Mwanamke ambaye amejiajiri kupitia uhalifu na urembo mtandaoni

Iliyochapishwa

Kwa wengine, kuna mambo machache ya kustarehesha zaidi kuliko kushikilia mafunzo ya kujipodoa kwenye YouTube.

Halafu kuna wale ambao wanapenda video za kujipodoa zilizojaa visa vya wauaji hatari na uhalifu wao. 

Ina maanisha nini?

Sio kwa watumiaji milioni 6.4 wa Bailey Sarian wa Los Angeles, msanii wa urembo wa kujipodoa mtandaoni ambaye amegeuka kuwa nyota wa uhalifu.

Video zake za YouTube zinazochanganya mada hizi mbili zinazopingana kabisa  katika mfululizo unaoitwa Murder, Mystery & Make-up, zimegeuka kutoka kuwa kitu anachopenda hadi kuwa kazi ya muda wote ambayo, pamoja na mambo mengine, imempatia mikataba mikubwa na makampuni kama vile Netflix.

Bailey mwenye umri wa miaka 33 mwenyewe anashangaa kwamba YouTube na uhalifu wa kweli - umekuwa ni kazi yake kwa siku.

"Nilidhani ni vizuri kupata pesa kutoka kwa YouTube, kulipa baadhi ya bili," Bi Sarian aliambia BBC. "Sasa kwa kuwa nimefika hapa na zaidi ya watu milioni sita waliojisajili, ni wengi sana. Sikuwahi kufikiria kwamba ingebadilika kuwa kama ilivyo leo."

Msingi wa video zake ni rahisi. Sarian anakaa mbele ya kamera, akijipodoa na kuzungumza kuhusu hadithi ya uhalifu ya kweli. Kila video inachukua kiasi kikubwa cha utafiti  kitendo kilichomfanya Sarian sasa kuajiri mtu wa kumsaidia  ambapo anajumuisha maelezo kutoka katika nakala za mahakama au mahojiano ya polisi.

Video maarufu zaidi katika mfululizo huu ni kuhusu muuaji Mmarekani Jeffrey Dahmer, ambaye aliwaua wanaume na wavulana 17 kati ya mwaka 1978 na 1991 na ambaye Sarian anamzungumzia alipokuwa akitengeneza sura yenye macho ya kijani inayometa pamoja na midomo yenye rangi ya asili yakupoa(nude).

Video hiyo imetazamwa zaidi ya mara milioni 22. Kwa muktadha tu, sehemu ya mwisho ya tamthilia ya Line of Duty imetazamwa kwa kuvunja rekodi ya watu milioni 12.8 nchini Uingereza. Kwa ujumla, video za YouTube za Sarian zimetazamwa karibu mara milioni 800.

Lakini kwa nini inafanya kazi? Hata Sarian hana uhakika: "Kusema kweli, hilo ndilo jambo moja ambalo bado sijafikiria ni kwa nini watu wanapenda vitu vya urembo."

Ajabu ni kwamba jambo hilo lote lilitokea kwa bahati mbaya.

Hadi karibu miaka mitatu iliyopita, Sarian alikuwa ameweka hasa mafunzo ya urembo kwenye chaneli yake ya youtube, ambayo alikuwa ameanzisha mwaka wa 2013. 

Alikuwa akichanganya kutengeneza video za YouTube na kazi yake kama msanii wa urembo wa vipodozi. Baada ya kupata mkataba na kampuni ya urembo ya Ipsy, Sarian aliweza kutegemea zaidi YouTube kwa mapato yake, ingawa aliendelea kujiajiri mara kwa mara.

Mwaka 2018, aliibua hadithi kuhusu mwanamume wa Colorado anayeitwa Chris Watts ambaye alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa mauaji ya mkewe mjamzito Shanann na binti zao wawili wachanga Bella na Celeste. Ulikuwa ni uhalifu wa kushtua ambao ulitangazwa ulimwenguni kote lakini Sarian alitaka kuonesha jinsi mtu alivyobadilika kutoka kuwa mume mzuri hadi kuua familia yake.

Alikuwa na woga wa kawaida kuzungumza kuhusu hilo. Maneno ya kuchukiza ya mtandaoni sio mzaha, hata hivyo. Ili kukabiliana na hilo, alifanya kile ambacho amekuwa akifanya kila mara akijipodoa.

"Nilikuwa nikifanya hivyo kwa sababu nilijisikia vibaya kukaa tu kwenye kamera nikizungumza na nilitaka kujiweka busy," anasema.

Alikuwa bado na wasiwasi kuhusu mwitikio wa uhalifu huo, ambayo alitarajia ungekuwa mbaya, "kwa sababu nilikuwa najipodoa na kuzungumza juu ya uhalifu wa kutisha, unajua, haileti maana".

Ndani ya saa 24 ingawa alijua kwamba alikuwa akifanya jambo tofauti huku nambari za kutazama zikiwekwa. Video ya Watts hatimaye iliishia kutazamwa na watu milioni 10.

"Kwa hivyo nilifikiria, 'Labda, wacha nijaribu tena na hadithi tofauti na nione kama itafanya vizuri kama hiyo.' Na ilifanyika, na niliendelea tu na kila wiki ilikuwa watu zaidi wanaojisajili na kunifuatilia zaidi, "anasema Bi Sarian.

Dk Ruth Tully, mwanasaikolojia mshauri wa uchunguzi wa mahakama ambaye amefanya kazi katika kesi mbaya za uhalifu, anaamini kwamba mchanganyiko huo hufanya kazi kwa sababu ya namna wengi wetu hutazama maudhui siku hizi.

Tunaweza kuwa na jicho moja kwenye televisheni na jingine kwenye simu au kompyuta zetu, inayojulikana kama "kuangalia kwa pamoja".

"Kwa upande mmoja anafanya kitu ambacho, watu wanaweza uvutiwa sana katika suala la kutazama mtu akijipodoa, Kwa hivyo watu wanapenda kutazama kipengele kwa wanavyoona lakini pia anasimulia hadithi hiyo," anasema Dk Tully.

"Tunafikiria kuhusu kipengele cha uhalifu ambacho anajadili lakini pia kuna kitu cha kutazama ambacho sio cha kutisha sana ambacho kinaweza kuwa cha kushangaza kwa njia fulani."

Pia kuna idadi ya watu. Picha ya watu waliotazama maudhui ya uhalifu wa kweli kwenye YouTube kati ya Januari na Juni 2020 iligundua kuwa 60% walikuwa wanawake. Sarian anasema ni wanawake wengi wanaotazama video zake, huku kundi kubwa zaidi wakiwa na umri wa kati ya miaka 25 na 35, wakifuatiwa na wenye umri wa miaka 18 hadi 25.

"Kuna mawazo machache kuhusu kwa nini hasa wanawake wanavutiwa na hili," anasema Dk Tully. "Sehemu ya hii imetajwa kama njia ya kushughulikia wasiwasi wetu na hiyo ni kuhusu kujilinda. Hilo linaweza kusababishwa na ukosefu wa imani katika mifumo kwa baadhi ya wanawake pia."

Sarian anasema: "Ninapoogopa kitu, ninajaribu kukibaini, inasaidia wasiwasi. Angalau ndiyo sababu nakuwa nahangaika nacho."

Janga la Covid pia lilichochea idadi ya waliojiandikisha kwani kufungiwa ndani kulisababisha watu kuangalia sana televisheni, filamu na kitu kingine chochote ambacho kingeweza kupoteza muda wakati huo. Wakati Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump akitoa wito wa dharura ya kitaifa Machi 2020, Sarian alikuwa na watu zaidi ya 780,000 waliojiandikisha. Kufikia mwisho wa mwaka, alifikia milioni 3.5 na sasa ana karibu mara mbili ya hiyo.

"Hakukuwa na kitu cha kutazama," anasema Sarian. "Kila mtu alikuwa kwenye YouTube na watu walianza kutafuta chaneli yangu na kutazama video zangu zote kupita kiasi na nilipata ujumbe na maoni mengi kutoka kwa watu wakisema, 'Ulinipisha karantini.'

Pia imepanua wigo wa kazi yake. Sarian sasa anafanya kazi na kampuni ya uzalishaji ya Marekani ya Wheelhouse DNA kwenye podcast na mfululizo wa video unaoitwa Historia ya Giza yenye vipindi kama  "Who stole grandma's body?! The Doctors' Riots ya 1788".

Pia kuna mkataba na Netflix kwenye chaneli yake ya YouTube ambapo anatazama filamu na kujaribu kujua simulizi za mauaji ya kutisha, ambayo anasema alipata baada ya  mtu mmoja wa Netflix kukutana na chaneli yake.

Nyuma ya hadithi za kweli za uhalifu anazozungumza pia huzungumzia waathirika halisi Je, Sarian amewahi kujihisi kuwatendea isivyo sawa?

"Sasa kwa kuwa chaneli yangu imekua najiona nina jukumu zaidi juu ya kile ninachosema kwa hivyo mbinu yangu imekuwa kulenga zaidi wauaji na sio kutaja sana waathirika kuonyesha picha zao," anasema.

"Ninahisi kama siwezi kuwasemea isipokuwa ninazungumza na familia moja kwa moja. Wameishi maisha marefu kwa nini wakumbukwe kwa jambo hili moja?"

Amewasiliana na watu waliounganishwa na kesi kadhaa ambazo ameshazijadili. "Kulikuwa na maoni mazuri kila wakati na wanataka kuongeza zaidi." Anasema kwamba ikiwa mtu yeyote aliyehusishwa na uhalifu alikasirishwa na video angeiondoa "hakuna maswali yaliyoulizwa".

Kwa hivyo ni nini kinachofuata? Sarian ana mfululizo mwingine wa Historia ya Giza utakaotoka tarehe 3 Agosti na angependa kuona Mauaji, Siri na Uundaji vikihamia katika jukwaa kubwa zaidi, labda huduma ya kuonesha maudhui mtandaoni.

"Lakini kwa kweli sina uhakika," anasema. "Nimejifunga tu, naenda sambasamba na safari."