Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Waziri wa ulinzi wa Ukraine: Sisi ni mwanachama halisi wa muungano wa Nato
Ukraine imekuwa mwanachama wa ukweli wa muungano wa Nato, waziri wa ulinzi wa Ukraine anasema, huku nchi za Magharibi, zilizowahi kuwa na wasiwasi kwamba msaada wa kijeshi unaweza kuonekana kama kuongezaa mvutano na Urusi, zikibadilisha fikra .
Katika mahojiano na BBC, Oleksii Reznikov alisema ana uhakika Ukraine itapokea silaha zilizotafutwa kwa muda mrefu, ikiwa ni pamoja na vifaru na ndege za kivita, kwani Ukraine na Urusi zinaonekana kujiandaa kwa mashambulizi mapya katika majira ya kuchipua.
"Wasiwasi huu juu ya kiwango kinachofuata cha kuongezeka kwa mzozo, kwangu, ni aina fulani ya itifaki," Bw Reznikov alisema.
"Ukraine kama nchi, na vikosi vya kijeshi vya Ukraine, vikawa [a] mwanachama wa Nato. Kikweli , na sio (kwa sheria). Kwa sababu tuna silaha, na ufahamu wa jinsi ya kuzitumia."
Rais wa Urusi Vladmir Putin ametaja uvamizi wake nchini Ukraine kama vita vilivyopo dhidi ya nchi za Magharibi zinazotaka kuidhoofisha Urusi.
Viongozi wa Urusi wamedai kuwa wanapambana na Nato nchini Ukraine, kwani nchi za Magharibi zimeipatia nchi hiyo silaha katika kile wanachoita vita vya uchokozi.
Ukraine, kwa miaka mingi, imekuwa ikitaka kujiunga na muungano wa kijeshi kati ya Marekani, Kanada na nchi 28 za Ulaya, jambo ambalo Rais Vladimir Putin ameeleza kuwa ni tishio la usalama kwa Urusi.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameshinikiza kusajiliwa kwa haraka, lakini haijulikani kama uanachama kamili ni jambo ambalo wanachama wa muungano watalizingatia kwa uzito hata baada ya vita kumalizika, licha ya ahadi za kuungwa mkono.
Kifungu cha 5 cha Mkataba wa Nato kinasema shambulio la silaha dhidi ya mwanachama yeyote linapaswa kuchukuliwa kuwa shambulio dhidi ya wote.
Bw Reznikov, hata hivyo, alikanusha kuwa maoni yake yataonekana kuwa ya utata, sio tu na Urusi lakini, labda, na Nato yenyewe, kwani muungano huo umechukua hatua kutoonekana kama sehemu ya mzozo.
"Kwa nini [ingekuwa] na utata? Ni kweli. Ni ukweli," Bw Reznikov alisema. "Nina uhakika kwamba katika siku za usoni, tutakuwa wanachama wa Nato, kihalisia."
Waziri wa ulinzi alizungumza katika mji mkuu wa Kyiv, wakati vikosi vya Ukraine na Urusi vikiendelea kupigania mji mdogo wa Soledar, eneo la mashariki la Donetsk, katika baadhi ya vita vikali zaidi katika vita vilivyodumu kwa takriban miezi 11.
Mashambulizi ya Urusi yanaongozwa na kundi la mamluki la Wagner, ambalo mwanzilishi wake Yevgeny Prigozhin, mshirika wa muda mrefu wa Putin, amekuwa mkosoaji mkubwa wa operesheni za jeshi la Urusi nchini Ukraine.
Siku ya Jumanne, Bw Prigozhin alidai kwamba wapiganaji wake waliudhibiti mji huo, madai ambayo yalikataliwa na Ukraine na, cha ajabu, na Kremlin, katika kile kilichochukuliwa kuwa ni kumpinga Bw Prigozhin.
Hali katika Soledar ilikuwa "ngumu sana", Bw Reznikov alisema, lakini "chini ya udhibiti". Alisema wapiganaji wa Wagner walikuwa wakitumiwa katika "wimbi baada ya wimbi baada ya wimbi" la mashambulizi, na kusababisha idadi kubwa ya vifo, na kwamba Bw Prigozhin anavutiwa na faida za kiuchumi za kuuteka mji huo, nyumbani kwa migodi mikubwa ya chumvi barani Ulaya.
"Watapata pesa kutokana na damu," alisema.
Soledar iko takriban kilomita 10 (maili sita) kutoka Bakhmut, mji wa kimkakati ambapo vikosi vya Ukraine na Urusi vimekuwa vikishiriki katika vita vya miezi kadhaa ambavyo vimesababisha uharibifu mkubwa na hasara kubwa kwa pande zote mbili. Huko, mamluki wa Wagner pia wametumwa kwa wingi, na Bw Prigozhin anaaminika kuwa amefanya kutekwa kwa Bakhmut kuwa lengo la kibinafsi.
Kundi hilo, Bw Reznikov alisema, "linahitaji kutoa uthibitisho wa aina fulani ili kutangaza kuwa wao ni bora kuliko vikosi vya kawaida vya kijeshi vya Shirikisho la Urusi". Iwapo itakamatwa, Bakhmut anaweza kufungua njia kwa msukumo wa Urusi kuelekea Kramatorsk na Sloyansk, ngome mbili za Ukraine huko Donetsk, eneo ambalo limekuwa shabaha kuu ya Rais Putin.
Mafanikio yoyote yatakuwa, zaidi ya kitu kingine chochote, ya thamani kubwa ya kielelezo kwa Urusi. Yatakuja baada ya msururu wa vikwazo vya kufedhehesha, ikiwa ni pamoja na kutoroka kwa machafuko kutoka eneo la kaskazini-mashariki la Kharkiv na kujiondoa katika mji wa kusini wa Kherson, mji mkuu wa kikanda pekee majeshi ya Urusi yaliuteka katika vita.
Bw Reznikov alidai kuwa "takriban wapiganaji 500 au 600" wa Urusi walikuwa wakiuawa kila siku kote nchini, huku Ukraine ikipoteza sehemu ya kumi kati ya hizo, takwimu ambazo hazingeweza kuthibitishwa kwa uhuru. Aliamini kuwa Urusi inaweza kuwa inajaribu kukusanya "vikosi, risasi na silaha" kwa ajili ya mashambulizi kutoka maeneo ambayo tayari inamiliki kusini na mashariki.
Ukraine, wakati huo huo, ilihitaji muda wa kujipanga upya na kujitayarisha huku ikisubiri kukabidhiwa kwa silaha za Magharibi. "Msimu ujao ni kipindi bora cha kuanzisha harakati kwa pande zote," alisema. "Tunaelewa watakuwa tayari kuanza na, hakika, lazima tuwe tayari kuanza."
Hata hivyo, hakurudia madai kwamba Urusi inaweza kuandaa uvamizi mwingine kutoka Belarus, onyo ambalo limetupiliwa mbali na mkuu wa shirika la kijasusi la kijeshi la Ukraine. Harakati kutoka kaskazini, Bw Reznikov alisema, "itachukua muda mwingi na wao [Urusi] hawana rasilimali".
Bw Reznikov alizungumza siku moja baada ya wizara ya ulinzi ya Urusi kuchukua kubadilisha kamanda wa vikosi vyake nchini Ukraine, tangazo la kushangaza ambalo lilionekana kuwa ishara ya mzozo wa madaraka. Jenerali Valery Gerasimov, mmoja wa waanzilishi wa uvamizi wa mwaka jana, amerudi kwenye wadhifa uliokuwa ukishikiliwa na Jenerali Sergei Surovikin, ambaye alikuwa ameteuliwa Oktoba.
Mabadiliko hayo, Bw Reznikov alisema, yalitokana na "mgogoro kati ya Bw Prigozhin na vikosi vya kijeshi vya Shirikisho la Urusi". Jenerali Surovikin alisimamia mashambulio ya kikatili ya hivi majuzi dhidi ya miundombinu ya nishati ya Ukraine ambayo, kulingana na Bw Reznikov, "yalipunguza hifadhi ya [kombora la Urusi] bila matokeo yoyote", akirudia dai la Ukraine kwamba "yanaishiwa na makombora".
Wakati Poland na Uingereza zikifichua mipango ya kuwasilisha vifaru vya vita kwa mara ya kwanza, Bw Reznikov alisema ana uhakika kwamba Ukraine itapokea "vifaru, ndege za kivita na silaha za masafa marefu kulenga shabaha katika kilomita 300 (maili 186) pia" kwa sababu "mambo yalikuwa yakibadilika" katika nchi za Magharibi.
Alipuuzilia mbali wasiwasi kwamba matangazo hayo yanaweza kusababisha jibu la Urusi, licha ya vitisho vinavyojulikana sasa kutoka kwa Moscow. "Nina vita katika nchi yangu," alisema. "Wanapiga miji yangu, hospitali yangu, shule zangu za chekechea, shule zangu. Waliua raia wengi, wengi sana. Ni jeshi la wabakaji, wauaji na waporaji. Je! ni hatua gani inayofuata ya kuongezeka?"