Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 04.09.2023
Nahodha wa zamani wa Uhispania Sergio Ramos, 37, amepiga hatua katika mazungumzo ya kurejea kwake Sevilla miaka 18 baada ya kuondoka katika klabu hiyo na kujiunga na Real Madrid. Beki huyo aliondoka Paris St-Germain msimu huu wa joto wakati mkataba wake ulipomalizika. (ESPN)
Kakake Joao Palhinha anasema uhamisho wa kiungo wa Ureno na Fulham kwenda Bayern Munich "uliahirishwa", baada ya mazungumzo kuvunjika siku ya mawisho ya uhamisho wa wachezaji. (Mail)
Chelsea ilitoa nafasi kwa Tottenham kumsajili kiungo wa kati wa England James Maddison, 26, msimu wa joto kwa sababu hakuendana na wasifu wa umri wa walengwa wao wa uhamisho. (Football Insider)
Kipa wa zamani wa Manchester United na Uhispania David de Gea, 32, ni miongoni mwa wachezaji kadhaa wanaopatikana kwa uhamisho wa bure ambao unavutia klabu za Saudia. (Marca kwa Kihispania)
Winga wa Atletico Madrid na Ubelgiji Yannick Carrasco, 29, anatazamiwa kuhamia Al Shabab ya Saudia kwa £12.8m. (ESPN)
Matumaini ya meneja Wayne Rooney kuwasajili tena kiungo wa Jamaica Ravel Morrison, 30, kiungo wa kati wa Uingereza Jesse Lingard, 30, na mshambuliaji wa Ghana Andre Ayew, 33, ambao wote ni wachezaji huru, yamezimwa na masuala ya mishahara katika klabu ya MLS DC United. (Washington Post - usajili unahitajika)
Klabu ya Monaco ya Ligue 1 inapanga kumsajili beki wa Fulham Muingereza Tosin Adarabioyo, 25, mwezi Januari baada ya kujitahidi sana kufanikisha dili lake katika uhamisho wa msimu wa kiangazi. (Fabrizio Romano)
Barcelona hawajafurahishwa na majaribio ya Manchester City kumsajili beki wa kushoto wa Uhispania Alejandro Balde, 19, winga aliyeitwa Lamine Yamal, 16 na mchezaji wa kimataifa wa Uhispania Pau Cubarsi, 16, msimu huu. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)
Beki wa Chelsea na Brazil Thiago Silva, 38, alizozana na mashabiki kwenye Instagram baada ya klabu hiyo kushindwa na Nottingham Forest katika mechi ya Ligi ya Premia na siku ya Jumamosi. (Telegraph - usajili unahitajika)