Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mkimbizi wa Sudan Kusini awasamehe vijana wa Misri waliomlenga kwa ajili ya rangi yake
Mkimbizi kutoka Sudan Kusini ambaye alidhulumiwa na Wanaume watatu kutoka Misri mjini Cairo mwezi jana, ameliambia Kongamano la World Youth Forum, kwamba amewasamehe waliomdhulumu na anataka kusonga mbele na maisha yake. Video ya John Manut mwenye umri wa miaka 16 ilivuma katika mtandao wa Kijamii wa Tik Tok ikionyesha akikabiliwa na vijana wawili raia wa Misri alipokuwa akienda shuleni.
Mtu wa tatu anayechukua video anaweza kusikika akicheka huku wanaume hao wakiendelea kumtania mwanafunzi huyo. Wanaume hao wote watatu wamekamatwa na kuachiliwa kwa dhamana. Bw Manut anasema alilengwa kwa ajili ya rangi yake.
"Ni vibaya kumyanyasa mtu kwa ajili ya rangi yake kwani mwisho wa siku sisi sote ni binadamu na tuko sawa. Iwapo nitakutana nao tena hii leo, sina kinyongo chochote Kwani nimewasamehe lakini walichofanya sio Sawa." Alisema. Mwanafunzi huyo alikuwa mgeni wa heshima wa rais Abdel Fattah el Sisi ambaye alimwalika katika Sherehe za ufunguzi za World Youth Forum Mwanafunzi huyo alikuwa amekaa kando ya rais el Sisi Katika kongamano hilo, linalowaleta pamoja vijana kutoka kote ulinwenguni, likipofunguliwa katika mji wa Sharm el Sheikh.