Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Korea Kaskazini yafanya ''jaribio muhimu'', vyasema vyombo vya habari vya taifa hilo
Korea Kaskaizni imefanya "jaribio muhimu " katika kituo chake cha uzinduzi wa safari Setilaiti ili kuinua kiwango chake cha udhiniti wa nyuklia, vimesema vyombo vya habari vya taifa hilo.
Msemaji ameliambia shirika la habari la KNCA kuwa jaribio hilo lilifanyika siku ya Ijumaa kalika uwanja wa kituo cha uzinduzi wa Setilaite cha Sohae, lakini hakutoa maelezo zaidi.
Mazungumzo baina ya Marekani ni Korea Kaskazini juu ya mpango wake wa Nyuklia bado yamekwama.
Rais wa Marekani Donald Trump amekataa kuondoa vikwazo hadi pale Korea Kaskazini itakapoacha mpango wake wa Nyuklia.
Lakini kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un badala yake amekuwa akitaka hakikisjho jipya kutoka kwa Marekani kabla ya mwisho wa mwaka.
Pyongyang imesema kuwa itachukua " njia mpya " kama hilo halitafanyika- ikisema kuwa Marekani itarajie "zawadi ya Krismasi " kama haitaheshimu wito wake.
Lilikua ni jaribio gani?
Haijawa wazi ni kitu gani hasa Korea Kaskazini ilikua inakifanyia majaribio kwenye eneo hilo.
Ankit Panda, mtaalamu wa Korea Kaskazini katika Shirikisho la Wanasayansi wa Marekani, ameiambia BBC, kuwa huenda lilikuwa ni jaribio la ardhini la injini ya makombora ya masafa. Waziri wa ulinzi wa Korea Kusini alisema awali kuwa hilo ndilo lililokuwa lengo la jaribio mapema mwezi Disemba.
Korea Kaskazini imekuwa ikiimarisha majaribio yake ya silaha na kutoa maneno makali dhidi ya Marekani wiki za hivi karibuni.
Japan iliilaumu nchi hiyo kwa "marudio ya ufyatuaji wa makombora " baada ya kufyatuliwa kwa makombora mawili mwezi wa Novemba.
Korea Kaskazini hata hivyo ilisema kuwa ilikuwa inafanyia majaribio "Mtambo wake mkubwa wa kufyatua roketi nyingi ", na ikatishia kuwa Japan huenda ikashuhudia makomborra halisi katika kipindi kijacho ambacho si kirefu.
Ni kwanini Korea Kaskazini inafanya jaribio sasa?
Jaribio hili linakuja huku kukiwa na hali ya taharuki katika kanda hiyo.
Baraza la usalama la Umoja wa mtaifa Jumatano lilikutana kufuatia ombi la Marekani kujadili mpango wa silaha wa Korea Kaskazini -hatua ambayo Korea Kaskazini iliita "uchokozi mkubwa''.
Na Jumapili , mwakilishi maalumu wa Marekani kwa ajili ya Korea Kaskazini Stephen Biegun anapanga kufanya ziara katika mji mkuu wa Korea Kaskazini Seoul.
Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa bado ana matumaini ya kufikia makubaliano na Korea Kaskazini.
Rais Trump alifanya mpango wa kutafuta amani na Korea Kaskazini kuwa agenda kuu ya sera ya kigeni mnamo mwaka 2018, lakini ameshindwa kufikia mapatano muhimu ya kuifanya Korea Kaskazini iachane na mpango wake wa nyuklia , licha ya kufanya mikutano miwili na kiongozi Kim Jong-un na hata kufanya ziara Korea Kaskazini.
Unaweza pia kusoma
Marekani ilifanya majaribio ya makombora ya masafa ya kati ya ballistic juu ya bahari ya Pacific Alhamisi -silaha ambayo ilitakiwa kuwea imezuiwa chini ya mkataba wa vikosi vya nuklia wa mwaka 1987 ambao Trump aliacha kuutekeleza mapema mwaka huu.