Maelezo ya picha, Jane Birkin kama muigizaji mchanga, hapa ilikuwa London, Septemba 1964
Iliyochapishwa
Mwimbaji na mwigizaji Jane Birkin aliyefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 76, alikuwa na asili ya Uingereza na alifanya shughuli zake zaidi nchini Ufaransa.
Aljulikana kwa uhusiano wake wa kikazi na wa kibinafsi na mwanamuziki Serge Gainsbourg na alichukuliwa kuwa mtu maarufu na wakuigwa mwishoni mwa miaka ya 1960 na 1970.
Vyombo vya habari vya Ufaransa viliripoti kwamba alikutwa amekufa nyumbani kwake huko Paris. Picha hizi zinaonyesha sehemu ya maisha yake.
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Birkin akiwa na Gainsbourg, jijini London mwaka wa 1977, walikuwa na uhusiano wenye misukosuko ambao inasemekana kulikua na ujeuri ndani yake, lakini alimtetea mara kwa mara.
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Birkin na Gainsbourg walikuwa na binti mmoja waliozaa, Charlotte (kushoto), na mwimbaji huyo alikuwa na binti mwingine, Kate (katikati), aliyezaa na mtunzi wa Uingereza John Barry. Alikuwa na mtoto mwingine wa tatu, Lou, (hayupo pichani) aliyezaa na mkurugenzi wa filamu wa Ufaransa Jacques Doillon
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Picha hii alipiga mwaka 1985
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Birkin pichani ilikuwa mwaka 1992 akiwa na mabinti zake wawili, Charlotte Gainsbourg (kushoto) na Lou Doillon (kulia), ambao pia walikuja kuwa waimbaji na waigizaji.
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Birkin, aliyekuwa mwanaharakati pia wa kutetea demokrasia, alitembelea moja ya makambi huko Myanmar, mwaka 2010