Mizinga kutoka Ujerumani, Marekani na Uingereza inavyoweza kubadili vita vya Ukraine  

G

Chanzo cha picha, EPA

Iliyochapishwa

Je wiki hii vita viligeuka ghafla na kuwa neema kwa Ukraine? Ni wakati wa maamuzi, huku muungano wa mataifa ya Magharibi ulithibitisha kuwa hatimaye wako tayari kupeleka silaha za kisasa  - hususan mizinga.   

 Ujerumani ilisema kuwa itatuma mizinga ya Leopard 2 na Marekani ilisema itatuma mizinga yake ya  M1 Abrams.

Uingereza na Poland kwa pamoja tayari zimetoa ahadi za kuaminika na nchi nyingine zinatarajia kufuata mkono huo. Baadhi ya wachambuzi wameelezea hatua hii kama  uwezekano wa "mabadiliko".

Lakini je hii inatosha kweli kuwawezesha kushinda vita?

Ben Barry, msoni katika taarisi ya kimataifa ya stadi za kimkakati  (ISS), anaiambia BBCkuwa mizinga ya Magharibi italeta tofauti. Lakini Brigadia wa zamani wa Uingereza pia anaonya kuwa ahadi zilizotolewa hadi sasa zisitimizwe.

 Katika vita vya sasa, mizinga imekuwa muhimu kwa operesheni za mashambulizi – kupiga maeneo ya adui na kuchukua eneo.   

 Ikitumiwa kwa ufanisi, mizinga inaweza kufyatuliwa kutoka eneo lolote lile, inaweza kutoa ulinzi , na kupiga mashambulio ya kishtukiza . Ikiwekwa mahali kwa wingi, inaweza kuharibu ulinzi wa adui. Lakini pia inahitaji usaidizi wa silaha kwanza kwa ajili ya kudhoofisha ulinzi huo na halafu usaidizi  wa askari wa kuifikisha kwenye maeneo ya vita.

Historia inaonyesha kuwa mizinga pekee haishindi vita.

Uingereza ilitumia mamia ya mizinga  katika makabiliano ya Cambrai  mwezi  Novemba 1917 – tili kumaliza mkwamo wa vita vilivyodumu kwa muda mrefu. Awali walifanikiwa kusonga mbele , lakini mizinga mingi iliharibika na  Uingereza  ikapoteza maeneo iliyokuwa imeyanyakua. 

Mizinga pia inaweza kutumiwa katika ulinzi. Katika mwaka 1940 ilitumiwa na wanajeshi wa Uingereza na Ufaransa  katika  Arras  kuzuia uvamizi wa  Wanazi na kusaidia kuwaondosha mara maoja wanajeshi wa uingereza kutoka  Dunkirk.

Lakini Ukraine imekwishatangaza wazi kwamba inataka silaha na sio tu za kukabiliana na shambulio linaloweza kufanywa na Urusi, bali inataka kurejesha tena maeneo yake yaliyonyakuliwa - inataka kwenda kushambulia.

Jinsi Ukraine inavyoweza kutumia mizinga katika mashambulio

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Haitakuwa na maana kubwa kwa Ukraine kupeleka mizinga ya ziada kote katika maeneo ya vita yenye urefu wa  Km 1,000 (maili 621). Kuvunja ngome za ulinzi za    Urusi , Ukraine itahitaji kuweka vikosi vyake vingi – labda katika eneo la kati ya kilomita tano hadi 20 ( kati ya maili tatu na 12).

 Hamish de Bretton-Gordon, kanali wa zamani  katika jeshi la Uingereza, anasema idadi  kubwa ya wanajeshi haimaanishi kuwa mafanikio.

 Kwa Brigedi yenye silaha  kupata mafanikio makubwa katika operesheni kwa kawaida huhitaji mizinga 70. Kwahiyo zaidi ya mizinga 100 ya mapigano ya Magharibi inaweza kuleta tofauti kubwa , anasema.

Ukraine ingekuwa na silaha na kufanya operesheni  iwezavyo ingefanya mashambulizi kwa wakati mmoja katika maeneo tofauti, kama ilivyofanya mwaka jana  kaskazini na kusini.

Uingereza haitumi Ukraine tu mizinga ya 14 Challenger , lakini pia inatuma mizinga   30 inayoweza kufyatua silaha yenyewe na vifaru vya kuwapeba na kuwalinda wnajeshi 

 Marekani pia inaipatia Ukraine zaidi ya silaha 100 za  magari ya kijeshi ya Bradley  na Stryker, huku Ujerumani ikitoa magari ya mapigano aina ya Marder yanayotumiwa na wanajeshi wa ardhini 40 kati vile vya aina ya  Marder  - pamoja na mizinga.

Mizinga ni sehemu ya mkuki, uliotengenezwa kwenda haraka kwenye eneo la wazi la ardhi.    

Mizinga ya  Challenger 2, Leopard 2  na  M1 ni ya kasi kuliko mingi ya mizinga iliyotengenezwa na urusi ikiwa na zaidi ya kilomita   25 kwa saa    (40km kwa saa) kwenye ardhi isiyo na barabara.

Kuchukua arhi haraka, kwa kushitukiza , watahitaji kuepuka maeneo ya mijini ambako wanaweza kushambuliwa. Urusi ilionyesha mapema katika vita hivi, katika jaribio lake lililofeli la kuuzingira mji wa Kyiv , kwamba msururu mrefu wa silaha barabarani ni rahisi kulengwa.   

Bw Barry, wa ISS, anasema shambulio lolote la mizinga litalenga maeneo dhaifu ya adui. Lakini ametahadharisha kuwa Urusi imetumia miezi michache iliyopita kuimarisha  maeneo yake ya ulinzi mitaro na vifaru.

 Mizinga ya Magharibi pia ina uzito wat ani zipatazo 20 kuliko ile ya wenzao wa Urusi. Silaha za ziada zinawapatia ulinzi bora lakini inamaanisha pia kwamba zitakuwa labda nzito  kweza kuvuka baadi ya madaraja ambayo sio thabiti. Urusi na Ukraine kwa p[amoja zimeipua madaraja ili kupunguza kasi ya vita kwa kila upande. 

Mashambulio ya kushitukiza usiku 

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ujerumani hutengeneza vifaru vingi vizito zaidi vya kisasa barani Ulaya vinavyofahamika kama Leopard 2s

Bw de Bretton Gordon, ambaye aliongoza kikosi cha mizinga ya Challenger cha Uingereza, anasema moja ya faida kubwa ya mizinga iliyotengenezwa Magharibi ni uwezo wake wa kupigana usiku.

 Uwezo wake wa kusafiri usiku na kamera zake ni za  kiwango cha juu. Ni mizinga ya mmoja tu wa kisasa wa Urusi   - kama  T-90 – inaweza kupigana usiku. 

Mashambulio nyakati za usiku pia huongeza hali ya mshituko na kushtukizwa.