Omar al Bashir ahukumiwa kufungwa miaka miwili katika kituo cha kijamii

Iliyochapishwa

Rais wa zamani wa Omar al Bashir amehukumiwa kifungo cha miaka miwili katika kituo cha kijamii kwa ufisadi.

Kesi hiyo ilihusu fedha za kigeni zenye thamani ya dola milioni 25, zilizopatikana katika nyumba ya Bwana Bashir muda mfupi baada kung'olewa madarakani mapema mwaka huu.

Bashir bado anasakwa na Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu dhidi ya binadamu.

Muda mfupi kabla ya kusomwa kwa hukumu dhidi yake, baadhi ya wafuasi wa rais huyo wa zamani walianza kushangilia kwa sauti ya juu wakisema kesi ilikuwa ni ya kisiasa, na baaadae hakimu aliwaamuru watoke nje ya mahakama.

Waliendelea na maandamano nje ya mahakama wakisema : "Hakuna mungu kuna Mungu."

Kesi yake yake ya udisadi ilihusiana na dola milioni $25 taslimu za malipo alizopokea kutoka kwa Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman.

Bashir calidai malipo hayo yalifanyika kama sehemu ya mkakati wa Sudan wa mahusiano na Saudi Arabia, na "hazikutumiwa kwa maslahi ya kibinafsi bali kama misaada ".

Baada ya hukumu kutolewa mmoja wa mawakili wa kiongozi huyo aliyeng'olewa madarakani, Ahmed Ibrahim, aliliambia shirika la habari la AFP kwamba watakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama.

Mohamed al-Hassan, ambaye ni wakili mwingine wa Bashir, awali alisema kuwa upande wa utetezi haukuichukulia kesi kama iliyokuwa ni ya kisheria bali ilikuwa ni ya "kusiasa" .

Bwana Bashir alikuwa anakabiliwa na kifungo cha miaka kumi gerezani kwa uhalifu, kwahivyo wengi watakiona kifungo cha miaka miwili gerezani kama cha huruma.

Lakini hakimu alisema kuwa kulingana na sheria ya Sudan watu wenye umri wa Zaidi ya miaka 70 hawahutumikii kifungo jela, na kwahivyo Bashir mwenye umri wa miaka 75- atatumikia adhabu yake katika kituo cha jamii cha kubadili.

Kesi ilianza vipi?

Mnamo Juni, waendesha mashtaka wamesema kiwango kikubwa cha fedha za kigeni zilizohodhiwa ziligunduliwa katika magunia ya nafaka nyumbani kwake.

Wanaharakati wa kutetea demokrasia na viongozi wa jeshi nchini humo waliomtimua madarakani Bashir, walisaini makubaliano yanayotoa fursa kufanyika uchaguzi mkuu nchini.

Kiongozi huyo wa zamani, aliyefika mahakamani na kusimama kizimbani alikuwa amevaa nguo nyeupe na kilemba. Hakujibu tuhuma zinazomkabili, Shirika la habari la Reuters linaripoti.

Kumekuwa na maafisa wengi wa usalama walioshika doria nje ya mahakama katika mji mkuu Khartoum, wakati Bashir alipowasili.

Bashir anakabiliwa na mashtaka gani mengine Sudan?

Mnamo Mei, nwendesha mashtaka nchini Sudan alimshtaki Bashir kwa uchochezi na kuhusika katika mauaji ya waandamanaji.

Mashtaka hayo yanatokana na uchunguzi wa kifo cha daktari aliyeuawa wakati wa maandamano yaliochangia kutimuliwa kwa Bashir madarakani mnamo Aprili.

Rais huyo wa zamani bado anakabiliwa na kesi kwa nafasi yake katika mapinduzi ya mwaka 1982 yaliyomuingiza madarakani.

Haijabainika wazi ikiwa atakabiliwa na mashitaka katika Mahakama ya Kimataifa ya jinai (ICC).

Unaweza pia kusoma:

Anatakiwa na mahakama hiyo ya Uholanzi kwa mauaji ya kimbari is katika jimbo la Darfur , ambako watu 300,000 waliuawa.

Baada ya Bashir kung'olewa madarakani mwezi Aprili, mwaendesha mashtaka wa mahakama ya kimataifa ya ICC mjini The Hague waliomba ashtkakiwe kwa mauaji ya Darfur.

Majenerali wa Sudan walionyakua mamlaka mara baada ya kupinduliwa walikataa kutekeleza a gizo la mahakama.

Lakini shirikisho la vuguvugu la waandamanaji - ambalo kwa sasa lina uwakilishi mkubwa katika baraza la taifa linaloongoza nchi- hivi karibuni lilisema kuwa halitapinga kupelekwa kwake katika ICC.

Waendeshamashtaka Sudan pia wameshitaki kwa kuwauwa wapinzani wakati wa maandamano yaliyosababisha kung'olewa kwake mamlakani.