Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jeremy Corbyn akabiliwa na upinzani mkali katika chama cha chake
Jeremy Corbyn amesema kwamba hatakiongoza chama cha Leba katika uchaguzi ujao , kufuatia 'usiku mbaya' wa chama chake.
Amesema kuwa atasalia kuwa kiongozi huku akiangazia uchaguzi huo ambao utabiri wa BBC umesema utakuwa pigo kubwa kwa chama hicho miongo kadhaa.
Ameongezea kwamba swala la Brexit limetawala siasa na kuwa zaidi ya mijadala ya kawaida ya kisiasa. Lakini wengi katika chama cha Leba wamelaumu uongozi wake.
Leba kimepoteza baadhi ya ngome zake kaskazini mwa England na Wales katika maeneo ambayo yalipiga kura ya kuunga mkono Brexit 2016 katika kura ya maoni.
Utabiri wa BBC umesema kwamba chama cha Leba kitashinda viti 199 ikiwa ni chini ya viti 63 ikilinganishwa na uchaguzi mkuu wa 2017.
Matokeo rasmi yanatarajiwa kutolewa kufikia mwendo wa saa sita saa za Uingereza siku ya Ijumaa.
Akizungumza baada ya kutetea kiti chake Corbyn alisema kwamba sera za chama hicho zilikuwa zikiungwa mkono pakubwa na kukosoa jinsi vyombo vya habari vilivyokiangazia chama chake wakati wa kampeni.
Lakini aliongezea: Brexit imetawala siasa na kuleta mgawanyiko katika mijadala ya taifa , swala hilo limekuwa zaidi ya mijadala ya kila siku ya taifa hili.
''Ninatambua kwamba tuliingia katika kampenii hizo kwa ahadi ya kuanzisha mjadala mpya kuhusu mpango wa kujiondo wa waziri mkuu Boris Johnson na baadaye kuwasilisha makubaliano hayo ili kupigiwa kura mbali na mbadala wa kusalia katika Muungano wa Ulaya''.
Mchakato huo ulikosolewa na mwenyekiti wa chama hicho Ian Levy aliyesema kwamba amewaongoza wapiga kura katika ngome za chama cha Leba kuamini kwamba Leba ni chama kilichokuwa kikipigia upatu kusalia katika muungano wa EU.
Lakini aliongezea kwamba mkakati huo haukuwa uamuzi wa Jeremy Corbyn , kwa kuwa ulipitishwa na wajumbe katika mkutano wa chama hicho uliofanyika mwezi Septemba.
Chansela Kivuli McDonald , mshirika muhimu wa Corbyn aliambia kitengo cha habari cha PA kwamba mpango wa Brexit wa chama hicho ulikuwa na kanuni na kwamba ulipanga kulileta pamoja taifa hilo, lakini ulishindwa.
Mapema , alisema kwamba hakuweza kufikiria iwapo kiongozi huyo wa Leba alikuwa swala nyeti la kampeni hiyo.
Gareth Snell, ambaye alipoteza kiti cha Central alitoa wito kwa bwana Corbyn na bwana McDonald kujizulu.
Aliwashutumu maafisa waandamizi katika baraza kivuli la mawaziri waliokuwa wakiunga mkono kura ya kusalia EU kwa kuwatumia vibaya wagombea katika maeneo ya mabunge yenye watu wachache katika eneo la Midland na kaskazini mwa England.
Mbunge mwengine wa chama cha Leba aliyepoteza kiti chake ni Caroline Flint katika eneo la Don Valley , ambaye alisema kwamba wafuasi wake wengi hawakutaka kumpigia kura Corbyn ili kuwa waziri mkuu.
Aliongezea: Ninaogopa kusema kwamba kuna wabunge wa msimamo wa wastani ambao wametusukuma kufika mwisho kuhusiana na Brexit na wamekuwa wakiunga mkono kura ya kusalia kwa Uingereza katika Eu bila kujali tabaka la watu wanaofanya kazi katika eneo la Heartland na nimekasirika sana kuhusu hatua hiyo.
Waziri kivuli wa maswala ya kigeni anayeunga mkono Braxit Sir Keir Starmer, akizungumza baada ya kutetea kiti chake cha Holborn na St Pancras akisema kwamba upande wote unafaa kutafakari na kuelewa lakini pia tunajukumu la kujenga upaya kuanzia sasa.
Yvette Cooper , ambaye alishindwa kumng'oa Corbyn katika uongozi wa chama hicho 2015 alisema kwamba matokeo hayo yanaonyesha kwamba chama cha Leba lazima kifanye mabadiliko.
Alisema kwamba Brexit ilikuwa na jukumu kubwa katika matokeo ya chama chake lakini kwamba uchaguzi huo haukuwa kuhusu Brexit,
''Ilikuwa jinsi wanavyokichukulia chama hiki na vile wanavyoungazia uongozi wa chama hiki'', aliongezea.
Akizungumza baada ya matokeo yasio rasmi kutabiri kwamba Leba itapoteza pakubwa , aliyekuwa waziri wa maswala ya ndani nchini Uingereza Alan Johnson aliambia chombo cha habari cha ITV kwamba bwana Corbyn amekuwa hana uwezo wa kuongoza chama hicho cha kisiasa.