamba Avrom alikuwa mgonjwa na Phyllis alilazimika kumpeleka kwa daktari, hakuwa mzazi wake kamili, hivyobasi nililazimika kumpatia barua rasmi aliyobeba''.

Lakini kile kilichonikwaza hasa ni kwamba iwapo kitu kingenitokea , asingekuwa na haki ya kisheria kudai kuwa mwanawe . Kisheria alikuwa mtu asiyemjua.

Wakati huo watu wa jinsia moja hawangeweza kuwa na uhusiano na mtoto mmoja.

Phyllis y Lillian na Avrom, mwaka 1979, wakati alipokuwa na umri wa miaka minne

Chanzo cha picha, Lillian Faderman

Maelezo ya picha, Phyllis y Lillian na Avrom, mwaka 1979, wakati alipokuwa na umri wa miaka minne

Lakini walipata njia ya kubuni familia iliotambulika.

Mama na mtoto

''Katika jimbo la California , iwapo kuna tofauti ya miaka 10 ama zaidi kati ya watu wawili wazima, mmoja anaweza kumchukua na kuishi naye'' , anasema Lilian.

Hivyo ndivyo Phyllis alikuwa anaweza kumchukua na kuishi naye na kuwa bibi yake Avrom.

Je haikuwa vibaya kwake kuwa mama na mtoto? Aliuliza Jo Fidgen, mwandalizi wa Outlook.

''Sikufikiria kwa mantiki hiyo, nilifikiria njia ya kuwa na uhusiano wa kisheria na Avrom'', alisema Phyllis, ambaye alicheka kwa kuwa mama ,mzazi wa Lillian, walikuwa na uhusiano wa kuchumbiana.

La zaidi Lilian alielezea: hatukuliona swala hilo kuwa baya kwa sababu hatukujihisi kama mama na mwanawe, tulifanya hivyo kama njia ya kukwepa sheria .

Phyllis y Lillian

Chanzo cha picha, Lillian Faderman

Maelezo ya picha, Kwa wanadoa hao ambao walikuwa pamoja kwa miaka 48 halikuwa jambo la kushangazakwa mmoja wao kuchukua mtoto na kuishi naye