Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Liverpool, Madrid zamgombania Wharton
Crystal Palace hawana mpango wa kumuuza kiungo wa kati wa Uingereza Adam Wharton, 21, katika dirisha la uhamisho la Januari, huku Liverpool na Real Madrid zikiwania saini yake. (Football Insider)
Beki wa Bayern Munich Mfaransa Dayot Upamecano, 26, anataka kuhamia Real Madrid mkataba wake utakapokamilika msimu ujao. (Marca - kwa Kihispania)
Tottenham Hotspur ina nia ya kubadilisha mkataba wa mkopo wa kiungo wa kati wa Ureno Joao Palhinha, 30 kutoka Bayern Munich kuwa wa kudumu mwezi Januari. (TBR Football)
Klabu ya Chelsea imefufua tena azma ya kumsajili kipa wa Ufaransa na AC Milan Mike Maignan, 30, na huenda ikamjumuisha kwenye orodha ya uhamisho katika dirisha lijalo la usajili wa wachezaji baada ya kipa wake wa sasa Mhispania Robert Sanchez, 27, kutofanya vizuri katika mechi yao dhidi ya Manchester United siku ya Jumamosi. (Daily Express)
Mkufunzi wa Brighton Fabian Hurzeler amemtaka kiungo Carlos Baleba kusalia licha ya tetesi kuibuka kwamba anandoka, huku Manchester United ikiwa na nia ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Cameroon mwenye umri wa miaka 21 msimu wa kiangaza. (Daily Mirror)
Everton wanafikiria kumsajili mchezaji huru Sergio Reguilon, 28, lakini beki huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur anasemekana kupendelea kurejea katika nchi yake ya Uhispania. (Football Insider)
Ruben Vargas wa Sevilla, 27, atasalia kwenye rada za Spurs iwapo wataamua kutafuta winga mwezi Januari. Kocha Thomas Frank huenda akazingatia usajili wa kiungo wa kati, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Uswizi ana nafasi nzuri zaidi. (Football Insider)
West Ham Unitedimeanza kumsaka mkufunzi mpya huku shinikizo la kumtaka Graham Potter kuondoka likiongezeka baada ya kushindwa Jumamosi na Crystal Palace. (Sky Sports)
Klabu za ligi kuu ya England kama vile Liverpool, Manchester United na Chelsea zina nia ya kumsajili beki wa Juventus na Brazil Gleison Bremer, 28. (Team Talk)