Vita vya Ukraine: Mambo unayopaswa kufahamu juu ya mashambulizi yaliyofanywa usiku kucha Kyiv

Ukraine

Chanzo cha picha, Reuters

Iliyochapishwa

Takriban usiku mzima wa Mei 28, 2023 tahadhari ya angani iliendelea katika sehemu kubwa ya Ukraine, na Kyiv ilikumbana na mashambulizi makubwa zaidi ya ndege zisizo na rubani za kamikaze katika historia ya vita ya Ukraine. Katika mji mkuu, ambao unaadhimisha siku ya jiji, mmoja alipoteza maisha kutokana na shambulio la Warusi.

Mamlaka ya jiji la Zhytomyr pia iliripoti juu ya mashambulizi hayo. Utawala wa kijeshi wa eneo hilo unafafanua kuwa warusi wamelenga kushambulia moja ya miundombinu yake, lakini unadai kuwa hakuna walioathirika.

Shambulio la usiku kwenye mji mkuu lilikuwa la 18 tangu mwanzoni mwa Mei, Utawala wa Kijeshi wa Kyiv uliripoti. Kyiv alishambuliwa kutoka karibu pande zote, kusini, kaskazini, mashariki, magharibi ya mji mkuu na katika maeneo ya kati.

Mashambulizi yalianza saa 7 usiku na kusimama saa 12 alfajiri.

Wakazi katika mji huo wa Kyiv wanaelezea kwmaba usiku mzima kulikuwa na mafataki na milipuko inayoendelea, na kuongeza ilikuwa mikubwa na haikuwahi kusikikika kama hiyo - tangu makombora sita ya Dagger yaliyopigwa mara moja.

Kwa jumla, Warusi walirusha ndege 54 zisizo na rubani juu ya Ukraine, ambapo 52 zilidunguliwa, jeshi la anga lilisema.

"Leo, adui ameamua 'kuwapongeza' watu wa Kyiv Siku ya Kyiv kwa ndege zao za mauaji. Hapo awali, hili lilikuwa shambulio kubwa zaidi la ndege zisizo na rubani kwenye mji mkuu tangu kuanza kwa uvamizi Februari, 2022," Mamalak za kijeshi Kyiv zimeripoti.

Ukraine

Chanzo cha picha, Reuters

Kulingana na taarifa za awali, zaidi ya ndege 40 zisizo na rubani ziliharibiwa na vikosi vya anga vya Kyiv.

Uharibifu mkubwa zaidi na kuzagaa kwa uchafu ulikuwa katika wilaya ya Holosiiv kusini.

Kuna shambulio katika jengo lisilo la makazi, lililosababisha kifo cha mzee wa miaka 41, na mwanamke mwenye umri wa miaka 35 aliishia hospitalini.

Ukraine

Chanzo cha picha, KMVA

Maelezo ya picha, Athari katika moja ya nyumba za makazi ya watu

Moto ulizuka kwenye paa la moja ya maduka makubwa, kwenye eneo la ujenzi na katika maeneo ya viwanda. Ghala za bidhaa kwenye eneo hili la hadi mita za mraba elfu zilishika moto.

Katika wilaya ya Pechersk, uchafu ulianguka juu ya paa la jengo la makazi la ghorofa 9, moto ulizuka, na angalau ghorofa moja iliharibiwa vibaya.

Ukraine war

Chanzo cha picha, KMVA

Maelezo ya picha, Jengo hili huko Pechersk liliathirika

Katika wilaya ya Solomyan, kipande cha ndege isiyo na rubani kiliharibu ghorofa ya 3 ya jengo la ghorofa saba.

Katika wilaya ya Darnytsky, madirisha na milango ya moja ya maduka yalikuwa yameharibiwa vibaya.

Kama meya wa mji mkuu Vitaliy Klitschko alivyoripoti, kulikuwa kubwa ya ulinzi wa anga na urushaji wa ndege zisizo na rubani kaskazini mwa mji katika wilaya ya Obolon ambapo hakukuwa na uharibifu.

Muelekeo mpya wa mashambulizi ya Urusi

Ukraine

Chanzo cha picha, Reuters

Asubuhi, msemaji wa operesheni "Kusini" Natalya Gumenyuk aliripoti kwamba Warusi walitumia njia zisizo za kawaida wakati wa kushambulia Ukraine usiku wa kuamkia Mei 28, 2023.

"Walijaribu kukwepa ulinzi wa anga ya kusini kadiri ilivyowezekana, kwa hivyo walivuka maeneo yaliyokaliwa kwa muda na kisha kutawanyika kote Ukraini. Ukweli ni kwamba wanajaribu kutafuta mbinu mpya. Wanavuka hadi kwenye mito, - Humenyuk alisema.

Jeshi la anga liliripoti kwamba usiku wa Mei 28, 2023, Urusi ilishambulia Ukraine kutoka upande wa kaskazini - Mkoa wa Bryansk, na kusini - Wilaya ya Krasnodar.

"Shambulio lingine la usiku lilielekezwa na adui katika vituo vya kijeshi na vifaa vya miundombinu muhimu ya serikali katika mikoa ya kati ya nchi, haswa katika mkoa wa Kyiv. Ndege nyingi zisizo na rubani ziliharibiwa hapa," jeshi la anga lilisema.