Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
MI6 na CIA: Mfumo unaoongoza dunia unakabiliwa na tisho kubwa kuwahi kushuhudiwa tangu Vita Baridi
Mfumo wa kimataifa wa dunia "unakabiliwa na tisho kwa njia ambayo hatujaona tangu Vita Baridi", wakuu wa idara za ujasusi wa kigeni wa Uingereza na Marekani wameonya.
Wakuu wa MI6 na CIA pia walisema nchi zote mbili zimenashirikiana kwa pamoja katika "kupinga Urusi yenye uthubutu na vita vya uchokozi vya Putin nchini Ukraine".
Katika makala ya kwanza kabisa ya pamoja, Sir Richard Moore na William Burns waliandika katika gazeti la Financial Times kwamba waliona vita vya Ukraine vikija mapema "na waliweza kuionya jumuiya ya kimataifa", kwa kwa kufuta siri za kuisaidia Kyiv.
Wamesema pia kwamba kuna kazi inayofanywa "kuvuruga kampeni ya kizembe ya hujuma" kote Ulaya inayofanywa na Urusi, kushinikiza kuzuka kwa vita vya Israel-Gaza, na kupambana na ugaidi ili kuzuia Dola ya Kiislam (IS) inayoibuka tena.
Katika ukurasa wa maoni wa gazeti hilo, FT op-ed, waliandika: "Hakuna shaka kwamba utaratibu wa kimataifa wa ulimwengu - mfumo wa usawa ambao umesababisha amani na utulivu wa kadiri na kutoa viwango vya maisha vinavyopanda, fursa na ustawi - unakabiliwa na jisho kwa njia ambayo haijawahi kuonekana tangu Vita Baridi."
"Kupambana na hatari hii kwa mafanikio" ni msingi wa uhusiano maalum kati ya Uingereza na Marekani, waliongeza.
Mojawapo ya "vitisho vingi" vinavyozikabili nchi zote mbili ni vita nchini Ukraine, ambayo ni mwaka wake wa tatu baada ya uvamizi wa Urusi mnamo Februari 2022.
Sir Richard na Bw Burns walisema "kusalia katika umakini ni muhimu zaidi kuliko hapo awali" linapokuja katika suala la kuiunga mkono Ukraine, na kuongeza kuwa Rais wa Urusi Vladimir Putin "hatafaulu".
Mgogoro huo umeonyesha jinsi teknolojia inavyoweza kubadilisha mkondo wa vita, na kusisitizia haja ya "kubadilika, kufanya majaribio na kuvumbua", walisema.
Waliendelea kusema kuwa : "Zaidi ya Ukraine, tunaendelea kufanya kazi pamoja ili kuvuruga kampeni ya hujuma kote Ulaya inayoendeshwa na ujasusi wa Urusi, na utumiaji wake wa kijinga wa teknolojia kueneza uongo na habari potofu zilizobuniwa ili kusababisha mifarakano kati yetu."
Wawili hao pia walionekana kwa mara ya kwanza katika wmazungumzo ya hadharani wakiwa pamoja katika Tamasha la Wikendi la FT katia jumba la Kenwood House mjini London Jumamosi.
Bwana Burns aliwaambia waliohudhuria kuwa haoni ushahidi kwamba nguvu ya Bw Putin kwenye mamlaka ilikuwa ikidhoofika, huku Sir Richard akiongeza: "Usiwahi kuchanganya mtego imara na mshiko thabiti."
Ukweli kwamba huduma za kijasusi za Urusi zinatumia vipengele vya uhalifu kwa shughuli za hujuma Ulaya ni ishara kwamba "wanakata tamaa kidogo", alisema mkuu wa MI6.
Huduma zote za kijasusi za kigeni zinashuhudia kuinuka kwa Uchina kama changamoto kuu ya kijasusi na kijiografia ya karne hii. Wamepanga upya huduma zao "ili kuakisi kipaumbele hicho", wawili hao walisema katika maoni yao.
Pia walisema wamesukuma "nguvu" kwa kujizuia na kupunguza kasi katika Mashariki ya Kati, na wamekuwa wakifanya kazi "bila kukoma" ili kufikiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano na utekaji nyara.
Bwana Burns, ambaye amekuwa akiongoza juhudi za kusitisha mapigano, alisema kunaweza kuwa na pendekezo la kina zaidi katika siku zijazo.
"Hatimaye hili ni suala la utashi wa kisiasa," alisema, akiongeza kuwa "kwa kiasi kikubwa" anatumai viongozi wa pande zote mbili watafanya makubaliano.
Ni miezi 11 tangu Hamas iliposhambulia kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba, na kuwaua takriban watu 1,200 na kuwachukua mateka wengine 251.
Zaidi ya watu 40,000 wameuawa huko Gaza tangu wakati huo katika mashambulizi ya kijeshi yanayoendelea ya Israeli, kulingana na wizara ya afya ya eneo hilo inayoendeshwa na Hamas.
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi