Salah akaribia kutua Trabzonspor

Chanzo cha picha, Getty Images
Mohamed Salah anakaribia kukamilisha uhamisho wake kwenda Trabzonspor, huku Bayern Munich ikimsaka mshambuliaji wa Manchester United, Benjamin Sesko. Wakati huohuo, kocha wa Manchester City, Enzo Maresca, anatamani kufanya kazi tena na winga wa Chelsea, Pedro Neto.
Mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, 34, yuko karibu kukamilisha uhamisho wake kwenda klabu ya Trabzonspor ya Uturuki, licha ya kuwa awali alikubaliana kwa mdomo kujiunga na Besiktas baada ya kuondoka Liverpool msimu huu wa kiangazi. (Foot Mercato)

Chanzo cha picha, Getty Images
Bayern Munich bado haijakata tamaa ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Benjamin Sesko, ikimwona kama mrithi wa muda mrefu wa Harry Kane. Mpango huo unalenga kumpa Kane nafasi ya kucheza zaidi kama kiungo mshambuliaji katika siku zijazo. (CF Bayern Insider)

Chanzo cha picha, Getty Images
Beki wa Aston Villa na timu ya taifa ya England, Ezri Konsa (28), avutiwa na uwezekano wa kuhamia Arsenal, huku The Gunners wakimtazama kama chaguo la kuimarisha safu yao ya ulinzi. (Caught Offside)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kocha wa Manchester City, Enzo Maresca, anataka kuungana tena na winga wa Chelsea, Pedro Neto, 26, huku City ikijipanga na dau la pauni milioni 70 kumng'oa Chelsea. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Vigogo wa London, Chelsea na Tottenham, wameingia rasmi kwenye vita ya kuwania saini ya beki wa kati wa Atalanta, Giorgio Scalvini (22), huku Newcastle nayo ikiendelea kufukuzia huduma za nyota huyo wa Italia. Magpies wanadaiwa kuwa tayari kufungua mazungumzo kwa ofa ya pauni milioni 34 kwa ajili ya Nyota huyo, anayekadiriwa kuwa thamani ya pauni milioni 42. (The Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa Liverpool, Curtis Jones, anaonekana kuweka wazi dhamira yake ya kutaka kutua Inter Milan, baada ya ofa ya awali ya euro milioni 25 kukataliwa na Liverpool. Hata hivyo, mazungumzo bado yanaendelea, huku miamba hiyo ya Italia ikijiandaa kuimarisha dau lake hadi pauni milioni 30, kiwango kinachoweza kufungua mlango wa nyota huyo wa England mwenye miaka 25 kuhamia Serie A. (TeamTalk)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Chelsea, Joao Pedro, mwenye umri wa miaka 24, anatarajiwa kupewa mkataba mpya licha ya mkataba wake wa sasa kuendelea hadi mwaka 2032. Hatua hiyo inakuja baada ya Barcelona kuonyesha nia ya kutaka kumsajili nyota huyo, 24, wa kimataifa wa Brazil huku Chelsea ikitaka kumfunga zaidi kwa ajili ya mipango yake ya baadaye. (The Athletic)
Paris Saint-Germain imeongeza nguvu katika mbio za kumnasa winga mahiri wa Ajax, Mika Godts, anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 52. Hata hivyo, PSG inakutana na ushindani mkali kutoka kwa vigogo wa Ligi ya Primia Arsenal, Liverpool, Manchester United na Tottenham, zote zikiwa na taarifa ya kuongezeka kwa hamasa ya kumuwania nyota huyo wa Ubelgiji mwenye miaka 21. (TeamTalk)















