Coronavirus: Mgonjwa wa nne agunduliwa Uingereza

Iliyochapishwa

Mgonjwa wa nne aliyeambukizwa virusi vya corona amegunduliwa Uingereza, kulingana na afisa mkuu wa tiba Uingereza.

Kisa hiki kipya kilikuwa kinafuatiliwa na wataalamu baada ya kubainika kwamba mgonjwa alikuwa ametangamana na mtu mwingine aliyepata virusi hivi Ufaransa.

Hii inawadia baada ya raia wa Uingereza na wengine wa kigeni karibia 200 kuhamishwa kutoka mji wa Wuhan kwa ndege ya mwisho ya Uingereza ambayo iliwasili katika uwanja wa ndege wa RAF Brize Norton Jumapili.

Kumekuwa na visa zaidi ya 37,000 vingi vikiwa ni kutoka Uchina chimbuko la virusi la corona.

Idadi ya waliokufa kwa virusi vya corona kwa sasa ni juu zaidi kuliko idadi ya waliokufa kwasababu ya virusi vya Sars mwaka 2003, kulingana na maafisa wa afya nchini Uchina.

Mwaka 2003 idadi ya waliokufa kwasababu ya virusi vya Sars ilifikia 774.

Katika taarifa iliyotolewa Jumapili, Profesa Chris Whitty, afisa mkuu wa tiba Uingereza, amesema kwamba mgonjwa wa hivi karibuni Uingereza amehamishwa hadi hospitali ya kitaifa ya Royal Free hospital kaskazini ya Uingereza.

"Kwasasa tunachukua hali ya tahadhari kuzuia uwezekano wa kusambaa kwa virusi hivyo," amesema.

"Hospitali ya kitaifa imejitayarisha vilivyo kukabiliana na visa hivi na kutoa tiba, na pia inajitahidi kutafuta wale ambao huenda wametangamana na mgonjwa wa sasa.

Meanwhile, a British man has been diagnosed with coronavirus in Majorca after contact with a carrier in France.

Wakati huohuo, mwanamume mmoja raia wa Uingereza amegunduliwa na virusi vya corona katika kisiwa cha Majorca baada ya kutangamana na mtu aliyekuwa na virusi hivyo Ufaransa.

Ofisi ya mambo ya nje imesema kuwa ndege hiyo ilikuwa ya pili na ya mwisho kutoka kwa serikali kuchukua wale waliokwama katika mji wa Wuhan kitovu cha virusi ipya vya corona.

Waliobebwa na ndege hiyo ni pamoja na raia 105 wa Uingereza na familia zao pomoja na raia 95 wa Ulaya. Pia wafanyakazi 13 na wahudumu wa afya walikuwa kwenye ndege hiyo.

Waliohamishwa wamepelekwa eneo la Milton Keynes na watawekwa katika karantini kwa siku 14 ili kuchunguzwa afya zao.

Balozi wa Uingereza Beijing, Dame Barbara Woodward, ameiambia BBC kwamba raia wawili wa Uingereza waliotaka kujumuishwa kwenye safari hiyo walizuiliwa baada ya joto la mwili kuwa juu wakati wa ukaguzi nchini Uchina.

Kwengineko, katika visiwa Balearic, serikali imethibitisha kwamba mwanamume mmoja amepatikana na virusi vya corona.

Mwanamume huyo amelazwa katika hospitali ya Palma Ijumaa, pamoja na mke wake na binti zake wawili. Familia yake nyengine wamebainika kwamba hawajaambukizwa virusi hivyo.

Wizara ya afya imesema inachunguza uwezekano wa yeyote ambaye huenda alitangamana na mwanamume huyo.

Zaidi ya raia 100 wa Uingereza na familia zao wamehamishwa hadi Uingereza kwa ndege zilizosimamiwa na serikali na nchi zingine.

Raia hao wako kwenye karantini katika hospitali ya Arrowe Park huko Wirral.

Wale waliorejeshwa hivi sasa ambao watatengwa kwa wiki mbili hotelini, wataruhusiwa kusoma majarida, vitabu, kupata vifaa vya kuchezea vya watoto, gemu, simu za mikononi, na hata kuwa na intaneti, hospitali ya taifa imesema.

Nguo za kubadilisha na bidhaa za zingine ziliwekwa kabla ya wao kufika tofauti na abiria wa awali waliohamishwa kutoka Wuhan ambao waliruhusiwa tu kusafiri na mabegi yenye uzito wa kilo 15 pekee.

Hatua ya ndege kuchukua wale waliokwama Wuhan imewadia baada ya uamuzi ulitolewa na Wizara ya mambo ya nje Februari 4 kwamba raia wote wa Uingereza waondoke nchini Uchina iwapo wanaweza kufanya hivyo.

Mashirika ya ndege ya Uingereza na Virgin Atlantic yamesitisha safari zake kwenda Uchina ingawa mashirika mengine bado yanaendeleza safari zao katika Uingereza na Uchina.

Wizara ya afya ya Uchina imesema idadi ya waliothibitishwa kuwa na virusi hivyo hadi Jumapili asubuhi imefikia 37,198.

Kufikia Jumamosi mchana jumla ya watu 686 walikuwa wamefanyiwa vipimo kuthibitisha iwapo wana virusi vya corona kulingana na wizara ya afya ya Uingereza.

Dalili za virusi vya corona

Virusi vya corona vinasababisha maambuzi katika mapafu na kusababisha matatizo ya kupumua.

Dalili zake ni kuwa na joto jingi mwilini ikifuatiwa na kikohozi kikavu, kuwa na homa, kisha baada ya wiki moja, mwathirika anakuwa na matatizo ya kupumua na kuhitaji matibabu kwa haraka.

Virusi hivi vipya pia huathiri wanyama.

Virusi vipya ya Corona vinaambukiza wakati wa kuatamia mayai - na dalili zinakuwa bado hazijaanza kujitokeza na kufanya iwe vigumu kudhibitika, wamesema maafisa wa China

Kipindi cha kuatamia mayai wakati ambao mtu ameambukizwa virusi lakini hakuna dalili zozote zinazojitokeza ni kati ya siku 1 hadi 14, maafisa wanaamini hivyo.

Bila ya kujitokeza kwa dalili mtu hawezi kufahamu ikiwa ameambukizwa virusi vya Corona lakini pia vinaweza kusambaa kwa wakati huo huo.