Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Una tatizo la kuchelewesha ua kuahirisha mambo?
Sote tuna tabia ya kuchelewa au kuahirisha kufanya mambo, lakini tatizo linakuja pale tunapokubali hali hiyo kuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku.
Tuamua kuahirisha jambo licha ya kujua madhara yake basi bila shaka hapo kuna tatizo.
Mwenendo wa kuchelewecha mambo kupindukia ni hatari kwa afya, kwa sababu inamletea mhusika msongo wa mawazo, unaoweza kumfanya aachane kwa mfano na mazoezi ya viungo au kula vyakula murua kwa afya.
Wakati mwingine muathiriwa huenda akachelewa kumuona daktari ili apate uchunguzi wa kimatibabu anapojikuta na dalili ya ugonjwa.
Je utafiti wa kisaikolojia umekuja kutusaidia kuepukana na suala la kuchelewesha mambo tunayotaka kufanya kwa kuahirisha mara kwa mara bila kuwa na sababu za kimsingi?
Haya hapa baadhi ya mambo yanayoweza kusaidia kuondokana na tabia ya kuchelewesha au kuahirisha.
1. Usitegemee azma pekee kupata motisha
Ian Taylor, mwanasaikolojia wa anaesomea masuala ya motisha katika Chuo Kikuu cha Loughborough, amegundua kuwa watu mara nyingi wanafikiria azma ya kufanya jambo pekee inatosha kuwapatia motisha wa kufanya kazi lakini anasema dhana hiyo haifai.
"Azma ni njia moja ya motisha, lakini sio mfano mzuri wa kufikia malenzo yako,"anasema.
Badala yake kigezo cha azma kinamfanya mtu kupuuza sehemu muhimu ya kazi, intakayomwezesha kufikia malengo yake.
2. Angazia manufaa ya kazi unayoahirisha kila wakati
Sababu halisi inayokufanya kuahirisha kitu unachotaka kufanya ni hofu ya kufeli?
Fuschia Sirois, kutoka Chuo Kikuu cha Sheffield amekuwa akifanya utafiti kuhusu tabia ya kuchelewesha jambo au kuwa na mwenendo wa kuahirisha mambo kwa miaka 15, na amebaini kuwa tatizo ni muda wote sio uvivu au ukosefu wa kuzingatia muda- inahusisha tatizo la kudhibiti hisia.
Ikiwa unahofu huenda usifaulu, utajipata ukitafutia vijisababu vya kuahirisha mpango mzima ili usijipate ukiwa na dhiki ya kutotekeleza jambo hilo.
Lakini hali hiyo humfanya mtu kurejelea tabia hiyo miaka nenda rudi: Kwa sababu kuchelewesha huko utakosa muda wa kutosha wa kufanya jambo hilo hali ambayo inakuweka katika hatari ya kufeli na kukufanya ujihisi vibaya na huenda usifanye kabisa.
Ili kukabilia na hisia hizi jaribu kuangazia umuhimu wa kazi unayotaka kufanya: huenda ukajifunza kitu au na kufurahia kazi yenyewe kuliko ulivyotarajia.
3. Jiandae mapema
Ikiwa unajua kitu fulani kinakufanya uwe na tabia ya kuchelewa kufanya jambo, jiandae mapema kwa kutumia mfumo unaojulikana kama "kama halita" - kuashiria umuhimu wa kile unachotaka kufanya.
Kwa vyovyote utalifanya kwasababu huna budi ..
Huenda rafiki kwa mfano akapendekeza mkutano mwisho wa juma wakati ambapo ulikua umepanga kudurusu ...badala ya kukataa pendekezo hilo unaweza kupendekeza muda mwingine kama jioni hivi badala ya kuvuruga mipango yako.
Mwanasaikolojia wa Marekani Peter Gollwitzer alipofanyia uchunguzi wa watu 94 kwa kutumia mbinu hii, alibaini kuwa walikuwa na uwezo mara mbili au tatu zaidi ya kufikia malengo yao ikilinganishwa na watu wasio na mpanho huo.
4. Punguza bidii inayohusika
Lifanye jambo lako kuwa rahisi zaidi kulianza.
Je! Umewahi kusikia juu ya usanifu wa kuchagua? Katika maeneo ya kula inasadikiwa kuwa ukiweka matunda mahali zinapoonekana badala ya chokoleti huwavfanya wateja kula vyakula vilivyo na afya.
Tunaweza kujiamulia mambo kama hayo maishani: valia nguo ya mazoezi ukiwa na mpango wa kufanya mazoezi mapema asubuhi; au weka nguo zako za mazoezi juu ya meza mahali unapoweza kuziona kwa urahisi kabla hujalala, ukiamka kitu cha kwanza utakachoona ni nguo zitakazo kukumbusha kile kinachokusubiri kabla ya kuanza siku.
Pia kumbuka kuweka pembeni vitu vitakavyokushawishi usifanye jamvo ulilopanga kufanya -Zima arifa kwenye skrini yako ya simu na ikiwezekana jiepushe na mitandao ya kijamii.
5. Jizawadie
Hali ya kuahirisha mambo inavutia kwasababu kunamfanya mhusika kujihisi kana kwamba amejizawadia hapo kwa hapo kufanya kazi ambayo inaonekana kuwa ngumu.
Kutokana na hilo wataalamu wanapendekeza haja ya kukabiliana na hali hiyo kwa kutumia njia mbadala.
Utafiti uliofanywa na Catherine Milkman, kutoka Chuo Kikuu cha Pennsylvania, umegundua kuwa watu wakipewa nafasi ya kusikiliza hadithi ya kusisimua wakiwa kwenye ukumbi wa mazoezi pekee uwezekano wao kurudi kusikiliza kilichofanyika upo juu zaidi - Hadithi hiyo ni sehemu ya zawadi ya papo kwa papo.
Tafuta kitu kitakacho kupatia msukumo wa kufanya kazi.
6. Kuza mtazamo wa kweli juu ya hali yako wa baadaye
Baadhi ya watu wanaamini kuwa watapata muda zaidi siku zijazo.
Hilo kwa kweli huenda lisifanyike na ndio maana tunapuuza muda tutakaochukua kukamilisha kazi tunayotarajia kufanya.
Mfano mzuri wa kukosa mpangilio wa mambo unapatikana katika toleo la kwanza la kamusi ya Kiingereza ya Oxford: Mwaka 1860 ilitangazwa itachukua miaka miwili kuikamilisha lakini haikukamilishwa hadi mwaka 1928... na kufikia wakati huo ilikuwa imepitwa na wakati hadi ikaanza kufanyiwa marekebisho mojo kwa moja baada ya kukamilishwa.
7. Jihurumie mwenyewe
Huwezi kufikia lengo lolote ikiwa muda wako mwingi utaumalizia katika mitandao ya kijamii badala ya kufanya kazi.
Ukweli ni kwamba, watu hujihisi vibaya kuhusu kazi walionayo haswa ikiwa utekelezaji wake unawapa changamoto- bila shaka kuongeza hisia inayowapa usumbufu wa mawazo ni jambo ambalo hawangelitaka kuliwazia.
Katika utafiti uliofanywa dhidi ya wanafunzi wanaosomea mtihani, wale walijihurumia kwa kuahirisha wakati wa kudurusu walikuwa katika nafasi nzuri ya kujirekebisha siku zijazo ikilinganishwa na wale waliojilaumu kwa kundekeza tabia hiyo.
Kama anavyosema Sirois, tunahitaji kujihurumia sawa na vile ambavyo hatuwezi kuwagombeza marafiki wetu kwa ukali ndivyo, "tunavyohitaji kujijali na kujisame kwa kiwango fulani" kwani kosa ni kurudia kosa.
8. Jiangazie kwa njia nzuri unapozungumza kujihusu
Hata jambo dogo kama lugha unayotumia inaweza na umuhimu mkubwa.
Muda mfupi kabla ya ushaguzi wa Urais wa Marekani mwaka 2008, kuna utafiti uliofanywa California: watuwaliojisajili kupiga kura waliombwa kushiriki utafiti huo kwa kujibu swali kuhusu vile wanavyojihisi ''wanapopiga kura" au jinsi walivyohisi kuwa "wapiga kura".
Tofauti ya lugha huenda ikiwa kidogo, lakini siku ya uchaguzi ilipofika, 95% ya watu walioulizwa kuhusu vile wanavyojihisi"wapiga kura" walishiriki uchaguzi, ikilinganishwa na 82% ya watu waliokuwa katika kundi la "kupiga kura" - hii inamaanisha jinsi tunavyojichukulia huathiri tabia yetu.