Darya Dugina: Kinachojulikana kuhusu mauaji ya binti wa mwandani wa Rais Putin

Darya Dugina

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Bi Dugina alikuwa mgeni wa kawaida kwenye habari za runinga za Urusi
Iliyochapishwa

Hili ni shambulio ambalo limeshangaza wengi na kuibua maswali mengi nchini Urusi.

Darya Dugina alikuwa binti wa mwanafalsafa wa Kirusi Alexander, ambaye anafahamika kama 'mshirika' wa Rais Vladimir Putin. Kwa mujibu wa Kamati ya Upelelezi ya Urusi, Darya Dugina alifariki dunia alipokuwa akielekea nyumbani kwake kwenye gari lake wakati gari lake lilipodaiwa kulipuka.

Maafisa wa Urusi wanasema kuwa baba yake, Alexander Dugin, huenda alikuwa mlengwa mkuu wa shambulio hilo lililotokea Jumamosi usiku karibu na Moscow.

Kuna dalili kwamba shambulio hilo lilipangwa. Vilipuzi vilivyowekwa chini ya gari la Alexander Dugin vililipuka.

Gari lililipuka karibu na kijiji cha Bolshiye Vyazemy.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Gari lililipuka karibu na kijiji cha Bolshiye Vyazemy.

Wakati huduma za dharura zilipofika eneo hilo, gari la Dugina liliungua. Mwanafalsafa Dugin alionekana kushtuka sana baada ya kuona picha zilizowekwa kwenye mtandao wa Telegram.

Urusi inaishutumu Ukraine, ambayo inakanusha kuhusika kwa vyovyote vile

Urusi siku ya Jumatatu iliishutumu Ukraine moja kwa moja kwa kupanga mauaji hayo.

Idara ya Usalama ya Shirikisho la Urusi (FSB) ilisema imesuluhisha kesi hiyo na kwamba idara za ujasusi za Ukraine ziliajiri mwanamke ambaye aliwasili Urusi katikati ya Julai na binti yake mdogo.

Ukraine hata hivyo ilikanusha kuhusika na shambulio hilo.

Mamlaka ya Ukraine imetupilia mbali shutuma hizo, ikisema shambulio hilo linahusiana na kisiasa za ndani za nchini Urusi.

‘’Ukraine, bila shaka, haina uhusiano wowote na hili, kwa sababu sisi si taifa la uhalifu kama Shirikisho la Urusi, na pia sisi sio taifa la kigaidi,’’ alisema Mykhailo Podolyak, mshauri wa Rais Volodymyr Zelensky.

FSB inadai kuwa mwanamke huyo alikodi nyumba katika jengo moja na Dugina ili kupata habari kuhusu maisha yake.

Shirika hilo la usalama pia lilisema washukiwa hao walitumia gari aina ya Mini Cooper lililokuwa na nambari tatu tofauti za usajili.

Mshukiwa alitorokea Estonia baada ya mlipuko huo, FSB ilisema.

Idara ya usalama ya Urusi, FSB, iliripoti kwamba raia wa Ukraine ambaye aliwasili nchini mnamo Julai alikuwa nyuma ya shambulio hilo.

BBC haiwezi kuthibitisha madai kama hayo kwa uhuru.

Uvumi

Kifo cha Dugina kilizua wimbi la uvumi nchini Urusi kuhusu historia na matokeo ya uhalifu huu, idhaa ya BBC ya Urusi iliripoti.

Ilya Ponomarev, mbunge wa zamani wa Urusi, alisema siku ya Jumapili kwamba makundi ya ndani yanayompinga Putin ndiyo yalihusika na mauaji hayo.

Kwa upande mwingine, wapinzani wa mawazo ya Dugin wanadokeza ushiriki wa huduma maalum za Kirusi, ingawa hawajatoa uthibitisho wowote.

Darya Dugina ameelezea mara kwa mara uungaji mkono wake kwa serikali ya Urusi nchini Ukraine.

Chanzo cha picha, DARIA DUGINA

Maelezo ya picha, Darya Dugina ameelezea mara kwa mara uungaji mkono wake kwa serikali ya Urusi nchini Ukraine.

Matukio kama haya yatawatia wasiwasi maafisa wa Moscow, haswa baada ya msururu wa milipuko na mashambulio kwenye rasi ya Crimea - iliyotwaliwa na Urusi mnamo 2014 - na katika mikoa ya Urusi karibu na mpaka wa Ukraine.

Propaganda ya Kremlin inasisitiza mara kwa mara jinsi Vladimir Putin alivyoleta usalama na utulivu kwa Urusi baada ya miaka ya 1990 yenye misukosuko, wakati mabomu ya magari na mauaji yalikuwa mambo ya kawaida.

Bomu hili la gari katika mji mkuu wa Urusi linadhoofisha maneno hayo.

 

Uvumi kila mahali, Uchambuzi na Will Vernon, mwandishi wa BBC mjini Moscow

Uvumi kila mahali, Uchambuzi na Will Vernon, mwandishi wa BBC mjini Moscow

Ingawa Aleksandr Dugin sio afisa wa serikali, yeye ni mtu wa kupigiwa mfano katika siasa za Urusi.

Falsafa yake ya uzalendo wa hali ya juu, dhidi ya Magharibi imekuwa itikadi kuu ya kisiasa nchini Urusi na imesaidia kuunda sera ya nje ya Rais Putin ya kujitanua, haswa nchini Ukraine.

Tahadhari sasa itaelekezwa kwa nani alikuwa nyuma ya shambulio hili.

Denis Pushilin, ‘’kichwa’’ cha Jamhuri ya Watu wa Donetsk’’. Iliyojitangazia uhuru wake, inayounga mkono Urusi, tayari ameilaumu Ukraine, akiandika kwenye Telegraph: ‘’Wabaya wabaya! Magaidi wa serikali ya Kiukrene, wakijaribu kumuondoa Alexander Dugin, wamlipua binti yake ... akiwa ndani yatika gari. Tunasherehekea kumbukumbu ya Darya, yeye ni binti wa kweli wa Urusi!

Vikwazo dhidi ya mwandishi

ALEXANDER DUGIN

Chanzo cha picha, ALEXANDER DUGIN

Maelezo ya picha, ALEXANDER DUGIN

Ingawa Aleksandr Dugin hana nafasi rasmi ya serikali, yeye ni mtu wa kupigiwa mfano katika siasa za Urusi.

Mwezi Mei, Dugina alielezea vita hivyo katika mahojiano kama ‘’mgongano wa ustaarabu’’ na alionyesha kiburi kwamba yeye na baba yake walikuwa wameidhinishwa na Magharibi.

Alexander Dugin aliwekewa vikwazo na Marekani mwaka 2015 kwa madai ya kuhusika katika kunyakua Crimea kwa Urusi.

Maandishi yake yanasifiwa kuwa na ushawishi mkubwa katika mtazamo wa ulimwengu wa Vladimir Putin na anachukuliwa kuwa mmoja wa wasanifu wakuu wa itikadi ya utaifa iliyopendekezwa na wengi huko Kremlin.

Kwa miaka mingi, Dugin ametoa wito kwa Moscow kujisisitiza kwa ukali zaidi kwenye jukwaa la dunia ana ameunga mkono hatua ya kijeshi ya Urusi nchini Ukraine.