Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mizinga kutoka Ujerumani, Marekani na Uingereza inavyoweza kubadili vita vya Ukraine
Je wiki hii vita viligeuka ghafla na kuwa neema kwa Ukraine? Ni wakati wa maamuzi, huku muungano wa mataifa ya Magharibi ulithibitisha kuwa hatimaye wako tayari kupeleka silaha za kisasa - hususan mizinga.
Ujerumani ilisema kuwa itatuma mizinga ya Leopard 2 na Marekani ilisema itatuma mizinga yake ya M1 Abrams.
Uingereza na Poland kwa pamoja tayari zimetoa ahadi za kuaminika na nchi nyingine zinatarajia kufuata mkono huo. Baadhi ya wachambuzi wameelezea hatua hii kama uwezekano wa "mabadiliko".
Lakini je hii inatosha kweli kuwawezesha kushinda vita?
Ben Barry, msoni katika taarisi ya kimataifa ya stadi za kimkakati (ISS), anaiambia BBCkuwa mizinga ya Magharibi italeta tofauti. Lakini Brigadia wa zamani wa Uingereza pia anaonya kuwa ahadi zilizotolewa hadi sasa zisitimizwe.
Katika vita vya sasa, mizinga imekuwa muhimu kwa operesheni za mashambulizi – kupiga maeneo ya adui na kuchukua eneo.
Ikitumiwa kwa ufanisi, mizinga inaweza kufyatuliwa kutoka eneo lolote lile, inaweza kutoa ulinzi , na kupiga mashambulio ya kishtukiza . Ikiwekwa mahali kwa wingi, inaweza kuharibu ulinzi wa adui. Lakini pia inahitaji usaidizi wa silaha kwanza kwa ajili ya kudhoofisha ulinzi huo na halafu usaidizi wa askari wa kuifikisha kwenye maeneo ya vita.
Historia inaonyesha kuwa mizinga pekee haishindi vita.
Uingereza ilitumia mamia ya mizinga katika makabiliano ya Cambrai mwezi Novemba 1917 – tili kumaliza mkwamo wa vita vilivyodumu kwa muda mrefu. Awali walifanikiwa kusonga mbele , lakini mizinga mingi iliharibika na Uingereza ikapoteza maeneo iliyokuwa imeyanyakua.
Mizinga pia inaweza kutumiwa katika ulinzi. Katika mwaka 1940 ilitumiwa na wanajeshi wa Uingereza na Ufaransa katika Arras kuzuia uvamizi wa Wanazi na kusaidia kuwaondosha mara maoja wanajeshi wa uingereza kutoka Dunkirk.
Lakini Ukraine imekwishatangaza wazi kwamba inataka silaha na sio tu za kukabiliana na shambulio linaloweza kufanywa na Urusi, bali inataka kurejesha tena maeneo yake yaliyonyakuliwa - inataka kwenda kushambulia.
Jinsi Ukraine inavyoweza kutumia mizinga katika mashambulio
Haitakuwa na maana kubwa kwa Ukraine kupeleka mizinga ya ziada kote katika maeneo ya vita yenye urefu wa Km 1,000 (maili 621). Kuvunja ngome za ulinzi za Urusi , Ukraine itahitaji kuweka vikosi vyake vingi – labda katika eneo la kati ya kilomita tano hadi 20 ( kati ya maili tatu na 12).
Hamish de Bretton-Gordon, kanali wa zamani katika jeshi la Uingereza, anasema idadi kubwa ya wanajeshi haimaanishi kuwa mafanikio.
Kwa Brigedi yenye silaha kupata mafanikio makubwa katika operesheni kwa kawaida huhitaji mizinga 70. Kwahiyo zaidi ya mizinga 100 ya mapigano ya Magharibi inaweza kuleta tofauti kubwa , anasema.
Ukraine ingekuwa na silaha na kufanya operesheni iwezavyo ingefanya mashambulizi kwa wakati mmoja katika maeneo tofauti, kama ilivyofanya mwaka jana kaskazini na kusini.
Uingereza haitumi Ukraine tu mizinga ya 14 Challenger , lakini pia inatuma mizinga 30 inayoweza kufyatua silaha yenyewe na vifaru vya kuwapeba na kuwalinda wnajeshi
Marekani pia inaipatia Ukraine zaidi ya silaha 100 za magari ya kijeshi ya Bradley na Stryker, huku Ujerumani ikitoa magari ya mapigano aina ya Marder yanayotumiwa na wanajeshi wa ardhini 40 kati vile vya aina ya Marder - pamoja na mizinga.
Mizinga ni sehemu ya mkuki, uliotengenezwa kwenda haraka kwenye eneo la wazi la ardhi.
Mizinga ya Challenger 2, Leopard 2 na M1 ni ya kasi kuliko mingi ya mizinga iliyotengenezwa na urusi ikiwa na zaidi ya kilomita 25 kwa saa (40km kwa saa) kwenye ardhi isiyo na barabara.
Kuchukua arhi haraka, kwa kushitukiza , watahitaji kuepuka maeneo ya mijini ambako wanaweza kushambuliwa. Urusi ilionyesha mapema katika vita hivi, katika jaribio lake lililofeli la kuuzingira mji wa Kyiv , kwamba msururu mrefu wa silaha barabarani ni rahisi kulengwa.
Bw Barry, wa ISS, anasema shambulio lolote la mizinga litalenga maeneo dhaifu ya adui. Lakini ametahadharisha kuwa Urusi imetumia miezi michache iliyopita kuimarisha maeneo yake ya ulinzi mitaro na vifaru.
Mizinga ya Magharibi pia ina uzito wat ani zipatazo 20 kuliko ile ya wenzao wa Urusi. Silaha za ziada zinawapatia ulinzi bora lakini inamaanisha pia kwamba zitakuwa labda nzito kweza kuvuka baadi ya madaraja ambayo sio thabiti. Urusi na Ukraine kwa p[amoja zimeipua madaraja ili kupunguza kasi ya vita kwa kila upande.
Mashambulio ya kushitukiza usiku
Bw de Bretton Gordon, ambaye aliongoza kikosi cha mizinga ya Challenger cha Uingereza, anasema moja ya faida kubwa ya mizinga iliyotengenezwa Magharibi ni uwezo wake wa kupigana usiku.
Uwezo wake wa kusafiri usiku na kamera zake ni za kiwango cha juu. Ni mizinga ya mmoja tu wa kisasa wa Urusi - kama T-90 – inaweza kupigana usiku.
Mashambulio nyakati za usiku pia huongeza hali ya mshituko na kushtukizwa.