Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
'Jehanamu' ya Qatar unayoweza kulala kwa $200 pekee
"Bado inajengwa. Mchana ni kama kuzimu. Ni jangwa. Kuna joto sana."
Ni Shogo Nakashima, akiwaza ni wapi ataishi kwa muda wa wiki mbili zijazo, huku akiwa na tabasamu usoni. Alisema "Nacheka ili nisilie".
“Siwezi kubadili nilipo sasa, kwa hiyo natakiwa kukubali na kusubiri mechi ya Japan,” alisema.
"Nitalala tu hapa mpaka basi. Kisha nitatoka niende kutembea mjini . Sitaki kukaa hapa tena."
Mwanaume huyo wa Kijapani mwenye umri wa miaka 31 alikuwa mmoja wa watu wa kwanza kufika katika Kijiji cha Sanaa cha Kisiwa cha Qetaifan, kaskazini mwa Jiji la Dosha, ambapo ujenzi ulikuwa bado unaendelea katika baadhi ya maeneo saa chache baada ya eneo hilo kufunguliwa .
Lakini wakati wageni wengi hawakufika mahali hapo, kulikuwa na dalili kwamba mambo hayakuwa kama ilivyotarajiwa.
Ukitazama kambi hiyo, utaona magari ya ujenzi na wafanyakazi wakiwa na kazi nyingi kama vile kujenga barabara na kufunga nyaya za umeme.
Na unapoenda kwenye eneo la mapokezi, kuna mahema 1,800, ambayo kila moja linaweza kulala watu wawili.
Pedro na Fatima wanaishi Uhispania lakini wako hapa kuishabikia Mexico. Walifunga ndoa mwezi Aprili na safari hii ni sehemu ya fungate yao.
Inagharimu dola 200 kwa usiku mmoja kulala. Kusema kweli, haikuwa kile nilichotarajia hapa. "Unapoona picha na kusoma maelezo ya uwanja wa Kombe la Dunia - unatarajia kumbi zenye ubora," alisema Pedro.
"Hii ni kama hoteli ya hali ya chini ambayo unaweza kuipata katika maeneo mengi."
"Ilikuwa kama tulikuwa kwenye chumba cha kuhifadhia mazingira," aliongeza, "kwa hivyo hatukuweza kulala baada ya saa 9 asubuhi, ingawa tulikuwa tumechoka kutokana na safari ya ndege."
Kila hema lina vitanda viwili