Tetesi za soka Ulaya Ijumaa: Casemiro kumfuata Ronaldo Al-Nassr?

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Al-Nassr anayochezea Christiano Ronaldo, wanalenga kumsajili kiungo wa Manchester United, Casemiro, 33, huku mkataba wa Mreno huyo katika Old Trafford ukitarajiwa kumalizika majira ya joto. (Mundo Deportivo)

Manchester United wanapigana vikumbo na Atletico Madrid na Barcelona kumsajili mshambuliaji wa Serbia, Dusan Vlahovic, 25, ambaye mkataba wake huko Juventus unamalizika majira ya joto yajayo. (La Gazzetta dello Sport, via Teamtalk)

Real Madrid wanaonyesha nia ya kumsajili beki wa Tottenham Hotspur, Micky van de Ven, 24, huku klabu hiyo ya kaskazini mwa London ikimthaminisha Mholanzi huyo kwa dau la takriban pauni 70 milioni. (Fichajes)

Inter Miami wako karibu kumpa mkataba mpya wa muda mrefu mshambuliaji wa Argentina, Lionel Messi, 38, aliyesajiliwa kwa mara ya kwanza na klabu hiyo ya MLS mwaka 2023. (ESPN)

Nyota wa Liverpool na Italia, Federico Chiesa, 27, anaweza kuondoka Anfield katika dirisha la usajili la Januari kurudi Italia. (Teamtalk)

Kocha wa Liverpool, Arne Slot anataka kumsajili beki wa Ajax, Youri Baas, 22 pale Anfield, ingawa Mholanzi huyo ana mkataba mrefu wa hadi 2028. (Fichajes)

Kocha wa Croatia, Slaven Bilic, anawaniwa na West Ham kuchukua nafasi ya Mwingereza Graham Potter iwapo klabu ya Ligi kuu England (EPL) itafanya mabadiliko ya kocha. (Talksport)

Kocha wa zamani wa Nottingham Forest, Nuno Espirito Santo, na Mwingereza Sean Dyche pia wako katika mjadala wa kuchukua nafasi ya Potter West Ham. (Guardian)

Tottenham ni miongoni mwa klabu kadhaa za EPL zinazovutiwa na kiungo wa Atletico Madrid na England, Conor Gallagher, 25. (TBR Football)

AC Milan wanaonyesha nia ya kumleta beki wa Udinese wa Denmark, Thomas Kristensen, 23, ambaye alikuwa akiswakwa na Aston Villa katika dirisha la usajili lililopita. (La Gazzetta dello Sport)

Manchester United itamruhusu mshambuliaji wake Mholanzi, Joshua Zirkzee, 24, kuondoka klabu hapo huku mshambuliaji wa Slovenia, Benjamin Sesko, 22, akiwa sasa ndiyo chaguo la kwanza. (Teamtalk)

Kiungo wa Barcelona na Hispania, Alexia Putellas, 31, alikataa ofa kubwa ya fedha kujiunga na timu ya wanawake ya Paris St-Germain, huku klabu hiyo ya Ufaransa ikikubali kulipa euro 1 milioni. (ESPN)