Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Neymar: Je nyota huyu wa Brazil anaondoka PSG na deni la kuacha alama?
Ni hatua iliyoleta mshtuko katika ulimwengu wa soka.
Miaka sita iliyopita gwiji wa Brazil Neymar aliondoka Barcelona na kujiunga na Paris St-Germain kwa mkataba uliovunja rekodi wa £200m.
Sasa akiwa na umri wa miaka 31, mshambuliaji huyo anahama tena, safari hii akiliacha soka la Ulaya - angalau kwa sasa - na kuungana na wachezaji kadhaa wa hadhi ya juu kuamua kucheza Saudi Arabia.
Inasemekana atalipwa euro 150m (£129m) kwa mwaka na Al-Hilal - mara sita ya pesa alizopata PSG - baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili.
Neymar alicheza mechi 173 akiwa na PSG, na kuisaidia kushinda mataji 13, yakiwemo mataji matano ya Ligue 1.
Lakini ilikuwa ni kushinda kombe la juu zaidi Ulaya- Ligi ya Mabingwa - ambalo ndio sababu ya Neymar kusajiliwa, kitu ambacho hakuweza kuwasaidia wababe hao wa Ufaransa kufikia, akikaribia kutwaa mwaka 2020, timu hiyo ilipotinga fainali.
"Haijafanikiwa machoni pa watu wengi. Na anaachana na soka la kiwango cha juu Ulaya," mtaalam wa soka wa Amerika Kusini Tim Vickery aliambia BBC World Service.
"Neymar mwenyewe hataliona hilo- nasio lazima kushinda akiwa Paris St-Germain, lakini akiwa na nia ya kurejea Ulaya katika muda wa miaka miwili - kwa sababu kwa wakati huu ni ngumu kuona ni chaguo gani lingine analoweza kuwa nalo zaidi ya hilo (Saudi)."
Neymar amekuwa na sura mbili ya kupanda na kushuka. BBC inakuletea ya milima na mabonde ya safari ya Neymar kutoka Santos hadi Saudi Arabia.
2009 - Kuichezea Santos kwa mara ya kwanza
Neymar alianza safari yake ya soka katika nchi yake ya asili ya Brazil, akitia saini mkataba wake wa kwanza klabu ya Santos akiwa na umri wa miaka 17.
Alianza kwa mara ya kwanza kucheza timu ya wakubwa katika umri huo huo, akitokea kama mchezaji wa akiba kipindi cha pili katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Oeste mnamo 7 Machi 2009.
Wiki moja baadaye alifunga bao lake la kwanza akiwa na Santos dhidi ya Mogi Mirim na kumaliza msimu akiwa na mabao 14 katika michezo 48.
2010 – Kichezea timu ya taifa ya Brazil kwa mara ya kwanza
Mwaka mmoja tu baada ya kucheza mechi yake ya kwanza , Santos, Neymar aliitwa na Brazil.
Mchezo wake wa kwanza ulikuwa wa kirafiki dhidi ya Marekani tarehe 10 Agosti. 2010. Na ilimchukua dakika 28 pekee kufurahia mchezo wake wa kwanza kwa kufunga bao, akiunganisha kwa kichwa krosi ya Andre Santos iliyompita Tim Howard.
Neymar amefunga mabao 77 katika mechi 124 alizochezea Brazil, lakini bao lake lake la kwanza linabaki kuwa moja ya vivutio kwa soka lake.
2013 – Mafanikio Barcelona na Brazil
Akiwa ameisaidia Santos kushinda Copa Libertadores mwaka 2011 - mara yao ya kwanza tangu mwaka 1963 - Neymar alijiunga na Barcelona baada ya kuhusishwa na msururu wa vilabu vikuu vya Ulaya.
Akicheza pamoja na Lionel Messi na Luis Suarez katika safu ya ushambuliaji iliyojulikana kama 'MSN', Neymar aliwasaidia wababe hao wa Hispania kushinda La Liga, Copa del Rey na Ligi ya Mabingwa katika msimu wake wa pili tu.
Muda mfupi baada ya kujiunga na Barcelona, pia aliisaidia Brazil kushinda Kombe la Shirikisho la Fifa na kutajwa kuwa mchezaji bora wa michuano hiyo.
2013 – Mafanikio Barcelona na Brazil
Akiwa ameisaidia Santos kushinda Copa Libertadores mwaka 2011 - mara yao ya kwanza tangu mwaka 1963 - Neymar alijiunga na Barcelona baada ya kuhusishwa na msururu wa vilabu vikuu vya Ulaya.
Akicheza pamoja na Lionel Messi na Luis Suarez katika safu ya ushambuliaji iliyojulikana kama 'MSN', Neymar aliwasaidia wababe hao wa Hispania kushinda La Liga, Copa del Rey na Ligi ya Mabingwa katika msimu wake wa pili tu.
Muda mfupi baada ya kujiunga na Barcelona, pia aliisaidia Brazil kushinda Kombe la Shirikisho la Fifa na kutajwa kuwa mchezaji bora wa michuano hiyo.
2014 - Huzuni nyumbani Kombe la Dunia
Kufikia sasa nyota ya Neymar ilikuwa inang'aa sana na, Brazil wakiwa wenyeji wa Kombe la Dunia 2014, alionekana na wengi kama mchezaji wa kuiongoza nchi yake kwenye utukufu.
Picha yake ilikuwa kila mahali kabla na wakati wa mchuano huo, lakini taifa lilishikilia pumzi yake wakati, katika robo fainali dhidi ya Colombia, Neymar alishuka akiwa amejishika mgongo baada ya kupigiwa goti na Juan Zuniga.
2014 - Aleta huzuni nyumbani wakati wa Kombe la Dunia
Kufikia mwaka 2014 nyota ya Neymar ilikuwa inang'aa sana na, Brazil wakiwa wenyeji wa Kombe la Dunia 2014, alionekana na wengi kama mchezaji wa kuiongoza nchi yake kwenye utukufu na kutwaa kombe.
Picha yake ilikuwa kila mahali kabla na wakati wa mchuano huo, lakini taifa liliingiwa na simaziumia baada ya kugongana na Juan Zuniga.
Brazil ilishinda 2-1, lakini ilikuja kwa gharama kubwa kwani Neymar aliondolewa na hakucheza michezo iliyosalia ya Kombe la Dunia kutokana na kuvunjika kwa uti wa mgongo.
Hali ilikuwa mbaya zaidi katika nusu-fainali huku Brazil ikipokea kichapo cha aibu cha mabao 7-1 kutoka kwa washindi Ujerumani.
2016 - Msimu wa kuvunja rekodi na dhahabu ya Olimpiki
Neymar, Messi na Suarez waliendelea kuwa miongoni mwa washambuliaji watatu hatari zaidi katika soka ya vilabu na mnamo 2015-16 kwa pamoja walifunga mabao 131 - mabao mengi zaidi kwa msimu kufungwa na wachezaji watatu wa ushambuliaji katika historia ya soka la Hispania.
Mabao hayo yaliisaidia Barcelona kutwaa mataji ya La Liga na Copa del Rey, kabla ya Neymar kujiunga na timu ya Brazil kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki ya 2016 huko Rio.
Miaka miwili baada ya jeraha lake la Kombe la Dunia, Neymar alifunga mkwaju wa penalti wakati Brazil ilipoishinda Ujerumani katika mikwaju ya penati na kushinda medali yao ya kwanza ya dhahabu ya Olimpiki kwa wanaume.
2017 - Kuhamia Ufaransa
Baada ya kufunga mabao 105 katika mechi 186, Neymar aligonga vichwa vya habari vya soka duniani kwa kuondoka Barcelona na kujiunga na PSG kwa kitita cha pauni milioni 200 mwaka 2017.
Mechi yake ya kwanza dhidi ya Guingamp mwezi Agosti alifunga bao moja na kutoa pasi moja. Akiwa sehemu ya washambuliaji watatu wakubwa pamoja na Kylian Mbappe na Edinson Cavani, Neymar alifunga mabao 28 katika mechi 30 huku PSG ikishinda mataji matatu ya Ligue 1, Kombe la Ufaransa na Kombe la Ligi.
Lakini msimu wake ulikatizwa alipopatwa na jeraha la kwanza kati ya kadhaa ambalo lingeharibu muda wake huko Paris.
2019-20 - Fainali ya Ligi ya Mabingwa lakini siku zijazo zisizo na uhakika
Baada ya miaka miwili PSG, Neymar alihusishwa na kurejea Barcelona na majira ya joto ya 2019 yalitawaliwa na tetesi za kuondoka kwake.
Aliikasirisha PSG baada ya kushindwa kuhudhuria katika siku ya kwanza ya mazoezi ya kujiandaa na msimu Julai, lakini mwishowe alibaki Paris.
Ingawa majeraha yaliathiri tena msimu wake, aliisaidia PSG kushinda taji la Ligue 1 na kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza, walipofungwa 1-0 na Bayern Munich.
2021-23 - Kupanda na kushuka kwa Neymar
Neymar aliungana tena na mchezaji mwenzake wa zamani wa Barcelona, Messi wakati nyota huyo wa Argentina alipojiunga na PSG Agosti 2021, lakini msimu huo ulikuwa wa kukatisha tamaa kwa Neymar kwani alimaliza akiwa na mabao 13 katika michuano yote - msimu mbaya zaidi tangu kuhamia Ulaya.
Pamoja na Messi na Mbappe, Neymar alionekana kurejesha kiwango chake tena, akifunga na kusaidia mabao 13 katika mechi zake tano za kwanza za ligi msimu wa 2022-23, lakini mwezi Machi aliumia na kutocheza katika kipindi kilichosalia cha msimu baada ya kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu.
Ushindi wa 4-3 dhidi ya Lille mwezi Februari, ambapo aliifungia PSG bao la pili, utakuwa mchezo wake wa mwisho kwa klabu hiyo.