Marilyn vos Savant: Mwanamke mwenye akili nyingi zaidi duniani

Katika miaka ya 1980, Marilyn vos Savant alizingatiwa "mtu mwenye akili zaidi duniani".

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Katika miaka ya 1980, Marilyn vos Savant alitajwa kuwa "mtu mwenye akili zaidi duniani".
Iliyochapishwa

Hebu tafakari unashiriki onyesho la mashindano.

Una nafasi ya kushinda gari mpya, lakini ili kuipata, unapaswa kuchagua moja kati ya milango mitatu ambayo ina funguo wa kufikia gari hilo.

Nyuma ya milango miwili iliyisalia kuna tuzo ambayo haitamhakikishia mtu yeyote- ushindi.

Tuseme kwa mfano umeamua kuchagua mlango wa pili, ulio katikati na ambao unakupa hisia kwamba ndio unaweza kuwa na ufunguo wa zawadi kuu.

Mtangazaji anayeendesha shindano hilo anataka kukusaidia kwa kukupatia fununu itakayokuwezesha kufichua kilicho nyuma ya mlango mmoja (tayari anajua ufunguo wa gari unaloshindania ziko wapi).

Marilyn Vos Savant

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Marilyn Vos Savant

Kwa hiyo anafungua mlango wa 3, ambapo mbuzi ambaye amefungwa kwa muda mrefu anaonekana.

Mtangazaji anakufanyia pendekezo: je, utasalia na mlango wa 2 uliyochagua ama ungependelea kuubadilisha na kwenda kwa mlango wa nambari 1?

Unaanza kufikiria kwa makoni ukifahamu fika kwamba umesalia na chaguo mbili na moja kati hilo linaweza kuwa sahihi kwa asilimia 50 na kushinda gari, na asilimia 50 iliyosalia inaweza kuwa ya kuondoka mbuzi.

Lakini ukitafakari kwa makini zaidi, kama Marilyn vos Savant alivyofanya, una karibu nafasi ya theluthi mbili ya kushinda gari.

Na yote yanafungamana na kitu rahisi au ngumu kama uchanganuzi wa uwezekano.

Uwerevu wake

Marilyn Mach vos Savant, ambaye sasa ana umri wa miaka 76, alikuwa mwandishi wa muda mrefu wa safu ya gazeti la "Ask Marilyn," ambapo alijibu maswali, kutoa mafumbo, na kutoa maoni yake juu ya mada tofauti.

Yeye pia ni mwandishi wa vitabu vya hadithi, na amekuwa mjasiriamali katika masuala ya uwekezaji. Lakini utotoni mwake alikuwa na jina lingine, la kushangaza zaidi.

Baada ya kufanyi vipimo vichache vya uwezo wa kiakili, alipata alama 228 kwenye mojawapo, zaidi ya mara mbili ya wastani.

Kitabu cha kumbukumbu cha Guinness kilimfuatilia na kumuorodhesha kutoka 1985 hadi 1989 kama mwanamke mwenye akili nyingi zaidi kuwahi kurekodiwa. Kwa sababu hii, aliitwa "mtu mwenye akili zaidi duniani".

B
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Vos Savant ni binti wa wahamiaji wa Ulaya walioishi katika jiji la St. Louis, Missouri, katikati mwa Marekani, ambako alizaliwa Agosti 1946.

Aliamini kwamba watu wanapaswa kutambulishwa kwa majina ya wazazi wote wawili. Kwa hivyo alichukua jina la kijakazi la mama yake, Savant, ambalo cha kushangaza linamaanisha "mtu mwenye busara" kwa Kifaransa.

Kipindi chote cha masomo yake, alifanya vyema katika somo la hesabati na sayansi shuleni. Akiwa na umri wa miaka 10, alifaulu majaribio ya Stanford-Binet na Hoeflin ya Mega IQ. Kiwango cha mwisho cha majaribio hayo ambapo anapata alama 228, ambayo shirika la Guinness linazingatia.

Tangu wakati huo, amekuwa akizingatiwa kuwa mtoto mchanga, ambayo haijabadilisha njia yake ya maisha. Akiwa kijana, alisema alisaidia katika duka la wazazi wake na alipenda sana kusoma.

Badala ya kupendezwa na chuo kikuu cha kifahari cha Marekani cha Ivy, aliamua kusomea falsafa katika Chuo Kikuu cha Washington, katika mji aliozaliwa wa Saint-Louis. Lakini, aliacha masomo yake alijishughulisha na biashara ya uwekezaji wa familia.

Lakini umaarufu wake wa mtihani wa IQ ulimfuata.

Vos Savant na mume wake Robert Jarvik

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Vos Savant na mume wake Robert Jarvik

Katika miaka ya 1970, alipata pesa za kutosha kufadhili ndoto yake ya kuwa mwandishi. Ameshiriki katika uchapisha majaribio ya kijasusi, kama vile Shindano la Omni IQ na Chemsha Bongo, pamoja na kazi zake za kifasihi na makala kwenye majarida na magazeti.

Baada ya kuhamia New York, alishiriki kwenye kipindi cha mazungumzo cha David Letterman na Joe Franklyn. Karibu kila mara alipokea maswali juu ya akili ni nini.

"Akili inaweza kuwa uwezo wako wa jumla wa kufaidika kutokana na uzoefu, anaelezea Joe Franklyn. IQ inaweza, hata kidogo, kupima uwezo wako wa kutumia akili hii."

Wakati huo, alianzisha makala ya "Ask Marilyn" (Muulize Marilyn), iliyosambazwa kitaifa katika jarida la Parade na kujumuishwa katika magazeti kadhaa.

Ilikuwa mwaka wa 1989 ambapo aliulizwa kuhusu tatizo la kuchagua mlango gani wa kushinda tuzo hiyo. Jibu lake lilizua gumzo, hata miongoni mwa wanatakwimu na wanasayansi.

Jibu la kitendawili

Wazo la kitendawili cha gari na mbuzi halikuwa geni lilipoonekana kwenye makala ya Savant.

Miongo michache mapema, ilijulikana kama "Monty Hall problem"

Mmoja wa watafiti, Steve Selvin, aliwasilisha matokeo katika jarida la chuo cha American Statistician mnamo 1975.

Lakini jibu la vos Savant, lililozingatiwa na jibu la Selvin, ndilo lililozua mjadala.

"Bila shaka, inatarajiwa kubadilika. Mlango wa kwanza una nafasi ya theluthi moja ya kushinda, lakini mlango wa pili una nafasi ya theluthi mbili. Hii ndiyo njia bora ya kujua kilichotokea. Tuseme kuna milango milioni moja na uchague mlango wa kwanza.

Mwanzilishi wa mashindano hayo, anayejua kilicho nyuma ya mlango na ajaribu kupita mlango halisi ulio na sifa hii, afungue zote, isipokuwa nambari ya mlango 777,777. Kwa hivyo inamaanisha usibadilishe mlango mara moja?", tunaweza kujifunza hayo kutokana na lililotolewa na mama yangu.

Baada ya hapo Bw. Savant alisema kwamba alipokea barua karibu 10,000, ikiwa ni pamoja na barua 1,000 kutoka kwa maprofesa wa vyuo vikuu na watahiniwa wa udaktari katika nyanja tofauti, kama ilivyoripotiwa na New York Times katika makala iliyochapishwa mwaka wa 1991.

Robert Sachs, profesa katika Chuo Kikuu cha George Mason huko Virginia, alisema: "Yote ni ukijinga! Kama mtaalamu katika chuo kikuu, nina wasiwasi kuhusu ukosefu wa elimu ya chuo kwa umma. Tafadhali kubali kwamba siku zijazo utakuwa makini zaidi."

Vos Savant alitumia muda mrefu kutetea jibu lake, ingawa kulikuwa na wakosoaji wengi.