Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwanini moto wa 'lango la Jehanamu' nchini Turkmenistan umekuwa ukiwaka kwa miongo kadhaa sasa?
Shimo hili linajulikana kama Crater of Darvaza ,lililopo kaskazini mwa lliliokuwa taifa la Muungano wa Usovieti la Turkmenistan.
''Wakati nilipoliona shimo hilo kwa mara ya kwanza na kulikaribia huku upepo wenye joto kali uliokuwa ukitoka ndani yake ukinipiga usoni , nilihisi kwamba hili ni eneo ambalo shetani anaweza kujitokeza ndani yake'' , alisema mtafiti wa Canada George Kourounis akizungumza na BBC.
Likiwa na upana wa mita 69 na kina cha mita 30 , shimo hilo limekuwa likitoa gesi asilia ambayo imekuwa ikichomeka kwa miongo kadhaa sasa.
Mwaka 2013 aliwasili katika eneo hilo na kituo cha National Geographic channel , ambapo alijaribu kubaini jinsi moto huu wa milele ulikotoka.
Lakini alimaliza uchunguzi wake na mashaka badala ya majibu.
Chanzo cha kushangaza
Hadithi ambayo imeenezwa sana ni kwamba mwaka 1971, wanajiolojia wa Muungano wa Usovieti walikuwa wakichimba jangwa la Karakum kwa lengo la kutafuta mafuta.
Ndani yake walipata bagi la gesi asilia ambayo ilifanya ardhi kudidimia na kusababisha mashimo matatu makubwa.
Ili kuzuia gesi hiyo ya Methane kutotoka , nadharia moja inasema kwamba wanajiolojia hao walichoma shimo moja, wakidhani gesi hiyo itachomeka na kumalizika kwa wiki chache.
Lakini Kouranis anasema kwamba hakuna stakhabadhi za kuthibitisha hilo.
Aliwasili katika eneo hilo mwaka 2013 na baada ya uchunguzi aligundua kwamba hakuna anayejua chanzo cha shimo na moto huo mkali.
''Kitu kinachoudhi kabisa kuhusu shimo hili ni kwamba hakuna habari ya kutosha kulihusu {huwezi kupata hata baada ya kutembelea taifa hilo'', alisema mtafiti huyo.
"Nilijaribu uwezo wangu wote kutafuta ripoti rasmi au rekodi au iwapo kuna magazeti yaliozungumzia kuhusu suala hilo , lakini hakuna."
Kulingana na wanajiolojia wa Turkimenistan , shimo hilo kubwa lilijitokeza mwaka 1960 na kuaanza kuwaka moto katika miaka ya themanini.
Pia kuna madai kwamba moto huo ulitokea kwa bahati mbaya, kama vile kupitia umeme ama iwapo uliwashwa makusudi, anasema Kourounis.
Nadharia nyengine inasema kwamba huenda walichoma gesi hiyo kwa makusudi kwa uchumi na usalama .
Iwapo hiyo ndio ilikuwa lengo lao , kwasababu kawi ni kitu muhimu kwa Usovieti, ripoti kama hizo huenda zikawa siri kubwa, wataalamu wanaamini.
Siri ilioko
Mwanahistoria Jeronim Perovic anasema kwamba maajabu ya lango hilo la jehanam ni la kimantiki.
''Ni tafakari ya jinsi mambo yalivyofanyika katika miaka ya Muungano wa uUovieti , ambapo wakati huo ni mafanikio pekee yaliotajwa. Hivyobasi iwapo wakaazi Walifanya makosa fulani , hakuna aliyetaka kujulikana'' , anaelezea BBC.
Na kwasababu muungano wa usovieti hauna tatizo la usambazaji wa gesi , kwasababu unazalisha mamilioni ya mapipa ya gesi kila mwaka , inawezekana kwamba suluhu mwafaka ilikuwa kuchoma shimo hilo kama njia mbadala , wataalam wanasema.
Kuchoma mita 15,000 au 16,000 za ujazo kila mwaka , kitu ambacho ni mara nne ambacho Switzerland inatumia kwa mwaka , kwao sio kitu kikubwa.
''Hivyobasi badala ya kufikiria kuhusu itakavyotumika ama kuweka katika bomba linalotegemea miundo mbinu, waliamua kulichoma shimo hilo', anasema.
Upande mwengine , Stefan Green mtafiti aliyeshiriki katika utafiti uliofanywa na Kourounis anaelezea kwamba gesi ya methane inayotoka bila udhibiti ni wazo baya , hivyobasi inaleta maana kuichoma.
''Ni hatari kwasababu inachomeka , haikai mahali pamoja , la sivyo ingesababisha mlipuko mkubwa'', anasema.