Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Sudan: 29 wahukumiwa kifo mauaji ya mwalimu
Mahakama nchini Sudan imewahukumu polisi kifo kwa kumtesa na kumuua mwalimu.
Ahmad al-Khair, 36, alikufa wakati ameshikiliwa na polisi baada ya kukamatwa wakati wa maandamano ya kumtoa Rais Omar al-Bashir madarakani.
hii ni moja ya kuhumu za mwanzo kabisa kutolewa mara baada ya machafuko ya kuleta utawala wa demokrasia nchini Sudan.
Unaweza kusoma zaidi
Hakimu anasema kuwa hukumu hizo za kifo ni sehemu ya kutoa funzo.
Baada ya hukumu Jaji aliwauliza kaka wa l-Khair kama anataka polisi hao wasamehewe , lakini alikataa na kusema anataka wauwawe.
Mwanasheria wa upande wa watetezi anasema kuwa atakata rufaa.
Pia mahakama imegundua kuwa Ahmad Al-Khair alipigwa na kuteswa hadi kufa na maafisa wakati amekamtwa kwenye eneo la utesaji huko jimbo la Kassala.
Chini ya rais aliyeondolewa madarakani Bashir, hukumu ya kifo ilipitishwa na watu wawili kuuwawa.
Kesi ya Ahmad Al-Khair imejizolea umaarufu mkubwa Sudan na kifo chake kilizua hasira kali kwa waandamaji. idadi kubwa ya watu walikusanyika kusikiliza kesi hiyo nje ya mahakama katika mji pacha na mji mkuu wa Khartoum.
Takribani watu 170 waliuwawa wakati wa maandamano dhidi ya Serikali. Bashir aliondolewa madarakani na jeshi baada ya kupata madaraka miaka 30 iliyopita kwa njia ya mapinduzi.
Bashir Mapema mwezi uliopita alihukumiwa miaka miwili kwa kosa la rushwa, mahakama iliamua awekwe kwenye kituo cha kijamii kwani umri wake ni mkubwa sana kukaa jela.
Unaweza pia kusoma:
Bashir bado anasakwa na Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu dhidi ya binadamu.
Muda mfupi kabla ya kusomwa kwa hukumu dhidi yake, baadhi ya wafuasi wa rais huyo wa zamani walianza kushangilia kwa sauti ya juu wakisema kesi ilikuwa ni ya kisiasa, na baaadae hakimu aliwaamuru watoke nje ya mahakama.