Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 29.08.2022

Iliyochapishwa

Wakala wa mshambuliaji wa Manchester United na Ureno Cristiano Ronaldo amerejea Chelsea akichunguza iwapo kuhamia Stamford Bridge kunawezekana kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37. . (Independent)

Chelsea wamefufua nia yao ya kumnunua fowadi wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha, 29, lakini mshambuliaji wa Barcelona na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 33, anasalia kuwa kipaumbele chao cha kwanza.  (Guardian)

Hata hivyo, Manchester United pia wameuliza kuhusu uwezekano wa uhamisho wa Aubameyang. (Caught Offside)

Ajax wanamlenga winga wa Chelsea na Morocco Hakim Ziyech, 29, kuchukua nafasi ya Antony, 22, baada ya kukubali ofa kutoka kwa Manchester United kwa ajili ya kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil. (Mail)

Chelsea wametoa ofa kwa mshambuliaji wa Everton Albania Armando Broja, 20, na kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher, 22, pamoja na £25m ili kumnunua mshambuliaji wa Uingereza Anthony Gordon, 21. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 25, anatarajiwa kusalia Nou Camp msimu huu wa joto, licha ya Manchester United, Chelsea na Liverpool kumtaka. (CBS Sports)

 Valencia wana uhakika wa kuipiku Real Sociedad katika kumsajili Edinson Cavani, 35, na wanatarajiwa kumpa mshambuliaji huyo wa Uruguay mkataba wa miaka miwili. (Fabrizio Romano)

Liverpool wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Sheffield United na Norway Sander Berge, 24 (Yorkshire Post)

Leicester na Everton wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Al Hilal raia wa Brazil Matheus Pereira, 26. (Sun)

Beki wa Tottenham na Uhispania Sergio Reguilon, 25, anatazamiwa kujiunga na Atletico Madrid kwa mkopo bila chaguo la kununua. (Fabrizio Romano)

Kiungo wa kati wa Spurs na England Harry Winks, 26, anakaribia kuhamia Sampdoria baada ya hapo awali kushikilia uwezekano wa kuwindwa na Premier League. (Evening Standard)

Chelsea wameamua mlinzi wao Mwingereza Trevoh Chalobah, 23, hataondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto licha ya kufanya mazungumzo na Inter Milan, AC Milan na RB Leipzig kuhusu uwezekano wa mkataba wa mkopo. (Fabrizio Romano)

Chelsea wanatumai kuwashinda Tottenham na Crystal Palace katika kumsajili beki wa Peterborough Muingereza Ronnie Edwards, 19. (Football Insider)

Spezia wanatazamiwa kumsajili kiungo wa kati wa Wales Ethan Ampadu, 21, kutoka Chelsea kwa mkataba wa mkopo na chaguo la kununua takriban euro 15m (£12.7m). (Fabrizio Romano)