Makombora kadhaa yaliyorushwa kutoka Iran yalilenga eneo la Irbil na Al Asad

Maelezo ya video, Tazama Iran ilivyoshambulia kambi za majeshi ya Marekani
Iliyochapishwa

Iran imefanya mashambulio ya makombora dhidi ya ngome za kijeshi za Marekani nchini Iraq kama hatua ya kulipiza kisasi mauaji ya jenerali Qasem Soleimani.

Makombora kadhaa yaliyorusha kutoka Iran yalilenga eneo la Irbil na Al Asad, magharibi mwa mji wa Baghdad.

Haijabainika ikiwa kuna majeruhi yoyote yaliyotokana na shambulio hilo.