Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwanini tunakoroma na je ni wakati gani kukoroma kunakuwa tatizo?
Kukoroma ni sauti inayotolewa na mtetemo wa tishu za koromeo unaosababishwa na kupungua kwa misuli ya njia ya upumuaji.
Sababu ni tofauti : kuna wengine wanakoroma wanapolala chali, baada ya kwa mfano kunywa pombe au kutumia dawa. Pia wapo wanaokoroma kutokana na mabadiliko ya kianatomia, kama vile mafindo findo au kutokana na sababu kama vile kunenepa kupita kiasi, kuvuta sigara, mimba na historia ya magonjwa ya mzio.
"kubadilisha namna ya kulala, kupumzika kwa misuli wakati wa kulala na sehemu zinazowezekana za kupungua huamua mabadiliko katika mtiririko wa hewa, na kusababisha kelele tofauti - kukoroma - na hata wakati ambapo kuna kizuizi kamili cha uingiaji wa hewa; apneas," anasema Edilson Zancanella, rais wa Chama cha Brazili cha dawa za Usingizi, mratibu wa huduma ya matatizo ya usingizi katika Hospitali ya das Clínicas da Unicamp na mkurugenzi wa Shirika la Usingizi la Brazil.
Inakadiriwa kuwa karibu nusu ya watu wazima duniani wanakoroma, na kwa upande wa watoto, mtoto mmoja kati ya 10 anakoroma pia.
"Kukoroma ni ishara ya onyo, au dalili mbaya. Kwa ujumla, kukoroma ni ishara kwamba njia ya hewa imezuiliwa, imepunguzwa ukubwa," Luciane Mello, mtaalamu wa magonjwa ya mapafu na mtafiti katika Taasisi ya Usingizi, aliambia BBC.
Mbali na athari za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, inahitajika pia kuchunguza uwepo wa patholojia, kama vile 'apnea' ya kuzuia usingizi, kuziba kwa njia ya hewa kwenye koo ambayo husababisha mtu kuacha kupumua kwa muda (katika hali mbaya inaweza hata kusababisha kifo).
Hata hivyo, ingawa inaweza kuonekana kama kukoroma ni suala la kawaida, ila wataalama wanasema sivyo, usichukulie jambo la kawaida.
Kulala na mtu anayekoroma
Ni kawaida kwa mtu kugundua kwamba anakoroma kupitia kwa mtu mwingine, inaweza kuwa jamaa au mtu wa karibu au mume ama mke anayelala naye.
Mara nyingi urafiki huu hauna raha, wengine hutafuta matibabu, na katika hali zingine mbaya hata husababisha kutengana kwa wanandoa. Inafaa kukumbuka kuwa wanaume huwa wanakoroma zaidi kuliko wanawake.
"Hii ni kwa sababu koromeo lao ni kubwa na lina uwezo mkubwa wa kuathirika. Wanawake huanza kukoroma zaidi baada ya kukoma hedhi, katika hatua ya climacteric, kutokana na kupungua kwa homoni kama vile estrogen na progesterone," anafafanua Danilo Sguillar, kutoka Idara ya Tiba ya Usingizi Brazil.
Lakini kukoroma sio tu ishara kwamba kuna kitu kibaya au husababisha shida za kijamii kwa wale wanaolala nao karibu.
Afya ya kimwili, kiakili na kijamii ya wale wanaokoroma pia inaweza kuathiriwa sana . Pia inahusiana na usiku usio na utulivu, usingizi usio bora kunahusishwa na hatari ya kuongezeka kwa ugonjwa wa moyo, kiharusi, matatizo ya mfadhaiko, na matatizo mengine yanayohusiana na afya.
Kukoroma ni nini na yapi ni madhara yake?
Njia za juu za hewa imeundwa na pua na koromeo. Na "kukoroma si kitu zaidi ya kuzunguka kwa hewa mahali ambapo njia ya juu ya hewa imefinywa," Sguillar anaelezea.
Kwa kupungua huku kwa njia ya hewa, kuna kupunguzwa kwa mtiririko wa hewa ambayo huharibu oksijeni wakati wa usingizi, kufikia kizuizi cha jumla katika baadhi ya matukio (kinachojulikana apnea).
Kelele hii ya kukoroma pia inaweza kuhusishwa na kulegea kwa misuli, mabadiliko ya kufungwa kwa koromeo, mabadiliko ya homoni na, mara nyingi, matumizi ya vitu vinavyosababisha utulivu mkubwa wa misuli, kama vile pombe, anxiolytics (dawa za matatizo ya wasiwasi) na kupumzika kwa misuli.
Bila kuangalia namna gani unalala: kulala chali kunaweza kusababisha kukoroma kwa sababu unavyolala kuna athiri nafasi ya ulimi ndani ya kinywa, kwa ndani.
Hili linahusishwa kawaida na kukosa usingizi mzuri usiku. Kulala vizuri ni jambo muhimu kwa afya na ubora wa maisha: ni wakati wa usingizi kwamba misuli hupumzika, homoni hutolewa na kumbukumbu huimarishwa.
Kwa ujumla, utulivu, usingizi wa utulivu sio mgumu na hauingiliki na hudumu kwa saa 7-9 kwa watu wazima na saa 12-17 kwa watoto, kulingana na NHS.
Kwa upande mwingine, athari za usingizi wa usiku usio mzuri, ama ukilala hovyo, athari zake zinaweza kuonekana siku inayofuata, ikiwemo kuharibu kumbukumbu.
Namna gani ya kutibu Kukoroma?
Matibabu hutegemea sababu na inaweza kuhusisha idara nyingi za kliniki na wataalamu wa afya. Kwa wale wanaokoroma kidogo, ama katika kesi ya kuziba pua kutokana na mafua, kwa mfano, kubadilisha tu namna ya kulala kunaweza kutosha kupunguza au kutatua tatizo.
Hii ni pamoja na kulala kwa upande wako na kuinamisha sehemu ya juu ya mwili wako kwa usaidizi wa mto, kwa mfano, ambayo inaweza kusaidia kuweka njia zako za juu za hewa wazi (kuna chaguzi za mto wa kuzuia kukoroma ambazo mtaalamu wa afya anaweza kupendekeza).
Mabadiliko ya mtindo wa maisha pia yanapendekezwa, kama vile kupunguza uzito, kuacha kuvuta sigara na matibabu ya mizio na magonjwa ya kupumua (ikiwa hii ndio sababu inayohusishwa na kukoroma), kufanya mazoezi ya mwili, kudhibiti shinikizo la damu na kufanya mazoezi. ambayo huimarisha muundo wa koo.
Matibabu yanaweza pia kujumuisha vipunguza pua, steroidi za ndani ya pua, na kile kinachoitwa kitaalam adenotonsillectomy. Lakini yote haya yanaweza kufafanuliwa tu baada ya uchunguzi na mtaalamu wa afya.
Katika hali ya wastani na kali, matumizi ya mashine ya hewa (CPAP) inaweza kupendekezwa, kwani inasaidia kuweka njia ya hewa wazi kupitia mkondo wa hewa.
Huvaliwa na kinyago kilichounganishwa kwenye mrija, kama vile zile zinazotumiwa kuvuta pumzi, ambapo mkondo wa hewa unapita kwenye koo na kuweka njia ya hewa wazi usiku.
Aina ya mashine hizi lazima zionyeshwe na mtaalamu anayemtibu mgonjwa.
"Iwapo kuna kizuizi cha pua, mara nyingi tunawafanyia upasuaji wagonjwa hawa ili kuboresha hali hii ya pua. Kuziba kwa pua na 'rhinitis' wakati mwingine husababisha kukoroma usiku na ikiwa tunafanikiwa kutibu ugonjwa wa rhinitis. , tutaboresha kukoroma", anaeleza Mello, kutoka Taasisi ya Usingizi.
"Mara nyingi tunatibu njia ya hewa, kwa tiba maalum ya kuimarisha misuli, ambayo husaidia katika suala hilo la kukoroma. Lakini yote inategemea sababu ama kile kinachosababisha kukoroma.
Tunamchunguza kila mgonjwa na kutathmini ni mkakati gani bora ama njia gani tutumie", anahitimisha mtaalam.
End of Unaweza pia kusoma