Siri ya kiumbe asiye na njia ya haja kubwa yafichuliwa

Iliyochapishwa

Wanasayansi wanasema wametatua fumbo linalohusishwa  na kiumbe chenye hadubini mwenye umri wa miaka milioni 500 na mwenye mdomo lakini hana njia ya haja kubwa.

Ilipogunduliwa mnamo 2017, iliripotiwa kuwa mabaki madogo ya mnyama huyu wa baharini anayefanana na gunia yanaweza kuwa ya zamani zaidi ya wanadamu.

Mnyama wa kale, Saccorhytus coronarius, aliwekwa katika kundi linaloitwa deuterostomes.

Hawa ndio mababu wa zamani wa wanyama wenye uti wa mgongo - ikiwemo wanadamu.

Utafiti mpya sasa unapendekeza kwamba Saccorhytus anapaswa kuwekwa katika kundi tofauti kabisa la wanyama.

Timu ya watafiti nchini China na Uingereza ilifanya uchunguzi wa kina wa X-ray wa kiumbe huyo, na kuhitimisha kuwa ni wa kikundi kinachoitwa ecdysozoans - mababu wa buibui na wadudu.

Chanzo kimoja cha mkanganyiko huu ilikuwa ukosefu wa haja kubwa

"Chaguo moja la kufurahisha", alisema, ni kwamba babu wa awali wa kundi hili lote hakuwa na njia ya haja kubwa, na kwamba Saccorhytusa walijitokea baada ya hapo.

"Inawezekana kuwa aliipoteza njia hiyo wakati wa mabadiliko  yake - labda hakuihitaji kwa sababu anaweza kukaa katika sehemu moja na kutumia njia moja  kwa kila kitu."

Sababu kuu ya mabadiliko hayo  ya Saccorhytus kwenye mti wa uzima wa Cambrian ni kwamba, kwenye uchunguzi wa awali, mashimo yaliyozunguka kinywa chake yalitafsiriwa kama mashimo madogo ya kupumulia - kipengele cha awali cha deuterostomes.

Wakati wanasayansi walipoichunguza kwa kina  kwa kutumia kifaa cha X-ray chenye uwezo mkubwa ili kumchunguza kiumbe huyo mwenye ukubwa wa milimita moja kwa ukaribu zaidi – waligundua kwamba ilikuwa chanzo cha miiba iliokuwa imetoka.

Wanasayansi wanaosomea mabaki hayo, walijaribu kumuweka kila mnyama katika mti wa uzima – ili kujaribu kuelewa wanakotoka na walivyoibuka

‘’Saccorhytus wangeishi baharini  - kwenye mchanga na miiba yake ikamsaidia kujidhibiti’’,  alielezea Bi Carlisle, ambaye anaishi katika Chuo Kikuu cha Bristol.

Miamba iliyo na  hivi vya Cambrian bado inachunguzwa.

"Kuna mengi bado tunaweza kujifunza kuhusu mazingira yake," Bi Carlisle aliongeza.

"Kadiri ninavyosoma palaeontolojia, ndivyo ninavyogundua ni kiasi gani kinakosekana. Kwa upande wa kiumbe hiki na ulimwengu alichoishi, kwa kweli tunajikuna tu."