Watuhumiwa wa kesi ya Escrow kuongezewa mashtaka nchini Tanzania

Mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Singh Sethi na mfanyabiashara James Rugemarila

Chanzo cha picha, Google

Maelezo ya picha, Mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Singh Sethi na mfanyabiashara James Rugemarila
Iliyochapishwa

Mmiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Singh Sethi na mfanyabiashara James Rugemarila wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na mashtaka 12, badala ya mashtaka sita waliyosomewa awali.

Miongoni mwa mashtaka hayo 12 ya uhujumu uchumi yamo mashtaka matano ya kutakatisha fedha na kuisababisha hasara ya USD 22, 198,544.60 na Sh 309,461,300,158.27(USD 138,275.82).

Mashtaka hayo yanayowakabili ni pamoja na kula njama, kujihusisha mtandao wa uhalifu , kughushi nyaraka, kutoa nyaraka za kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kuisababishia Serikali hasara na kutakatisha fedha.

Miongoni mwa mashtaka hayo ni kudaiwa, kati ya oktoba 18 ,2011 na Machi 19 , 2014 jijini Dar es Salaam ,Rugemarila na Sethi walikula njama katika nchi za Afrika Kusini, Kenya na India ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Washtakiwa wote, wanadaiwa kuwa kati ya Novemba 28/29, 2011 na Januari 23,2014 makao makuu Benki ya Stanbic kinondoni na Benki ya Mkombozi tawi la St .Joseph kwa ulaghai washtakiwa hao walijipatia kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT), walijipatia USD 22,198,544.60 na Tsh 309, 461,300,158.27.

Baaada ya kusomewa mashtaka hayo, wakili Shedrack Kimaro alidai upelelezi bado haujakamilika na washtakiwa wamepelekwa rumande hadi Julai14,217.