Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uchaguzi Kenya 2022: 'Lazima tupige kura'
Zaidi ya wapiga kura milioni 22 wanatarajiwa kushiriki kupiga kura kumchagua Rais wa tano wa Kenya, pamoja na viongozi wengine wa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Ikiwa ni chini ya saa 24 kabla ya zoezi hilo kuanza, wengi wamejitokeza katika vituo vya kupigia kura ili kuthibitisha kuwa majina yao yapo katika sajili ya wapiga kura.
Hatua hiyo inajiri baada ya tume ya uchaguzi kuamrisha kutumika kwa daftari la usajili wa wapiga kura
Mwanahabari wetu Roncliffe Odit alikutana na baadhi ya wakazi wa Kisumu wakitafuta majina yao katika Shule ya Msingi ya Pandpieri, eneo bunge la Kisumu ya Kati.