Ujerumani yabadili msimamo na kuamua kupeleka vifaru Ukraine

Mabadiliko makubwa ya kisera yalitangazwa na serikali ya Ujerumani, ambayo imeidhinisha usambazaji wa takriban tanki 50 za kukinga ndege za Gepard Flakpanzer.

Moja kwa moja

  1. Mpaka hapa tumefika mwisho wa matangazo ya moja kwa moja ya ukurasa wa BBC Swahili, Shukrani

  2. Kwanini Wakenya wana wasiwasi kuhusu ghasia za uchaguzi?

    m

    Chanzo cha picha, AFP

    Chaguzi nyingi za Kenya katika kipindi cha miaka 20 iliyopita zimehusisha kiwango fulani cha ghasia na maandamano.

    Hali ilikuwa mbaya zaidi mwaka 2007 ambapo watu wasiopungua 1,000 waliuawa na zaidi ya nusu milioni kuyahama makazi yao.

    Hivyo si jambo la kushangaza kwamba watu wengi nchini Kenya wanatazamia uchaguzi ujao mwezi Agosti kwa hali ya hpfu.

    Mwanahabari wa Kenya John Allan Namu anatuambia kwamba haisaidii kwamba baadhi ya wanasiasa wanatumia lugha chafu kwenye mitandao ya kijamii, kwamba chombo huru cha uchaguzi hakina fedha na hakiaminiwi na Wakenya wengi, na kwamba mchakato wa hivi karibuni wa kuwateua wagombea ulikuwa na utata.

    "Hatuondolei mzimu wa vurugu katika chaguzi zetu... Ingawa haujaanza, kuna vurugu na kutovumiliana kwa sasa ambazo zinaweza kusababisha ghasia wakati wowote," anasema.

    "Sisi ni nchi ambayo imekataa kuchukua hatua nyingi za mabadiliko ambazo zimetolewa kwetu kupitia pointi ngumu katika maisha yetu ya nyuma au kupitia fursa," anaongeza.

    Lakini je kuna matumaini gani kwa uchaguzi wa amani nchini Kenya?

    • Uchaguzi Kenya 2022:Ukabila unavyotumiwa kama kigezo cha kuunda miungano ya kisiasa Kenya
    • Uchaguzi Kenya 2022: Je ni masuala gani muhimu yanayotawala uchaguzi wa 2022 nchini Kenya?
  3. Ujerumani yabadilisha sera zake na kuamua kutuma vifaru Ukraine

    Hans-Hermann Bühling

    Chanzo cha picha, Hans-Hermann Bühling

    Tuliripoti kuwa , mawaziri wa ulinzi kutoka nchi wanachama wa NATO na nchi za Umoja wa Ulaya wamekuwa wakikutana leo katika uwanja wa ndege wa Marekani huko Ramstein na kusini-magharibi mwa Ujerumani, kujadili kutoa msaada zaidi kwa Ukraine.

    Mabadiliko makubwa ya kisera yalitangazwa na serikali ya Ujerumani, ambayo imeidhinisha usambazaji wa takriban tanki 50 za kukinga ndege za Gepard Flakpanzer.

    Silaha hizo zikiwa zimehifadhiwa kwa muongo mmoja uliopita, zitafanyiwa maboresho ya kiufundi kabla ya kusafirishwa hadi Ukraine.

    Kwa muda mrefu Ujerumani imekuwa na sera ya kutosafirisha silaha nzito katika maeneo yenye migogoro, lakini serikali yake imekuwa chini ya shinikizo kubwa la kutoa msaada zaidi kwa Kyiv.

    Akitoa tangazo hilo, waziri wa ulinzi wa nchi hiyo, Christine Lambrecht, alisema Ujerumani "itaangalia uwezekano wa jinsi itakavyoweza kuisaidia zaidi Ukraine katika vita vyake vya kijasiri na muhimu vya kupigania uhuru na amani".

    • Urusi na Ukraine: Usaidizi wa kijeshi ambao nchi za Magharibi zitatuma kwa serikali ya Ukraine (na mabadiliko ya msimamo wa Ujerumani)
  4. Madai ya uhalifu wa kivita yanahitaji uchunguzi - mkuu wa UN

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alipoulizwa kuhusu ripoti za madai ya uhalifu wa kivita na Moscow, Antonio Guterres amesema kuwa ni suala analolipa kipaumbele.

    Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa anasema wanahitaji "uchunguzi huru". Anaendelea kusema anakubali Urusi ina "malalamiko" lakini anaongeza UN iko tayari kusaidia kushughulikia masuala kama hayo.

  5. 'Kiwanda cha mionzi katika Chernobyl si kawaida'-UN

    m

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mkuu wa shirika la atomiki la Umoja wa Mataifa amesema viwango vya mionzi katika kituo cha zamani cha nguvu za nyuklia cha Chernobyl, eneo lililokuwa na mapigano ya wiki kadhaa baada ya uvamizi wa Urusi, "si pa kawaida".

    Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki Rafael Grossi aliwaambia waandishi wa habari kwamba kukaliwa kwa wiki moja na Urusi kwenye eneo hilo ni "hatari sana", kwa mujibu wa AFP.

    Kituo cha nishati ambacho hakijatumika kilikuwa mahali pa maafa mabaya zaidi ya nyuklia katika historia mnamo 1986 na bado kinatumika kudhibiti taka za nyuklia.

  6. Habari za hivi punde, Lavrov akubali hakuna wanajeshi wa Ukraine nchini Urusi

    Mazungumzo ya wazi kutoka kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres , wakati anapoambia ripota kwamba : Kuna kitu kimoja ambacho ni kweli na kwamba hakuna mjadala wowote unaoweza kubadili: Hakuna wanajeshi wa Ukraine nchini Urusi lakini kuna wanajeshi wa Urusi nchini Ukraine .

    Waziri wa masuala ya kigeni nchini Urusi Segei Lavrov akubali.

    ‘’Hilo ni kweli, naweza kuthibitisha hilo’’, anasema

  7. Kim Jong-un aahidi kuimarisha mpango wa silaha za nyuklia

    m

    Chanzo cha picha, Reuters

    Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alitoa hotuba ya kejeli katika gwaride la kijeshi Jumatatu usiku, na kuapa kuongeza silaha za nyuklia nchini humo.

    Gwaride hilo, la kuadhimisha mwaka wa kuanzishwa kwa vikosi vya jeshi, pia lilionesha makombora yaliyopigwa marufuku ya balestiki ya mabara (ICBMs).

    Mnamo Machi, Korea Kaskazini ilijaribu ICBM yake inayojulikana zaidi kwa mara ya kwanza tangu 2017.

    m

    Chanzo cha picha, Reuters

    Ilizua shutuma nyingi kutoka kwa jumuiya ya kimataifa.

    Marekani pia iliiwekea nchi hiyo vikwazo kadhaa baada ya jaribio hilo.

    ICBM, zilizoundwa kwa ajili ya usambazaji wa silaha za nyuklia, huongeza safu ya mgomo wa Korea Kaskazini hadi bara la Marekani.

    Gwaride hilo pia lilikuwa na makombora ya balestiki yaliyorushwa pamoja na makombora ya hypersonic.

    m

    Chanzo cha picha, EPA

    Hata hivyo, Bw Kim hajakatishwa tamaa na shutuma hizo kufikia sasa. "Tutaendelea kuchukua hatua za kuimarisha na kuendeleza uwezo wa nyuklia wa taifa letu kwa kasi kubwa zaidi," alisema, akiongeza kwamba nguvu zao za nyuklia "lazima ziwe tayari" kutekelezwa wakati wowote, kulingana na ripoti ya Shirika rasmi la Habari la Korea. (KCNA

    • Majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini: Picha kutoka angani zatolewa
    • Majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini: Kombora kubwa zaidi lafyatuliwa tangu 2017
  8. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na Lavrov wa Urusi wafanya mkutano na waandishi wa habari

    m

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov mjini Moscow, ambapo wamefanya mkutano kushinikiza kusitishwa kwa vita nchini Ukraine kwa njia ya kidiplomasia.

    Mazungumzo hayo pia yalitarajiwa kulenga msaada wa kibinadamu kwa ajili ya mji wa bandari uliosambaratika wa Mariupol.

    Viongozi hao wawili wana mkutano wa wanahabari .

  9. Wanyarwanda wanavyomkumbuka Hayati Mwai Kibaki kwa kupewa zawadi ya ng'ombe

    m

    Miongoni mwa mambo ambayo wanyarwanda wanasema yatabaki kwenye kumbukumbu zao daima ni wema na upendo wa Mwai Kibaki ni kuhusiana na mchango wake katika kusaidia wananchi .

    Mapema mwaka wa 2004 aliwagawia ngombe 120 wa kisasa ambao wamekuwa wakiendelea pia za zoezi la wakigawia wananchi wenzao wasio nao kwa kuwawezesha kimaisha.

    Ni sehemu ya utamaduni wa wanyarwanda hususan wafugaji kufanya ushairi wa majigambo kama moja ya burudani na huwa kivutio kikubwa kwa ng'ombe na wasikilizaji kwa ujumla.

    BBC imetembelea mmoja wa wafugaji walionufaika na ng'ombe wa kisasa aliogawiwa na marehemu Mwai Kibaki pamoja na wafugaji wenzake 120 mwaka 2004 Novemba.

    Rutagarama Appollo anao ng'ombe zaidi ya 100 wa kisasa, anasema kwa wastani ngombe mmoja hukamuliwa lita 22 kwa siku, hukamua si chini ya lita 200 za maziwa ambazo huuza kwa sehemu kubwa katika vituo maalum ambapo hukusanywa kupimwa na kufanyiwa usafi kabla ua kusombwa na magari maalum ya maziwa na kuuzwa katika vituo mbali mbali nchini.

    m

    ''Wakati huo tulikuwa tukifuga ng'ombe kwa kuzingatia wingi wa ng'ombe wa kienyeji lakini tulipokwenda Kenya tuliona kwamba ng'ombe wa kisasa ni muhimu mno ,kwa maana ya uzalishaji wa maziwa na wengi kati ya wafugaji walibadili mitazamo na kuzingatia ufugaji wa kisasa, mfugaji Gasana Charles amesema .''

    Charles anasema maisha ya leo nchini yameboreka kwa mchango mkubwa wa programu ya serikali ya kupambana na umaskini maarufu kamagira inka munyarwanda yenye wito wa ng'ombe mmoja kwa kila familia.

    Wananchi nilioongea nao wanaaelezea majonzi na simanzi kwa msiba mkubwa wa marehemu rais Kibaki.

    • Mwai Kibaki: Fahamu mambo matano usiyoyajua kuhusu Mwai Kibaki
    • Mwai Kibaki: Rais aliyebadili uchumi wa Kenya kwa kiwango kikubwa
  10. Nato inahusika vipi katika vita?

    m

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Tumekuwa tukiripoti kuwa kutakuwa na mkutano kati ya mawaziri wa ulinzi wa Nato na nchi za Umoja wa Ulaya kujadili msaada zaidi wa kijeshi kwa Ukraine - lakini Nato ni nini?

    Shirika la Mkataba wa Atlantiki ya Kaskazini ni muungano wa kijeshi ulioanzishwa baada ya Vita vya Pili vya Dunia mwaka 1949 na nchi 12 zikiwemo Uingereza na Marekani.

    Wanachama wake 30 wa sasa wanakubali kusaidiana katika tukio la shambulio la silaha dhidi ya nchi yoyote mwanachama.

    Ukraine si mwanachama wa Nato - kwa hivyo muungano huo haulazimiki kuja katika ulinzi wa nchi hiyo.

    Lakini nchi za Nato hata hivyo zimekuwa zikiiunga mkono Ukraine - ambayo inapakana na wanachama kadhaa, ikiwa ni pamoja na Poland na Romania - kwa msaada wa kifedha wa kijeshi na vifaa.

    Nato imekataa wito wa Ukraine wa kuweka eneo lisilo na ndege nchini humo na kutuma wanajeshi huko, ikisema haitaki vita hivyo kuenea na kuwa mzozo mkubwa zaidi unaovuka mipaka ya Ukraine.

    Urusi imekuwa ikisema mara kwa mara kwamba Ukraine haipaswi kamwe kuruhusiwa kujiunga na Nato, kwa sababu hii italeta muungano huo katika uwanja wake wa nyuma.

    • Ukraine: Njia tatu ambazo zingechochea ongezeko la vita na Nato kuingilia kati
  11. Urusi: tumeua wanajeshi 500 wa Ukraine ndani ya usiku mmoja

    w

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Urusi inadai kuwaua takriban wanajeshi 500 wa Ukraine usiku wa jana.

    Wizara ya ulinzi ya Urusi inadai kuwa iliwaua wanajeshi 500 wa Ukraine usiku kucha baada ya jeshi lake la anga kushambulia maeneo 87 ya kijeshi nchini Ukraine.

    Maghala mawili ya silaha katika eneo la Kharkiv yanasemekana kuwa miongoni mwa shabaha zilizopigwa.

    Wizara hiyo pia ilichapisha video kwenye tovuti yao inayoripotiwa kuonyesha kambi ya kuhifadhi na kukarabati wanajeshi wa Ukraine ambayo wanadai kuwa wameichukua.

    Mizinga ya kijeshi na magari mengine yanaweza kuonekana kwenye video hiyo.

    Inasemekana kuwa na risasi, silaha, nyaraka na vifaa vingine vya jeshi la Ukraine.

    BBC haijaweza kuthibitisha madai haya.

    Unaweza pia kusoma

  12. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anatarajiwa kukutana na Rais wa Urusi Putin leo

    w

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anatazamiwa kukutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin mjini Moscow baadaye leo lakini matarajio kutoka kwa mkutano huo yanasemekana kuwa madogo baada ya juhudi kadhaa za kidiplomasia kushindwa kufikia sasa.

    Mazungumzo kati ya Putin na Guterres yanatarajiwa kuangazia mji uliozingirwa wa Mariupol ambapo licha ya kutangaza ushindi, vikosi vya Urusi vimeshindwa kuchukua vyuma vya Azovstal.

    Vikosi vya Ukraine vilisema mapema Jumanne kwamba Urusi iliendelea kuzuia vitengo vyake kwenye kiwanda hicho.Ukraine imemtaka Guterres kudhamini ukanda wa misaada ya kibinadamu ili kuwaondoa raia wanaohifadhiwa ndani ya Azovstal.

    Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa pia anatarajiwa kusafiri kuelekea Kyiv siku ya Alhamisi ambapo atakutana na Rais Volodomyr Zelensky.

    Marekani pia inatarajiwa kuanza mazungumzo ya ulinzi kuhusiana na Ukraine na mataifa kadhaa leo, huku waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin akiwa mwenyeji nchini Ujerumani.

    Mazungumzo haya yanakuja wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Moscow Sergei Lavrov ameonya hatari ya Vita vya Tatu vya Dunia "ni kubwa" na kukosoa mbinu ya Kyiv ya mazungumzo ya amani ya kuyumba.

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba, hata hivyo, alijibu kwamba Lavrov alikuwa akijaribu "kuitisha dunia" kutokana na kuunga mkono nchi hiyo.

    Unaweza pia kusoma

  13. Chaneli ya YouTube ya Diamond Platnumz yarudi baada ya kudukuliwa

    Akaunti ya YouTube ya mmoja wa wasanii maarufu barani Afrika imerejea baada ya kuripotiwa kuchukuliwa na wadukuzi jambo ambalo lilisababisha kusimamishwa kwake.

    Chaneli ya Diamond Platnumz, ambayo ina watumiaji zaidi ya milioni 6.5 na yenye kutazamwa na watu zaidi ya bilioni moja, ilisemekana kuwa ilidukuliwa siku ya Jumapili.

    Afisa wa kampuni ya rekodi ya Diamond Platnumz, Wasafi, alisema kuwa walipokea barua pepe kutoka YouTube ikiwajulisha kuwa akaunti hiyo imesimamishwa.

    Majid Ramadhani alisema ilisitishwa baada ya wadukuzi hao kuweka wazi maudhui ambayo yalikiuka miongozo ya jukwaa la kidigitali.

    Aliiambia tovuti ya Daily Nation ya Kenya kwamba walipata hasara kubwa na wanajitahidi kusuluhisha suala hilo.Siku ya Jumatatu, nyota huyo wa muziki aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akionyesha kuwa ukurasa huo umerejea.

    "Asante wapenzi wangu....chaneli yangu ya Youtube imerejea," alisema.

    Chaneli hiyo ina wafuasi zaidi ya milioni 6 na kumfanya Diamond kuwa kati ya wasanii wenye wafuasi wengi zaidi kwenye mtandao wa Youtube barani Afrika.

    Ruka Instagram ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa Instagram ujumbe

  14. Hospitali yashambuliwa Darfur

    w

    Shirika la misaada ya matibabu la madaktari wasio na mipaka (MSF), linasema kuwa watu watatu wameuawa ndani ya hospitali katika eneo la Kreneik huko Darfur nchini Sudan.

    Duka la dawa la hospitali hiyo pia liliporwa, ilisema taarifa ya shirika hilo.Waathiriwa ni pamoja na wafanyikazi wawili wa matibabu. Timu za MSF hazikuwepo kwenye kituo hicho wakati wa shambulio hilo, shirika la misaada liliongeza.

    MSF inasema uvamizi wa pili ulifanyika katika Hospitali ya Mafunzo ya El Geneina, katika mji mkuu wa Darfur Magharibi, huku ufyatuaji risasi ukifanyika ndani ya kituo hicho, ikiwa ni pamoja na chumba cha dharura.

    Mfanyikazi mmoja wa hospitali aliuawa, na wafanyikazi wa afya, wakiwemo wale wa MSF, walihamishwa.“Tumeshtushwa na mashambulizi haya na kutuma rambirambi zetu za dhati kwa familia za waliouawa.

    Tunalaani uvamizi huu mbaya kwa maneno makali iwezekanavyo," ilisema taarifa hiyo.Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusu mapigano katika siku za hivi karibuni kati ya jamii hasimu ambayo yaliripotiwa kusababisha vifo vya zaidi ya watu 160.

    • Mzozo wa Sudan: Waandamanaji walioapa kupigania uhuru wao Sudan
    • Polisi wa siri wa Sudan wanaogopwa wamerejea tena
  15. Kim Jong-un aahidi kuimarisha mpango wa silaha za nyuklia

    h

    Chanzo cha picha, KCNA VIA REUTERS

    Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alitoa hotuba ya kibabe katika gwaride la kijeshi Jumatatu usiku, na kuapa kuongeza silaha za nyuklia nchini humo.

    Gwaride hilo, la kuadhimisha mwaka wa kuanzishwa kwa majeshi ya Korea Kaskazini, pia lilishuhudia makombora kadhaa yaliyopigwa marufuku ya masafa ya mbali (ICBMs) yakionyeshwa.

    Mnamo Machi, Korea Kaskazini ilijaribu ICBM kwa mara ya kwanza tangu 2017.Hii ilizua shutuma nyingi kutoka kwa jumuiya ya kimataifa.

    Marekani pia iliiwekea nchi hiyo vikwazo kadhaa baada ya jaribio hilo - ICBM, iliyoundwa kwa ajili ya usambazaji wa silaha za nyuklia, iliongeza muda wa mashambulizi ya Korea Kaskazini hadi bara la Amerika.

    Hata hivyo, Bw Kim hajakatishwa tamaa na shutuma hizo kufikia sasa."Tutaendelea kuchukua hatua za kuimarisha na kuendeleza uwezo wa nyuklia wa taifa letu kwa kasi ya juu," alisema, kwa mujibu wa ripoti ya Shirika rasmi la Habari la Korea.

    • Majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini: Kombora kubwa zaidi lafyatuliwa tangu 2017
    • Je ni nini haswa kinachomshinikiza rais Kim Jong Un wa Korea Kaskazini kufyatua makombora?
    • Kwanini ulimwengu unavutiwa na taarifa za Korea Kaskazini?
  16. Marekani yakana taarifa kuwa ilisita kumuwekea vikwazo mwanamke anayeaminika kuwa mpenzi wa Putin

    Alina Kabaeva ni mshindi wa medali ya dhahabu ya Olimpiki mwenye umri wa miaka 38

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Msemaji wa Ikulu ya White House Jen Psaki amekanusha katika taarifa ya kila siku ya Jumatatu kwa waandishi wa habari kwamba Marekani ilisita makusudi kumuwekea vikwazo mwanamke anayeaminika kuwa mpenzi wa Putin.

    "Tunaendelea kupitia vikwazo," Psaki alisema alipoulizwa ni kwa nini mwanasiasa wa Urusi na mchezaji wa zamani wa mazoezi ya viungo Alina Kabaeva alikuwa bado hajalengwa na vikwazo.

    "Hakuna aliye salama kutokana na vikwazo vyetu," Psaki aliendelea. "Tayari tumemuidhinisha Rais Putin, lakini pia binti yake na wasaidizi wake wa karibu, na tutaendelea kukagua zaidi," aliongeza.

    Kumekuwa na wito kwa Marekani kumuwekea vikwazo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 ambaye ni mshindi wa medali ya dhahabu ya Olimpiki, kama Marekani ilivyowafanyia mabinti wawili wa Putin.

    Putin anajulikana kwa kuwa msiri sana kuhusu maisha yake ya binafsi, na hajawahi kukiri uhusiano wowote wa kimapenzi, kama alivyotajwa kwenye vyombo vya habari vya Urusi na nje.

    Kwa mujibu wa ripoti ya Wall Street Journal, maafisa wa Marekani wamezuia vikwazo kwa Kabaeva kutokana na wasiwasi kwamba Putin ataliona kama shambulio binafsi.

    Inaweza kuonekana kama "pigo la binafsi kwa Bw Putin kwamba inaweza kuongeza mvutano kati ya Urusi na Marekani," Jarida hilo liliandika.

  17. Urusi yachukua jengo la utawala katika jiji la Kherson

    w

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Wakazi wa Kherson wamekua wakiandama kupinga uvamizi wa Urusi

    Meya wa Kherson, jiji kuu pekee ambalo majeshi ya Kirusi yamechukua na kuendelea kukalia, Ihor Kolykhayev, ameripoti kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba watu wenye silaha wa Urusi walichukua udhibiti wa jengo la baraza la jiji siku ya Jumatatu.

    Ingawa Kherson imekuwa chini ya uvamizi wa Urusi tangu mapema Machi, baraza la jiji lilikuwa bado likifanya kazi chini ya udhibiti wa Ukraine.

    Kolykhayev alisema jeshi la Urusi lilichukua funguo za jengo hilo na kubadilishana walinzi na ulinzi wa eneo hilo.Alisema aliondoka kwenye jengo hilo saa 19.45 kwa saa za huko.

    Pravda, chombo cha habari cha Kiukreni, kiliripoti kuwa kuanzia tarehe 26 Aprili, baraza la jiji la Kherson halitafanya kazi.Iliongeza kuwa meya na wafanyakazi wa baraza la jiji walipewa nafasi ya kwenda nyumbani.

    Unaweza pia kusoma

  18. Lavrov: Tishio la vita vya nyuklia ni kweli sio utani

    w

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov amekiri kuwa kuna uwezekano wa mzozo huo kuongezeka hadi kufikia silaha za nyuklia, ingawa pia alitoa maoni ya matumaini kuhusu matarajio ya makubaliano ya amani.

    Akizungumza na Idhaa ya Kwanza ya Urusi siku ya Jumatatu, alisema Moscow ilitaka kuepuka hatari zilizo juu za mzozo kama huo.

    "Huu ndio msimamo wetu muhimu ambao tunaegemeza kila kitu. Hatari sasa ni kubwa," Lavrov alisema.

    "Nisingependa kueleza hatari hizo kwa njia ya uwongo. Wengi wangependa hilo. Hatari ni kubwa, halisi, na hatupaswi kuidharau."

    Lavrov pia alimshutumu Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine kwa "kujifanya" kufanya mazungumzo, akimwita "muigizaji mzuri".

    "Ukitazama kwa makini na kusoma kwa makini anachosema, utapata utata mara elfu moja," mwanadiplomasia mkuu wa Urusi alisema.

    Waziri huyo alisema wiki iliyopita kuwa Moscow imejitolea kuepusha vita vya nyuklia.

    Siku ya Jumatatu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba maoni ya hivi punde zaidi ya Lavrov yalikuwa ni ishara kwamba Urusi imepoteza "matumaini yake ya mwisho ya kutisha ulimwengu dhidi ya kuunga mkono Ukraine".

    "Hivyo mazungumzo ya hatari 'halisi' ya WWIII. Hii inamaanisha tu kwamba Moscow inahisi kushindwa nchini Ukraine," alisema.

    Siku chache baada ya uvamizi huo kuanza tena tarehe 24 Februari, Rais wa Urusi Vladimir Putin aliamuru vikosi vyake vya nyuklia kuwa tayari.

    Marekani na washirika wake wa Nato wamesema hawataki uingiliaji wa kijeshi wa moja kwa moja nchini Ukraine, ili kuepusha hatari ya Vita vya Tatu vya Dunia.

    Unaweza pia kusoma