Jinsi rekodi ya dirisha la uhamisho Uingereza ilivyovunjwa

.
Maelezo ya picha, Jinsi klabu za Uingerwza zilivyovunja rekodi ya dirisha la uhamisho mwezi Januari
Iliyochapishwa

Rekodi ya uhamisho ya Uingereza ilivunjwa siku ya mwisho wakati dirisha la uhamisho la Januari ambalo halijawahi kushuhudiwa baada ya kukamilika huku vilabu vya Premier League vikiwa vimetumia £2.8bn msimu wa 2022-23.

Mkataba wa Chelsea wa euro 121m (£107m) kwa kiungo wa kati wa Benfica na Argentina Enzo Fernandez - ukithibitishwa – utajumlisha matumizi ya vilabu vya ligi kuu mwezi Januari hadi kufikia rekodi ya £815m

Zaidi ya pauni milioni 275 zilitumika kwa siku ya mwisho pekee kabla ya dirisha la vilabu vya Uingereza kufungwa saa 23:00 GMT Jumanne usiku.

Matumizi ya siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho yaliongeza 83% kwenye rekodi ya awali ya Januari ya £150m, iliyowekwa mwaka wa 2018.

.
Maelezo ya picha, Uhamisho kwa takwimu

Na, ingawa matumizi ya muda mrefu ya msimu wa juu katika madirisha ya majira ya joto na majira ya baridi yalihakikishwa baada ya rekodi ya £1.9bn kuwekwa mnamo Septemba, jumla ya mwisho ni mara mbili ya rekodi ya awali ya £ 1.4bn mwaka wa 2017.

Rekodi ya msimu wa baridi wa 2018 ya matumizi ya pauni milioni 430 miongoni mwa vilabu vya Ligi Kuu pia ilikuwa tayari imevunjwa kabla ya siku ya mwisho ya Jumanne, na mwishowe mnamo 2023 ongezeko la 90% - na karibu mara tatu ya matumizi ya dirisha lililopita la Januari (£295m), kulingana na kampuni ya huduma za kifedha ya Deloitte.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Utawala wa kifedha wa Ligi ya Premia barani Ulaya uliongezeka hadi kiwango cha juu zaidi kuwahi kuripotiwa, kwani matumizi ya vilabu vya ligi kuu ya Uingereza yalichukua 79% ya jumla ya ligi kuu tano za kandanda za Uropa, ambapo matumizi ya Januari yalipungua kwa 35% kutoka 2022 hadi €255m (£225m).

Hakika, Chelsea walifanya matumizi ua juu zaidi mwezi Januari - karibu £288m - kuliko jumla ya vilabu vyote kwenye ligi ya Ujerumani ya Bundesliga, La Ligaya Uhispania , Serie A ya Itali na Ligue 1 ya Ufaransa.

Miongoni mwa vilabu vya Ligi ya Soka ya Uingereza, matumizi yalipanda hadi £25m, kutoka £20m katika dirisha lililopita la majira ya baridi.

Hata hivyo ni asilimia 3 tu ya jumla ya gharama za vilabu vya Premier League (£25m) zilitumika kupata wachezaji kutoka EFL, huku rekodi ya 85% ikitumika kununua vipaji nje ya Uingereza.

Tim Bridge, mshirika mkuu katika Kundi la Biashara la Michezo la Deloitte, alisema: "Rekodi ya matumizi ya vilabu vya Ligi Kuu msimu huu ni zaidi ya chochote ambacho tumeona hapo awali.

"Klabu za Ligi Kuu ya Uingereza zimetumia zaidi ya matumizi ya ligi kuu tano za Ulaya kwa takriban kiwango cha nne kwa moja katika dirisha hili la usajili, na hivyo kuwaruhusu kuwashikilia wachezaji wao muhimu, huku zikiwavutia wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu kutoka ng'ambo.

"Hata hivyo, ingawa kuna haja ya wazi ya kuwekeza katika ukubwa wa kikosi na ubora ili kuhifadhi makali ya ushindani, daima kutakuwa na uwiano mzuri kati ya kutanguliza mafanikio uwanjani na kudumisha uendelevu wa kifedha.

"Kupungua kwa matumizi katika mfumo wa kandanda ya Uingereza kunaweza kuwa na wasiwasi mkubwa kwa wanachama wa EFL na kunaweza kuchochea mjadala kuhusu matumizi ya fedha kwa usawa zaidi katika piramidi."

Je ni mikataba gani ilioafikiwa katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho ?

.
Maelezo ya picha, Pedro Porro, Jorginho, Marcel Sabitzer, Harry Souttar

Kuchelewa kwa Chelsea kumnasa Fernandez ndio kulikuwa kichwa cha habari siku ya mwisho ambapo The Blues walivunja rekodi ya uhamisho wa Uingereza - hapo awali Manchester City ililipa pauni milioni 100 kwa Jack Grealish mnamo 2021 - kumpata mshindi huyo wa Kombe la Dunia mwenye umri wa miaka 22.

Kwingineko, Tottenham ilitangaza kumsajili beki wa pembeni Pedro Porro kutoka Sporting Lisbon kwa mkopo hadi mwisho wa msimu, akiwa na wajibu wa kumnunua kwa mkataba wa kudumu wa euro 45m (£40m) - huku mabeki Matt Doherty (wa kudumu) na Djed Spence (kwa mkopo) wakiruhusiwa kuondoka.

Viongozi wa Ligi ya Premia Arsenal waliimarika kwa kumnunua kiungo wa kati wa Italia Jorginho kutoka Chelsea kwa pauni milioni 12, huku Manchester United iliyo katika nafasi ya nne ikikamilisha usajili wa mkopo wa kiungo wa Austria Marcel Sabitzer kutoka Bayern Munich.

Southampton walimaliza dirisha hili wakiwa na shughuli nyingi za kuchelewa, na kukamilisha dili la rekodi la klabu la £22m kwa winga wa Ghana Kamaldeen Sulemana pamoja na kumsajili mshambuliaji wa Nigeria Paul Onuachu.

Bournemouth ilimsajili beki wa kati wa Ukraine Illia Zabarnyi kwa kitita cha pauni milioni 24 na kiungo wa kati wa Ivory Coast Hamed Traore kwa mkopo wa awali kabla ya uhamisho wa pauni milioni 20 majira ya kiangazi.

Timu iliopandishwa daraja Nottingham Forest pia ilikuwa na shughuli nyingi, ikikamilisha mikataba ya beki wa Atletico Madrid Mbrazili Felipe na kiungo wa Newcastle Jonjo Shelvey kwa ada ambazo hazijawekwa wazi, huku kipa wa Paris St-Germain Keylor Navas akiwasili kwa mkopo.

Leicester City ilimsajili beki Harry Souttar kutoka Stoke City kwa mkataba ambao unaweza kupanda hadi pauni milioni 20 ikiwa na nyongeza, na Crystal Palace wakamsajili mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Naouirou Ahamada kutoka Stuttgart kwa euro 11m (£9.7m).

Beki wa pembeni wa Manchester City Joao Cancelo alijiunga na Bayern Munich kwa mkopo wa muda wote uliosalia, akiwa na chaguo la euro 70m (£61.5m) kujiunga kabisa msimu wa joto.

Je uhamisho mkubwa wa dirisha la Januari ulikuwa upi?

.
Maelezo ya picha, Mchezaji wa Chelsea Mudryk na mwenzake wa liverpool Gapko

Mkataba wa Chelsea kwa Fernandez ulikuwa mwisho mwafaka kwa dirisha lingine la kushangaza. Huku kukiwa na msururu mwingine mzuri wa matumizi, The Blues walikubali mkataba wa £89m na Shakhtar Donetsk kumnunua fowadi wa Ukraine mwenye umri wa miaka 22 Mykhailo Mudryk mapema Januari.

Mbali na siku ya mwisho ya kumsajili Jorginho, Arsenal ilimsajili mshambuliaji wa Ubelgiji Leandro Trossard kutoka Brighton kwa £21m pamoja na nyongeza, pamoja na Jakub Kiwior kutoka Spezia ya Serie A kwa euro 20m (£17.6m).

Kwingineko, Liverpool ilikubali dili la thamani ya euro 40-50m (£35.4m-£44.3m) kumsajili fowadi wa Uholanzi Cody Gakpo, 23, kutoka klabu ya Uholanzi PSV Eindhoven.

Na usajili wa Newcastle United wa Anthony Gordon mwenye umri wa miaka 21 kutoka Everton unaweza kuwa na thamani ya £45m.

Kulikuwa na pesa nyingi zilizotumika kati ya timu za sasa za ligi zilizo mkiani pia, huku Leeds United ikisajili fowadi Mfaransa Georginio Rutter, 20, kutoka Hoffenheim kwa rekodi ya klabu ya euro 40m (£36m).

Bournemouth pia ilimsajili winga wa Burkina Faso Dango Ouattara kutoka Lorient kwa takriban £20m na Leicester ikalipa £17m kumnunua beki Victor Kristiansen.

Kufuatia mauzo ya Danny Ings kwa £15m kwenda West Ham, Aston Villa ilimsajili mshambuliaji chipukizi wa Colombia Jhon Duran kutoka Chicago Fire kwa £18m.

Chelsea ilitawala dirisha la uhamisho la mwezi Januari EPL

Iimekuwa dirisha la ajabu kwa uhamisho wa Chelsea tangu klabu hiyo ilipouzwa kwa pauni bilioni 4.25 kwa muungano unaoongozwa na mwekezaji Mmarekani Todd Boehly mwezi Mei mwaka jana.

Na ilionekana hivyo hata kabla ya kiasi cha kuvutia cha fedha kubalika na Benfica kwa Fernandez muda wa mwisho wa siku ya mwishoya uhamisho.

Ni kauli ya hivi punde ya ari katika siku za mwanzo za enzi mpya ya Chelsea chini ya Boehly, ambaye ametumia zaidi ya pauni milioni 550 kusajili wachezaji wapya.

Matumizi yao Januari pekee yalizidi £300m kununua wachezaji wanane wapya, Mudryk, Malo Gusto (£30.7m), Benoit Badiashile (£35m), Noni Madueke (£30.7m), Andrey Santos (£18m) na David Datro Fofana ( £8m-£10m) wote wakiwekwa katika mikataba ya kudumu.

Wakati huo huo, fowadi wa Ureno mwenye talanta, 23, Joao Felix alihamia Stamford Bridge kwa mkopo kutoka Atletico Madrid kwa gharama ya euro milioni 11 (£9.7m).

Hilo lilikuja baada ya majira ya kiangazi ambayo yaliwashuhudia wakitumia rekodi ya Ligi Kuu ya Uingereza £270m - ikiwa ni klabu ya kote duniani kufanya hivyo baada ya Real Madrid iliotumia (£292m) mwaka 2019.

Kwa jumla, Chelsea ilichangia 37% ya pesa zote zilizotumiwa na vilabu vya Premier League mnamo Januari.

.
Maelezo ya picha, Takwimu za matumizi ya ligi ya Premia

Ligi kuu barani Ulaya imewasili – na iko nchini England

Mwanahabari wa kandanda wa Uhispania Guillem Balague kwenye kipindi cha Kandanda cha kila siku cha BBC Radio 5 Live

[Matumizi ya Chelsea] ni ya kuvutia, sivyo. Kitu kinachosema kuwa Ligi Kuu ya Ulaya imefika...na makao yake makuu yapo nchini Uingereza. Hapa ndipo wasimamizi wanataka kuwa na pale ambapo wachezaji wanataka kuwa.

Kilichotokea kwa kesi ya Mykhailo Mudryk, ambapo Chelsea waliongeza mara mbili ya mishahara ambayo Arsenal walikuwa wakitoa, jambo la aina hiyo linaweza kutokea England pekee.

Hakuna kurudi nyuma. La Liga inafanya juhudi kubwa kuongeza uwezo wa ushindani, lakini bado iko maili mbali na Ligi Kuu.

Ni jambo ambalo watu wanapaswa kukubali na kuzoea. Ikiwa ni kweli kwamba kila wakati unapokuza mchezaji mwenye ubora kidogo anaenda Ligi Kuu, endelea.

Kuna idadi ndogo ya wachezaji unaoweza kusajili, licha ya kile Chelsea wanachofanya, kwa hivyo, ndio, ligi zingine za Uropa zinahitaji kujiuza kwa njia tofauti.

Mikataba ya Januari ambayo haikufua dafu

Licha ya pesa zote zilizotumika, sio kila mtu alipata alichotaka.

Pendekezo la siku ya mwisho la fowadi wa Morocco Hakim Ziyech kuhama kutoka Chelsea kwenda PSG lilionekana kuporomoka huku mchezaji huyo akisubiri jijini Paris kwa sababu hati za kukamilisha uhamisho huo hazikuwasilishwa kwa wakati.

Arsenal ilikataliwa dau la pauni milioni 60 na Brighton katika harakati zao za kumnasa kiungo Moises Caicedo, licha ya kiungo huyo kuthibitisha nia yake ya kuondoka klabuni hapo kwa barua ya wazi kwenye Instagram yake. Hayo yamejiri baada ya The Gunners kushindwa kumsajili Mudryk aliyehamia Chelsea.

Kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher aliamua kusalia Stamford Bridge licha ya Everton wanaohangaika katika Ligi ya Premia.

Hakika, licha ya kumteua bosi wa zamani wa Burnley Sean Dyche kama meneja mpya wa klabu siku ya Jumatatu, Toffees walio katika nafasi ya 19 hawakufanya biashara yoyote siku ya mwisho ya dirisha la usajili.