Chukwuemeka Ike: Mfalme wa Nigeria mwandishi wa kitabu 'Toads for Supper'

Iliyochapishwa

Mwandishi wa Nigeria Chukwuemeka Ike, aliyeaga dunia mwezi uliopita akiwa na umri wa miaka 88, alikuwa na mchango mkubwa katika utamaduni wa Nigeria lakini hakuwahi kutambuliwa kimataifa, ameandika mwandishi wa BBC Nduka Orjinmo mjini Lagos.

Ike atakumbukwa kwa riwaya zake lakini urithi alioacha utaendelea kuwepo daima nchini Nigeria.

Sema neno "expo" kwa yeyote yule hapa na moja kwa moja watakuwa na ufahamu wa kile unachozungumzia - vitendo udanganyifu visivyokubalika wakati wa kufanya mtihani.

Ike alisaidia sana neno hili kuwa mashuhuri katika maonesho ya kibiashara ya 77, neno aliloliandika katika riwaya yenye kuakisi maisha ya kweli vile mtihani ulivyovuja katika shule mashuhuri mara mbili mwaka 1977.

Kinaya ni kwamba alikuwa miongoni mwa bodi ya mtihani wakati sakata hiyo inatokea na akaamua kutoa yaliyokuwa yanamkera kuhusu vile jamii inavyoendeleza maadili mabaya - kuanzia wazazi, wanafunzi hadi kwa utawala wa shule kupitia kazi yake ya fasihi.

Riwaya yake hiyo ilipaza sauti kwa masuala ya sasa na kutetea Afrika hususan kwa utamaduni wa Igbo.

Wakati kauli mbiu ya wakati huo ilikuwa imejikita kwenye mapigano yaliyokuwepo kati ya nchi za Magharibi na Afrika, ni mmoja wa waandishi wa awali kabisa waliozungumzia mambo mbalimbali nchini Nigeria.

Hakuzungumzia tu misemo ya Afrika ya wakati wa nyuma. Pia aliangazia siku za mbeleni: na kumgusa kila mmoja kuanzia mwanasiasa hadi kahaba na kubashiri matatizo yaliyokuwa yanakuja siku zijazo.

Kujibadilsha na kuwa chui

Alikuwa mtu mwenye kuzungumza kwa kinaya na aliangazia taasisi kwa kuzikejeli japo kwa maneno ya tamu chungu. Alitafuta mambo ya kudhihaki tu katika Nigeria ya kisasa.

Katika kitabu chake cha kwanza, Vyura kwa chakula cha Jioni yaani Toads for Supper aliangazia mapenzi kwa namna ya ucheshi na kuonyesha wasiwasi uliokuwepo katika makabila mbalimbali ya Nigeria.

Riwaya hiyo ambayo mandhari yake ni Chuo Kikuu cha Nigeria magharibi mwa Afrika katika taifa ambalo ni maaufu, inazungumzia simulizi ya mwanafunzi, Amadi ambaye alikuwa wa kwanza kujiunga na chuo kikuu katika kijiji chake mashariki mwa Nigeria.

Kitabu hicho kilimuakisi aliyedhamiriwa kuwa mwanafunzi wa kabila la Igbo magharibi mwa Nigeria kabla ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, kulikochochewa na kugawanyika kwa kabila la Igbo na Biafra, 1967.

Ike aliviita vita vya wenyewe kwa wenyewe kama kipindi muhimu katika historia ya Nigeria.

Baadaye alijaribu kutofautisha kati ya kabila la Biafra na kilichojumuisha utamaduni wa kabila hilo.

Katika kitabu hicho alizungumzia maafa yaliyotokea kupitia Fatima ambaye anatoroka kwa kutumia ndege za adui akiwa na kijana wake mdogo.

Katika simulizi ya riwaya hiyo, mwanafunzi wa shule, kijana ambaye amechaguliwa na mizimu ya mababu zake kuwa na nguvu ya ajabu kwa kizazi chake: nguvu ya kubadilika na kuwa chui.

Wengi wanaichukulia kazi hii yake kama bora zaidi lakini lakini hii huenda ni kwasababu ilisomwa na vizazi vingi.

Ushawishi wa Achebe

Alizaliwa katika familia ya kifalme mashariki mwa Nigeria, Ike alikuwa mwanafunzi katika chuo kikuu maarufu cha serikali cha Umuahia ambapo waandishi wengi walisomea hapo.

Mwandishi mashuhuri Chinua Achebe alikuwa kama mwanafunzi, mkubwa wake aliyemuongoza kwa mengi akiwa shule ya upili na kuna wakati ambapo Ike alisema katika mahojiano kwamba Achebe alikuwa na mchango mkubwa sana katika kumtia moyo kwenye safari yake ya kuwa mwandishi.

"Sikuwahi kufikiria kuhusu kuandika riwaya hadi Chinua Achebe alipochapisha kitabu chake cha Things Fall Apart, 1958," amesema.

Pengine halikuwa jambo zuri sana kuwa mwandishi wa Igbo karne moja na Achebe.

Wengi wanaamini kwamba hili lilibadilisha fikra za Ike na kwamba uandishi wake ulihitaji kupata wasomaji wengi zaidi.

Hilo pia linaweza kufananishwa na waandishi wengine nguli wa Nigeria wakati huo kama vile Cyprian Ekwensi, Mabel Segun na Elechi Amadi. Lakini wote hao walionekana kufunikwa na Achebe na Wole Soyinka.

Kilikuwa kipindi cha waandishi waliokuwa na wakati mgumu kufasiri maneno ya kabila lao kwa maana za moja kwa moja hadi Kiingereza.

Na ni katika hili ambapo Ike hawezi kuachwa nje linapokuja suala la fwaandishi bora wa fasihi.

Mara nyingi katika uandishi wake alifanikiwa kujumuisha mfumo mpya wa uzungumzaji wa makibala mbalimbali.

Aliakisi uwezo wao wa kubadilisha namna ya kuzungumza kutoka maneno maarufu ya kabila fulani hadi Kiingereza, lugha za mitaani, lugha za vijana hadi Kiingereza cha mtaani na hata lugha ya asili.

Maonesho ya 77, hatua iliyochukuliwa na afisa wa polisi kumsaidia msichana mmoja kwa kutumia visodo na kudanganya katika mtihani ilikuwa maarufu katika uandishi wa Ike wakati huo.

Mwaka 2008, alianza kutetea utamaduni wake katika kurasa za kitabu hadi utawala wa mfalme Ndikelionwu mashariki mwa Nigeria. Kisha akachukua nafasi ya kutawala baada ya kifo cha baba yake.

Aliondoa kafara ya wanyama

Familia ya Ike ilikuwa imetawala kwa miongo mingi lakini watu wake walikuwa hawajapata mtu ambaye anataka kudumisha utawala na wakati huohuo kubadilisha utamaduni.

Mwaka 2018, aliomba watu wake kuacha kutoa sadaka ya wanyama kwa miungu wa ardhini Ala wakati wa sherehe za kuvuna viazi vikuu.

Badala yake alitaka kufanyike ibada ya kikiristo ya kumshukuru Mungu katika Kanisa la Anglican ambapo kawaida mstari wa mbele ulikuwa unahifadhiwa kwa ajili ya familia yake.

Mwandishi huyo ambaye alizungumzia utamaduni wa Afrika katika vitabu vyake. Na kuzungumzia vile wanaume walivyobadilika na kuwa chui. Alihisi kuwa sadaka haistahili tena kuhusishwa na watu na wengi wao wakakubaliana naye.

Kama mfalme, aliheshimu na kuzingatia haki kwa wote na pia alipenda demokrasia na kushirkiana na mabaraza madogo kufanya maamuzi.

Wanamuelezea kama mtu aliyekuwa mnyenyekevu, mpenda amani aliyetawala kwa ujasiri.

Watu wake wanasema kama mfalme bado yuko hai, lakini ameenda kuungana na mababu zake. Wamekataa kabisa kuzungumza akuhusu kifo chake, na wala hawamzungumzii kama mtu ambaye hayuko tena duniani.

Mtazamo wa aina hii huenda ndio uliomfanya Ike kuwa na fahari ya utamaduni wake. Mfalme huyu

huenda amekufa lakini anaishi kwa riwaya zake alizoandika.