Wanajeshi wa Marekani walioathirika ubongo kutokana na shambulio la Iran wafikia 109

Iran iliishambulia kambi hiyo ya wanajeshi wa marekani ili kulipiza kisasi mauaji ya jenerali Qasem Suleimani

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Iran iliishambulia kambi hiyo ya wanajeshi wa marekani ili kulipiza kisasi mauaji ya jenerali Qasem Suleimani
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Idadi ya wanajeshi wa Marekani wanaougua majeraha ya ubongo kufuatia shambulio la Iran dhidi ya wanajeshi wa Marekani katika kambi moja nchini Iraq mwezi Januari imefikia 109, kulingana na maafisa wa Marekani.

Idadi hiyo iliongezeka kutoka wanajeshi 64 walioripotiwa hapo awali na Pentagon. Rais Donald Trump awali alisema kwamba hakuna raia wa Marekani waliojeruhiwa wakati wa shambulio hilo.

Shambulio hilo la tarehe 8 mwezi Januari linajiri huku kukiwa na wasiwasi kuhusu mauaji ya jenerali mmoja wa Iran. karibia asilimia 70 ya wanajeshi waliojeruhiwa wamerudi kazini , pentagon iliongezea katika taarifa.

Ongezeko la visa vilivyoripotiwa linatokana na majeraha madogo ikimaanisha kwamba dalili huchukua muda kujitokeza , Pentagon ilisema katika mkutano na vyombo vya habari mwezi Januari.

Mbunge wa chama cha Republic nchini Marekani Joni Ernst alitoa wito wa kutolewa kwa majibu zaidi siku ya Jumatatu.

''Ni muhimu kuwa na mpango wa kuwatibu hawa waliojeruhiwa'' .

"Nimetoa wito kwa Pentagon kuhakikisha usalama na utunzaji wa vikosi vyetu vilivyopelekwa ambao wanaweza kuwa na majeraha ya mlipuko nchini Iraq," aliandika katika twitter.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Mwezi uliopita Rais Trump alipuuzilia mbali uwepo wa majerha ya ubongo alipoulizwa juu ya athari ya shambulio hilo.

"Nilisikia kuwa walikuwa na maumivu ya kichwa, na mambo kadhaa, lakini ningesema, na naweza kuripoti, sio mbaya sana," alisema.

Alipoulizwa kuhusu majerha ya ubongo au TBI alisema: "Sidhani kama ni majeraha makubwa sana ikilinganishwa na majeraha mengine ambayo nimeona."

Kambi ya Al Asab nchini Iraq ilioharibia na mashambulio ya kulipiza kisasi mauaji ya kamanda mkuu wa Iran
Maelezo ya picha, Kambi ya Al Asab nchini Iraq ilioharibia na mashambulio ya kulipiza kisasi mauaji ya kamndan mkuu wa Iran
Presentational white space

Je majaraha mabaya ya ubongo ni yapi?

Majeraha ya TBI hupatikana sana katika maeneo ya vita , kulingana na jeshi la Marekani.

Sababu kubwa ya TBI kwa wanajeshi waliopelekwa katika maeneo ya vita ni milipuko, kulingana na kituo cha Ulinzi cha Marekani kinachokabiliana na majeraha ya ubongo.

Majeraha hayo hutajwa kuwa madogo , kiwango cha kadri ama mabaya zaidi. Majeraha madogo ya TBI hutajwa kuwa mshtuko. na unaweza kusababishwa na mlipuko.

Shinikizo ya juu ya anga ikifuatiwa na shinikizo ndogo au ukosefu wa hewa. ". Ukosefu huo wa hewa unaweza kuingiza vitu hatua inayowafanya wanajeshi kuumia na hivyobasi kupata jeraha.

Zaidi ya wanajeshi 400,000 wamepatikana na TBI tangu 2000 kulingana na serikali ya Marekani.